Mahakamani 28 Septemba: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Mahakamani 28 Septemba: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Kutoka mahakama kuu ya Tanzania, masjala ndogo jijini Dar es Salaam, kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA dhidi ya Jamhuri inaendelea.

Tayari mshtakiwa Tundu Lissu ameshawasili mahakamani

Kaa tayari kwa updates

=====

Leo September 28, 2026

Last time tuliishia 467

Sehemu ya 468

Imepigwa high court Majaji wameingia na kwenda kuketi kwenye viti vyao, wapo watatu kama kawaida yao.

Mwenyekiti Lissu nae pia ameingia.

Mawakili wa Serikali wao waliingia kabla Majaji hawajaingia.

Karani kasoma kesi number ___ Jamhuri vs Tundu Lissu.

Anasimama Katuga yuko na wenzake anawatambulisha wenzake kwa majina yao, mmoja mmoja.

Anasema wao wako tayari kama na mwenzao yaani Tundu Lissu atakuwa tayari basi hawana Pingamizi.

Mhe. LISSU amesimama anasema kabla sijazungumza ya leo naomba niseme mambo yafuatayo. Kwa vile nategemea kumaliza leo nisipoyasema sasa hivi pengine sitayasema tena na sitapata nafasi ya kuzungumza.

Jaji Ndunguru anasema kwanini usiendelee na kutoa hoja zako halafu utasema baadae.

Mhe. Lissu anasema hilo nalo neno, sasa hoja ya neno kwa kuzingatia majibu ya hoja 7 zilizotangulia upande wa Mashitaka umethibitisha mashitaka yake kwa kiwango cha uthibitisho kinachotakiwa na Sheria? Kiwango cha uthibitisho kinachotakiwa na Sheria katika kesi za jinai kama hii ni uthibitisho usiokuwa na shaka yoyote ya msingi.

Proof beyond any reasonable doubt. Kwa kesi za jinai kama hii kwa mujibu wa kifungu cha 3(2)(a) cha Sheria ya Ushahidi. Hicho ndicho walichotakiwa kuthibitisha upande wa mashitaka bila kuacha shaka yoyote ya msingi.Katika maswali 7 niliyouliza na kupendekeza muyatafakari kwenye maswali yote 7 upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha hayo maswali 7 na ushahidi uliopo nao pia umeshindwa kabisa kuthibitisha maswali hayo saba na kesi iliyopo mahakamani.

Swali la kwanza lilikuwa kama mshitakiwa ndo aliyeitisha, kuandaa mkutano wa Tarehe 03/04/2025 ambako maneno yanayodaiwa yalisemwa huko kwenye swali hili upande wa mashitaka umeshindwa na hauwezi kuthibitisha kwamba Mshitakiwa ndo aliyeandaa wala kuitisha huo mkutano.???

Swali la pili lilikuwa kama mshitakiwa ndo aliyewaalika waandishi wa Habari kwenye huo Mkutano wa tarehe 03/04/2025? Kwenye hili swali vilevile upande wa mashitaka umeshindwa na kwa ushahidi uliopo mahakamani hauwezi kuthibitisha kuwa mimi ndie niliyealika waandishi wa Habari kwenye mkutano huo? Swali la tatu lilikuwa kama mshitakiwa aliunda nia ya kuchochea mtu au kikundi cha watu kuzuia Uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Waheshimiwa Majaji kwenye swala hili la tatu, upande wa mashitaka umeshindwa kabisa na kwa ushahidi uliopo Mahakamani hauwezi kuthibitisha tuhuma zilizopo Mahakamani kwamba mshitakiwa alitengeneza ya kuchochea mtu au kikundi cha watu kwa lengo la kuitishia serikali.

Swali la nne lilikuwa kama maneno yanayodaiwa kutamkwa na mshitakiwa yanategengeneza kosa lolote linalojulikana na Sheria za Tanzania? Kwenye swali hili la nne upande wa mashitaka umeshindwa kabisa na kwa ushahidi uliopo hauwezi kuthibitishwa kwani maneno yale hayatengenezi kosa lolote kwenye sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Swali la tano lilikuwa kama maneno yanayodaiwa kutamkwa na mshitakiwa ni matendo kwa mujibu wa kifungu cha 29(2)(d) cha Penal Code?

Kwenye swali hili la tano upande wa mashitaka umeshindwa kabisa na kwa ushahidi ulioko Mahakamani hauwezi kuthibitisha maneno kuwa ni matendo. Maneno sio matendo kabisa na kwa ushahidi uliopo hawawezi kuthibitisha hilo. Swali la sita lilikuwa kama mshitakiwa ndo aliyechapisha maneno anayolalamikiwa kwamba alichapisha kwenye mtandao wa YouTube wa Jambo TV?

Kwenye swali hili la 6 umeshindwa kabisa na kwa ushahidi uliopo Mahakamani hauwezi kuthibitisha kwamba mimi mshitakiwa ndio niliyechapisha hizo video kwenye mtandao wa Youtube wa Jambo TV. Swali la 7 lilikuwa kama Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika kutokana na maneno yanayodaiwa kuwa ya kihaini?

Sehemu ya 469

Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission) Mhe. Lissu anasema, Upande wa mashitaka umeshindwa kabisa na wala hawakujaribu kuthibitisha kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika kutokana na hayo maneno na kwa ushahidi waliouleta tuhuma hiyo haiwezi kuthibitishwa. Kwahiyo Waheshimiwa Majaji kwenye maswali yote 7 upande wa mashitaka umeshindwa kabisa na kwa ushahidi uliopo Mahakamani hauwezi kuthibitisha tuhuma yoyote ile dhidi ya mshitakiwa kwa kiwango cha uthibitisho kinachotakiwa na sheria yaani uthibitisho bila kuacha shaka yoyote.

Sasa Waheshimiwa Majaji. Je ni hayo tu? Upande wa mashitaka umeshindwa na hauwezi kuthibitisha? Ninachotaka kusema kwa ushahidi ulioko Mahakamani kuna masuala mengine yaliyojitokeza na ambayo yametolewa ushahidi yanayothibitisha kuwepo kwa mashaka makubwa na ya msingi juu ya kesi yote ya upande wa Mashitaka, mashaka makubwa na ya msingi. Waheshimiwa Majaji eneo la kwanza linaloonesha mashaka makubwa. Ni kwamba kesi hii yote imetengenezwa na mtu mmoja pengine wawili, underline neno pengine.

Kesi yote hii imetengenezwa na mtu mmoja au wawili. Ushahidi unasemaje kuhusu hili? Huyo mtu ni nani na ushahidi ukoje nianzie hapo??Huyu Mtu ni Shahidi namba 1 George Wilbard Bagyemu, huyu ndo aliyeamua ku determine kuwa hayo maneno yanatengeneza kosa la Uhaini, ni yeye peke yake.?Nawaalikeni records ya Mahakama ukurasa wa 145 hadi 146. Yeye anasema hivi "On 7th april 2025 in the morning i instructed Assistant Insp. Michael to Open two diffrent case files. One for the treason and the second for publication of false infirmation. That order complied with. Treason case opened with no.....

Kwahiyo yeye ndio alimuaru Michael kufungua file la Uhaini na hiyo aliifanya siku nne tu baada ya kuwa ameonyeshwa ile video ya Uhaini katika hizo siku nne hakufanya yafuatayo; a) PW1 hakuomba Mwongozo wala maekekezo kutoka kwa wakubwa wake wa kazi kabla hajafungua file la Uhaini. Hakuuliza jamani nifanyaje na hii kitu? Hakuomba guidance from any of his superiors.

Nilimuuliza ulitoa taarifa kwa ZPC akasema hapana, huyo ZPC kamanda wa Polisi wa Kanda ndo mkubwa wake na Boss wake kiutendaji. Je aliomba guidance kwa Ramadhani Kingai ambae ni DCI hata huko hakuomba. Baada ya kufungua file la Uhaini akasema yafuatyo ; I formed Investigation team and then communicated with DCP Ng'anzi and informed him about opening the treason file and he told me that he add DCP Amin Mahamba as part of the investigating team.

Kwahiyo hakuomba mwongozo kwa mkubwa wake yoyote. Ukurasa wa 158 wa record ndio ushahidi wa kwamba hakuomba ushauri kwa yeyote. b) PW 1 hakuomba na wala hakupata ushauri wowote wa kisheria kabla hajafungua file na baada ya kufungua file la uhai, na hili nitalirudia kwasababu wanasheria ofisi ya DPP walitupilia mbali wajibu wao wa kisheria. Ushahidi unasemaje? Ukurasa wa 159 wa record from 4th/04/2025 to 08/04/2025 I did report to DPP about the treason case. Sikuripoti chochote kuhusu kufunguliwa kesi ya Uhaini na ukurasa wa 162 anasema yafuatayo: The mational Prosecution Act where the offence involve death penalty the DPP's office must be informed.

The NPS Act provide that the DPP must be informed on the investigation of the offence. Kwahiyo PW 1 anatambua sheria inataka nini? Kwamba lazima DPP ajulishwe na mimi sikumjulisha. Halafu anasema DPP alikuwa anapata taarifa mtandaoni na kwahiyo alikuwa anaratibu. Alikuwa anapataje taarifa mtandaoni wakati nyie hamkumjulisha?

Mimi katika mashahidi 17 waliokuja sikumuona DPP wala maafisa wake kuja kusema kuhusu kusimamia upelelezi wa shauri hili. c) Hiyo timu ya Wapelelezi haikuwa na Mwanasheria hata mmoja. The investigation team no a single lawyer involved, ambae angeweza kuwashauri juu ya matakwa ya sheria.

Sehemu ya 470

Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission) d) Wamekaa Mapolisi wanadanganyana hawajui sheria mambumbumbu hawana mwanasheria hata mmoja wanatengeneza kosa. Ukurasa wa 158 wa Record ya Mahakama PW 1 ametaja majina ya timu yake na orodha ya mashahidi wake. Kwa akili yote hii kesi ilitokea kwa PW 1 George Bagyemu. The investigation included ASP Gyumi, Mwakabongo, Numbu, Ibrahim, Ramadhani.

Hiyo ndio timu ya upelelezi ambayo wote ni Mapolisi tu hapo. PW 1 baada ya kugundua kuwa hii habari ya kutomshirikisha DPP alibadilisha msimamo akala matapishi yake. He contradicted himself, page 169 akasema yafuatayo "The chief investigator Amin Mahamba was the one who reported to the DPP by the time I opened the file I did not report officially to DPP.” Na anadai DPP alikuwa anajua hiyo habari maana aliambiwa na Amin Mahamba. e) PW 1 hakuhusisha wala kutoa taarifa kwa mamlaka nyingine yoyote ya kiuchunguzi wala kiserikali kuhusiana na hilo file la Uhaini.

He did not involve or report to any other government authority about the open up of the treason file na hapa namaanisha sio kesi ya Maembe ni kesi ha Uhaini. Ushahidi unasemaje? Ukurasa wa 170 wa record unasema treason ni kosa kubwa sana na pia linahusisha na watu wa TISS na sikuwahi kuzungumza na Mkurugenzi wa TISS kuhusu mambo haya ya Uhaini na sijui kama TISS walipewa taarifa kuhusu kesi hii ya Uhaini. Anakubali kabisa kwamba kesi ya Uhaini ni kubwa sana lakini anasema sijawahi kuwasiliana sio tu na Mkurugenzi Mkuu wa TISS bali hata Mkuu wa Usalama wa Mkoa wa Dar es salaam kwasababu sio kazi yangu kujulisha.

Sasa Waheshimiwa Majaji kesi kubwa kuliko zote kwenye Jamhuri halafu huyu Polisi anasema hajawahi kuwasiliana na watu wanaohusika na usalama wa nchi hii. Huo ndio ushahidi mnaotizamiwa muukubali mtoe adhabu ya kifo.Waheshimiwa Majaji haya ambayo nimeyasema hadi hapo kuhusu PW1 katika haya maeneo manne haukuwa clarified kwenye Re-examination na hakuna aliyemuomba afanye clarification angalia ukurasa wa 176 wa record. Hakuna clarification yoyote kwahiyo maana yake wameukubali na wanategemea Mahakama ikubali kwamba kuna Uhaini na itoe hukumu ya kifo. Sasa hayo ndo aliyoyafanya PW 1 siku nne za kwanza za kosa hadi Tarehe 08.

Sasa twende kwa Amin Mahamba ambae alikuwa Mkuu wa Upelelezi kuanzia Tarehe 08/04. The first remarkable thing about PW 16 is that aliimeza hadhithi ya PW 1 hook, line and sinker. Hilo ndio jambo la kwanza, alikubali kila kitu alichoambiwa na George Bagyemu. Kitu cha pili nilisema juu ya Confusion juu ya kesi ya Upande wa Mashitaka kwa maana ya Confusion kwa mfano PW 16 flattered contradicted about the composition of the investigation team.

Ni lugha gongana kabisa kati ya PW 16 NA PW 1, ukurasa wa 460 PW 16 anasema yafuatayo: The investigation analysis and legal advisory team comprises PW 1 and another officer from DPP office. Hao watu hawakusema kama walimjulisha DPP na ghafla team ilikuwa na muwakilishi kutoka office ya DPP hakutajwa jina na hakuna aliyekuja kutoa ushahidi hapa Mahakamani.Of course tofauti kati ya PW 1 na PW 16 wanatoa ushahidi ulikuwa ni muda umepita PW 1 aliwahi kutoa ushahidi na baadae PW 16 ndio akaja. Nilimuuliza anaitwa nani? Akasema jina fulani la Kibantu nimelisahau.

Nilipomkumbusha kuhusu PW 1 kusema hakukuwa na Mwanasheria wewe unasemaje alikuwepo ukurasa wa 160. The Court should accept my testimony that a team included a lawyer lakini naomba Mahakama ikubali ushahidi wako kwamba kulikuwa na Mwanasheria. Mahakama ikikubali ushahidi wa PW 16 maana yake PW 1 ni muongo. Sasa ni Mahakama gani itakayoconvict charge of treason kwa ushahidi wa mashahidi wa Jamhuri wanaoitana waongo. Kwa waongo hawa unamtia nani hatiani?

Sehemu ya 471

Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission) Hakuna maelezo yoyote kuhusu uwepo wa Mwanasheria na hakuna mwanasheria aliyekuja kutoa ushahidi kwamba alikuwepo kwenye hiyo timu. Kwahiyo ni maneno ya uongo ya mapolisi kwamba ofisi ya DPP ilikuwepo kumbe hamna kitu. Waheshimiwa Majaji comparing the 2 testimonies side by side one could not believe these two Senior Police Officer they were talking about the same case.

Mtu mwenye akili ya kawaida hawezi amini kabisa kwa kutumia akili ya kawaida kabisa. Kwenye ukurasa wa 462 wa Record ushahidi wa PW 16 anasema hivi “I testified after watching the video clip, I was satsified that the accused formed an intention to overthrow the goverment.”Shitaka linasema kuitishia Serikali na huyu anasema kuipindua Serikali. This one is separate case.

Ndimi mbili kama za nyoka, Ulimi mmoja anataka kuipindua Serikali na ulimi mwingine anataka kuitishia Serikali? Sasa Waheshimiwa Majaji mtaenda na ulimi upi kati ya hizi ndimi mbili za hawa walioongoza upelelezi wa kesi hii.?PW 16 Amin Mahamba amethibitisha kuwa ushahidi wa PW 1 kwamba genge la Mapolisi wapelelezi halikuthibitisha mamlaka nyingine ya Serikali kushirikishwa isipokuwa genge lako. Alisema I did not involve RSO of Dar es salaam, Director of TISS or any officer in the investigation. Hakuwezi kuihusisha kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa and even State house was not involved. Sikuwashirikisha wote hao. Unawezaje kupeleleza kesi ya Uhaini kwa style hiyo.?

Huyu PW 16 akajikanyaga tena ukurasa wa 460 kuwa niliwasiliana na DPP kupitia Mayenga ambae ni RPO. Ukisema RPO ni nani hakuna tumachojua kirefu chake na huyu Mayenga hakuitwa kuja kutoa ushahidi kwahiyo ni maneno ya waongo. PW 16 alisema the DPP appointed native name Lawyer from Dodoma ambae alisimamia upelelezi. Watu wanavaaa uniform za Jeshi la Polisi kumbe waongo, wanakuja Mahakamani wanajifanya wana Mavyeo makubwa kumbe waongo tu. Kumbe DPP aliteua WAKILI mwenye jina gumu la Kibantu ambalo Pengine Majaji msingeweza hata kuandika jina lake ni uongo tu huko mwanzo hajasema. Hivyo ndivyo walivyo tengeneza ushahidi wa uongo.

Nje ya hawa Mapolis, upo ushahidi wa MAFICHONI. Waheshimiwa Majaji PW 16 alitoa ushahidi muhimu sana kuhusiana na hao mashahidi waliotoa ushahidi wa kificho, ushahidi uko ukurasa wa 481 wa Record Ushahidi huu ni muhimu kwasababu unathibitisha bila shaka yoyote kwamba mashahidi waliotoa ushahidi mafichoni ukimuondoa PW 17 Mwandishi wa Habari mashahidi wengine ni mashahidi waliokuwa na maslahi makubwa ya kusema uongo Mahakamani.

Ni ushahidi wa mashahidi wenye Massive interest to serve, na PW 16 confirm to the Court hawa wanaoitwa mashahidi wa siri kuwa wana interest. Alisema hivi the undercover witnesses were in deed arrested by the police kwasababu walikuwa wanapanga kufanya fujo na kushawishiana. It is true that upon their arrest they admitted they have been planing to engage in those violence and that they recorded statement in that respect.

These act constituted criminal offences. When they were brought before the Court they admitted the charges. And mwishoni baada ya kuchunguza tuligundua walishawishiwa hayo na Mshitakiwa Tundu Lissu ndio maana tukafuta kesi zao baadae. Yaani umemkamata mtu ambae amepanga kufanya vitendo vya Uhalifu na wakaenda Mahakamani na kukiri halafu baadae wakazungumza nao na kwa vile wamekiri hawa hawana kosa kwahiyo wafutieni kesi.

Sasa hao ndio wameletwa kuja kutoa ushahidi sasa je wangekuja kuwakana hao waliowafutia kesi.???Mnategemea nini kwa mashahidi wa aina hiyo?

Sehemu ya 472

Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission) Sasa hao ndio wameletwa kuja kutoa ushahidi sasa je wangekuja kuwakana hao waliowafutia kesi.???Mnategemea nini kwa mashahidi wa aina hiyo? Kwamba waje kusema ukweli Mahakamani? Kwenye ukurasa 448 wa record PW 16 alikuwa ameiambia Mahakama hivi kuhusiana na hao kwamba the files to be returned to the respected station and the suspect to be recorded statement as witnessses.

Mwanzoni walikuwa wanakamatwa kama watuhumiwa lakini baadae wakasema watafutwe na Wakamatwe lakini waandikishe kama mashahidi wa kesi ya Uhaini, waandikeni maelezo yao upya kabisa. Kwahiyo mashahidi wa Mafichoni ni mashahidi wahalifu waliokamatwa na kuja kutoa ushahidi kwa kificho ili wasionekane wala wasijulikane na mnakumbuka kila mmoja wao niliwauliza ulitishiwa maisha akawa anajibu Hapana hapana.

Mashahidi waliwekwa mafichoni kwa njia za udanganyifu na kusema walitishiwa wakati hakuna aliyewatishia. Hiyo ndio kesi wanayotegemea na nyie Majaji mconvict mshitakiwa. Sasa Sheria inasemaje kuhusu relying on inherent danger through partisan witnessess Mahakama zetu zimetambua hatari za kutegemea ushahidi wa mashahidi wa aina hiyo. Maslahi ya aina hiyo. Kwamba wanaambiwa nitakufutia kesi ukikubali kuwa shahidi wa kesi ya yule. Kushitakiwa sio jambo zuri kwenye taifa hili.

Ukimwambia mtu ukikubali kutoa ushahidi wa yule basi atakubali tu ndo maana Mahakama zetu siki nyingi inasema Abraham Sagulani vs R 1981 TLR 265 Mahakama iliamua yafuatayo kuhusu na suala la mashahidi wa aina hii mashahidi wenye interest to safe their evidence must be approached with care and not reliep with upon unless corroborated with other evidence.

Vilevile kesi ya Asia Iddy vs Jamhuri 1989 TLR 174Kesi ya Justice Rumima Katiti Kesi ya Basilio John Mlai vs R CA 306/2018 CAT at Arusha. Vilevile kesi hizi zote zimezungumzia hiyo habari ya ushahidi wa shahidi mwenye interest to save. Na Mahakama ya Rufani inasema mashahidi wa aina hii ni Liars na waongo. Sasa Majaji kwa msingi wa maamuzi haya ambayo nimeyataja, mashahidi hawa wa mafichoni haupaswi kuguswa kabisa ni ushahidi wa maslahi na hautakiwi kuwa Corroborated kabisa. Ushahidi wa PW 5 utakumbuka ni yule aliyedanganya kuhusu Dini yake.

Mahakamani amekula kiapo kama mkristu na maelezo yake ya maandishi kinasema yeye ni Muislamu. Huyo anayedanganya mpaka dini atamfunga nani? Ukurasa wa 342 wa record. Shahidi huyo pia alidnaganya kuhusu uanachama wake wa Chadema ameulizwa kadi haelewi. PW 7 huyu alisema uongo kuhusu kupelekwa kituo cha Polisi Songea na alidanganya kuhusu uanachama wake kuhusu Chadema.

Ukurasa 358/359. PW 8 Ushahidi wake uko ukurasa wa 353 na 354 nae ushahidi wake incosistent and contradiction, Discrepancies and lies. PW 10 ukurasa wa 378 alidanganya kwamba mshitakiwa alisema tumejipanga kufanya vurugu.

PW 11 ushahidi wake ulijaaa contradictions, Discrepancies. PW 13 Huyu alidanganya juu ya uanachama wake wa Chadema kwenye maelezo mimi ni mwanachama wa Chadema lakini kizimbani mimi bado sijawa mwanachama. Na shahidi wa mwisho PW 14 alidanganya kuhusu kazi yake kwani Polisi alisema yeye ni Mkulima wa Kata ya Mwakibete.

Alipokuja Mahakamani akasema yeye ni fundi umeme wa Jiji la Mbeya na huyu shahidi alisema lazima tukichafue wakati mimi nilisema lazima tukinukishe. Kwahiyo Waheshimiwa Majaji Majaji na watu wanacheka sana. Mashahidi 9 wa kifichoni na mashahidi 7 ni ushahidi wenye mashaka na hakuna ushahidi nje ya ushahidi wa Mapolisi na hawa wa gizani maana yake huo ushahidi should not be acted upon at all.

Part 473Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission) Unabaki ushahidi wa PW 17 ambao umeniunga mkono kwenye mambo yote ya msingi. Waheshimiwa Majaji as a matter of general principle ushahidi wa jamhuri unapaswa kutafsiriwa na kuzingatiwa kwa ujumla wake na kwa vipande pande vyake vilete maana moja. Ushahidi unatakiwa utafsiriwe kwa ujumla wake. Oscar Lwela na Nguza Viking supra zinasema hivyo.

Swali muhimu la kujiuliza huo ushahidi wa upande wa mashitaka unalinganaje na ushahidi wa upande wa utetezi. Ukiufananisha. Relative the prosecution witnesses. All defence witnesses and their Evidence were materially different. Shade character witnesses by the prosecution differ with the defence witnesses. Upande wa Utetezi ni mashahidi wa aina gani waliwaleta: 1. Prominent, well know and experienced political leader. Viongozi wajuu, wanaojulikana na wenye uzoefu na wenye sifa njema. Mwanaharakati anayejulikana kimataifa kwa kutetea haki za Binadamu.

Akiwemo Mshitakiwa ambae ni An intentionally respected human right defender, National Chairman of the largest political party in Tanzania. Ninachotaka kusema DW1 ushahidi wake na wasifu wake kwenye kurasa 559 hadi 563, 566 hadi 577. Wasifu wa shahidi No. 1 wa utetezi. DW 2 Katibu Mkuu wa Chadema, Distinguished political parliamentarian career na wasifu wake uko kwneye kurasa zifuatazo za Record 658, 682 hadi 685, 706 hadi 707DW 3 Amani Golugwa Deputy General Secretary na ushahidi wake uko kuanzia ukurasa wa 729 hadi 730, 754 hadi 759.

Na 764 wa record ya Mahakama.DW 4 ukurasa 807 hadi 810, 814, 821 na 827 hadi 828. DW 5 John Heche a distinguished a political and parlimentary career ukurasa wa 835 hadi 837, 839 hadi 845, 848 hadi 856 na 892 hadi 896.Hao ndio waliokuja kutoa ushahidi mbele yenu. Watu wa maana katika siasa na wenye heshima kwenye Taifa hili sio watu wa Mafichoni. Waheshimiwa Majaji mashahidi wote wa upande wa utetezi walikuwa ni mashahidi wa kuona.

They were there, they were eye witness kwa kila lililotokea siku ile ukilinganisha wa upande wa mashitaka ambao wote hawakuwepo na mmoja aliyekuwepo eneo la tukio anaungana mkono na mashahidi wa upande wa utetezi. Mashahidi wote wa Utetezi wamezungumza sio tu mambo yaliyotokea Tar. 03/04 vilevile walizungumza juu ya uzoefu wao na wa Chama chao juu ya matatizo ya kisiasa, Kikatiba na Kiuchaguzi ya Nchi hii from their direct Experience.

Walizungumza kutoka kwenye mioyo yao. Waheshimiwa Majaji viongozi hao walisema jinsi ambavyo kila mmoja wao alivyowahi kukamatwa kwa tuhuma za uongo na kwamba wamewahi kukamatwa na kufunguliwa Mashitaka. Walizungumza juu ya mauaji ya viongozi na wanachama wa chama chao waliokufa kutona na matatizo ya Uchaguzi nchini. They spoke direct from their experience. All of them, walikiambia Mahakama hii kile ambacho Mahakama hii haikuambiwa na upande wa mashitaka.

Kwamba maneno yalizungumzwa kwenye context gani na kwanini jambo ambalo halikusemwa na upande wa mashitaka. Mashahidi wote hao walisema wana maslahi na kesi hii kwasababu mwenyekiti wao yuko ndani kwa kosa la Uhaini ni kiongozi gani ataona kiongozi wake anashitakiwa kwa makosa ya uongo na walisema kitu muhimu kuwa wana maslahi ya HAKI.

Hawakuja kama wale wengine wa Jamhuri kwamba wanaogopa kufungwa. They just come for the interest of justice ili mateso ya Mwenyekiti wao yakome. Nani atakayesema hayo MASLAHI ni Haramu? Who will say their interest are the same as the interest of the ctiminals who arrested by police and turned as their witnesses. Kwenye kesi ya Goodluck Kyando vs Republic CA 118/2003Mahakama ya Rufani ilisema kila shahidi anastahili kuaminiwa na ushahidi wake kukubaliwa isipokuwa tu. Kama kuna sababu nzuri na za maaana zinazoeleweka za kutokumuamini shahidi huyo.

Sehemu ya 474

Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission) Kati ya hizi shahidi mbili za hawa wakwangu na za hawa wa Mapolisi au ziamini mashahidi wangu? Ushahidi wa watu waongo kama Mapolisi.

Rai yangu on the basis of Goodluck Kyando ushahidi na mashahidi wote wa Upande wa Mashitaka hawastahili kuaminiwa hata kidogo kwa sababu nilizozisema kwa kirefu sana kwasababu nzuri na za maana nilizoonesha kwenye ushahidi huu. Hawastahili kuaminiwa hata kidogo. Kati ya mashahidi wote 17 wa Jamhuri namuondoa shahidi PW 17 ambae ushahidi wake naona ni wa ukweli.

Ushahidi wa mashahidi wote wa Utetezi unastahili kuaminiwa na kukubaliwa kwasababu ambazo nimezizungumzia pia kwa kirefu. Waheshimiwa Majaji kwa kusema hayo sina maana na naomba isichukuliwe kuwa ushahidi wote wa Utetezi haukuwa na mawaaaa. Sina maana hiyo. This is not to suggest that the defence evidence was in every sport sportless and free from blameshes.

Hakuna ushahidi ambao utatolewa kwenye Mahakama ambao hauna shida kwa asilimia 100 kupitia binadamu wa namna hii. Na ushahidi wa mashahidi wote wa upande wa utetezi ni ushahidi wa Binadamu. Hata hivyo mashahidi wote wa utetezi tuliburuzwa sana kwenye cross Examination were able to show descrepancies. Lakini kitu muhimu ni ushahidi wao kwenye maswala muhimu yanayotengeneza hii kesi ushahidi wao ulikuwaje? On all fundamental issues ushahidi wao ulikuwaje?

Mambk ya Jezi ya Arsenal, Umelala Dubai hayo yote yalikuwa hayaibui wala kujibu jambo la msingi kwenye mambo ya msingi kuhusu kesi. Nguza Vikings alias Babu Seya ilisemaje kuhusu contradictions or descrepancies za Upande wa Utetezi. Ilisema yafuatayo at page 25 a conviction in criminal cases is not based on contradiction of the defence evidence rather on the evidence adduced by the prosecution witnesses. Burden of proof lies on the prosecution side and not on the defence and the standard is beyond reasonable doubt.

Discrepancies from the defence may assist the court to determine the prosecution has proved the case beyond reasonable doubt.Nimemaliza kuzungumzia ushahidi na ushahidi niliouzungumzia unaonesha hakuna ushahidi wa kumtia mshitakiwa hatiani katika kesi hii. Badala yake kuna ushahidi wa kutosha wa kumuachia Mtuhumiwa. Waheshimiwa Majaji naomba nizungumzie eneo lingine linaloleta mashaka makubwa kwenye kesi hii. Maeneo yanayocreate reasonable doubt.

Eneo lingine linaloleta mashaka makubwa na ya msingi ni jinsi ambavyo upande wa mashitaka umejaribu kuficha mambo muhimu kuhusu hiyo hotuba ya Tarehe 03/04/2025. Kuna kila sababu ya kuonesha kesi imetengenezwa kwa kuficha na kuondoa maneno mengi ambayo yangekuwa ingeonesha hakukuwa na kesi yoyote. Umefanya kazi ya Cherry picking yaani maneno wasiyoyataka na kuyaondoa ili kuleta maana tofauti wasiyohitaji.

Naomba kwa ridhaa yenu niwarudishe kwenye hati ya mashitaka kwenye hayo maneno wanayoyalalamikia ukiyaangalia hayo maneno kwa makini una realize immediately kuna mambo mengi yameondolewa. Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, wanasema hivi msimamo huu unaashiria uasi.... anasoma hadi mwisho. Hayo ndio maneno mtu asiyekuwa makini hataelewa Kabla ya neno la kwanza kuna dot dot ziko tatu. Elpsis ziko hapo na maana yake kulikuwa na maneno kabla ya wanasema.

Maneno ya kabla hapo wameyaondoa. Inaendelea hapo anasoma msimamo huu unaashiria uasi ni kweli, ni kweli kwasababu .. kuna neno mabadiliko halafu elpsis sasa hapo napo kuna maneno yameondolewa. Kwahiyo kwenye baada ya mabadiliko pia nako yameondolewa. Je ni maneno gani na kwanini yaondolewe. Kwahiyo tutaenda kukinukisha sanasana sasa kati ya kukinukisha na sanasana kuna elpsis na maneno yameondolewa. Hayo nayo ni maneno gani?

Tutaenda kukinukisha sanasana hapo napo kuna elpsis kwa maana ya maneno yameondolewa. Je yalikuwa na maana gani hayo maneno na kwanini hawajayaweka na hakuna ushahidi wowote kuhusu kwanini wametoa maneno hayo?

Sehemu ya 475M


he. Lissu anaendelea anasema Waheshimiwa Majaji, facts are very sturbon things (ukweli ni mbishi sana, ukweli huwa unakaa kufichwa and truth is concrete, ukweli ni mgumu kama jiwe. Hicho ambacho kimefichwa kwenye hati ya mashtaka, yale ambayo hayapo kwasababu ya ellipses yameletwa kwenye ushahidi, huo ushahidi unaiwezesha mahakama kupata kile ambacho hati ya mashtaka ilitaka kukificha.

Ukweli wa kwanza ambao umeletwa na ushahidi ni kwamba hii kesi ni mgogoro wa kisiasa na wa kikatiba kuhusu chaguzi za Tanzania. Mgogoro ambao umepiganiwa kwa miaka zaidi ya 30, ni mgogoro kuhusu chaguzi za nchi hii sasa umehamishiwa Mahakamani na kuvalishwa mavazi ya uhaini. Waheshimiwa majaji mmeletewa muamue ugonvi wa kisiasa kati ya Chadema na viongozi wake na CCM na Serikali yake.

Waheshimiwa majaji kwenye preliminary hearing iliyoko ukurasa wa 131-132 wa record upande wa mashtaka ulileta maelezo yanayoonyesha kwamba mgogoro huu ni wa uchaguzi, hata hati ya mashtaka yenyewe, hayo maneno yenyewe yanahusu uchaguzi, nia kwenye hati ya mashtaka ni kuchochea watu ili wazuie uchaguziUkiacha hayo, maelezo yote ya maandishi, vielelezo vyote D1 hadi D16 vyote vinaonyesha ni mgogoro wa uchaguzi.

Documentary records zote zinathibitisha kuwa huu ni mgogoro wa uchaguzi. Ushahidi uliotolewa na mashahidi 17 wa mashtaka na mashahidi 5 wa utetezi unaonyesha ni mgogoro wa kisiasa kuhusu uchaguzi. Waheshimiwa Majaji huo muktadha ni muhimu sana kueelewa kuwa ni mgogoro wa kisiasa wa uchaguzi unaokuwa litigated in a criminal court. Kwa miaka zaidi ya 30 from 1993 mtikila one mgogoro huu ulikuwa unapiganiwa katika mahakama za civil na majukwaa ya hadhara, vyombo vya habari na majukwaa ya sasa kama Bunge.

Sasa Mawakili wa Serikali na Mapolisi wao wameuvalisha huu mgogoro mavazi ya kijinai. Waheshimiwa majaji katika ushahidi wa pande zote mbili, ushahdii wa utetezi wa mashahidi wake wote ndio umetoa muktadha sahihi wa kesi hii. Ushahidi wa utetezi umeonyesha huu mgogoro mrefu wa miaka mingi wa kikatiba na kisiasa kuhusu uchaguzi katika nchi yetu ambao umetufikisha hadi kwenye mgogoro wa uchaguzi wa mwaka jana. Mashahidi wote wa upande wa utetezi wameelezea kwa kirefu hayo maneno yakiyopo kwenye hati ya mashtaka kama no reforms no election, ni kitu gani, imetokana na nini, wameelezea extensively.

Mashahidi wa upande wa utetezi in this particular case DW4 ameelezea mahakama kuwa hayo maneno wanasema “mshtakiwa aliposema wanasema kitu kimoja sahihi hapa” kwenye ukurasa wa 810-811 amesema Mwenyekiti alikuwa anawajibu G-55 waliokuwa wameandika mtandaoni, tumeipata hii kwa DW4 na hatukuipata kwa wale wenye wajibu wa kuthibitisha mashtaka yaoWaheshimiwa majaji upande wa mashtaka hawakusema chochote kuhusu juu ya maneno kama kukinukisha, maana tumeipata kutoka ushahidi wa utetezi.

Upande wa mashtaka kwa jinsi walivyoandika draft ya mashtaka na kunyofoa nyofoa hayo maneno walitaka kuonyesha kuna kosa kubwa sana lakini ushahidi wa utetezi umeonyesha hakuna kosa lolote lililofanyika, sio kukinukisha, sio kuvuruga uchaguzi, sio kuhamasisha uasi, hakuna kosa hilo Ushahidi wa utetezi umetusaidia kuonyesha the missing context, upande wa mashtaka hawakutaka kutuonyesha hiyo context ila tumejua kwasababu ya utetezi.

Ukiangalia hayo maneno yanayolalamikiwa utafikiri kwamba huo mkutano wa 3/4/2025 ulikuwa na maneno hayo tu, kwamba mshtakiwa aliongea hayo maneno ya nusu dakika then washiriki wakaondoka.

Waheshimiwa majaji naomba mtafakari yafuatayo yaliyoko kwenye ushahidi. PW1

Jaji Ndunguru anasema kwanini tusibreak kwanza baadae ndio uje useme after breakMhe.

Lissu: Ni sawa waheshimiwa majaji, leo tutamaliza sitaki kesho kurudi hapa

Jaji Ndunguru: Ni wewe tu , kwa sauti ya upole huku akicheka

Watu kicheko sana.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa tambua kuwa tukirudi tuna masaa mawili na nusu tu

Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji, I intend kumaliza leo

Jaji Ndunguru: Mahakama inahairishwa hadi saa nane na nusu.
 
MAHAKAMA IMEANZA TUNDU LISSU ANABISHANA KIDOGO NA MAJAJI KISHA ANAENDELEA.

SEHEMU YA 1. TAREHE 28.9.2026.

MAHAKAMA INAANZA HAPA

Ameingia Lissu, kisha wakafuatia Majaji kwa pamoja.

Karani wa Mahakama: Anaanza kusoma Criminal Session, Kesi Na. 19605 ya mwaka 2025, Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu.

Anasimama Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga.

Nassoro Katuga: Iwapendeze Mahakama hii Tukufu, Waheshimiwa Majaji wa Mahakama hii Kuu. Naitwa Nassoro Katuga, Wakili wa Serikali Mkuu. Nipo pamoja na:

1. Job Mrema, Wakili wa Serikali Mkuu
2. Ignas Mwinuka, Wakili wa Serikali Mkuu
3. Tawabu Issa, Wakili Mwandamizi
4. Cuthbert Mbilinyi, Wakili wa Serikali
5. Winniwa Kasara, Wakili wa Serikali

Waheshimiwa, jopo la mawakili sita linaiwakilisha Jamhuri, na mshtakiwa yupo kizimbani.

Shauri limekuja kwa ajili ya mawasilisho ya mshtakiwa.

Sisi upande wa Jamhuri tupo tayari. Sijui mwenzetu.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa?

Lissu: Nipo tayari, Mheshimiwa Jaji.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Unakumbuka Ijumaa wakati tunahairisha ulikuwa umemaliza hoja ya saba. Tuanze ya nane.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nawashukuru sana.

Waheshimiwa Majaji, kabla sijazungumza ya leo, naomba niseme yafuatayo.

Na haya nayazungumza kwa sababu leo namaliza hoja yangu ya mawasilisho.

Jaji Ndunguru: Katika session hii ya asubuhi?

Lissu: Hilo siwezi kusema.

Kwa sababu leo namalizia kuwasilisha, kuna maneno ambayo naweza nisiyazungumze tena.

Naomba sasa kusema mbele ya Majaji yale ambayo nilitaka kusema.

Jaji Ndunguru: Kwanini usiyaweke mwisho, tukupe muda ili twende kwa mtiririko?

Lissu: Hilo nalo ni gumu. Kwa kweli, naomba muda niweze kusema.

Lissu: Hoja ya nane inauliza kama, kwa kuzingatia majibu ya hoja saba zilizotangulia, upande wa mashitaka umethibitisha mashitaka yake kwa kiwango cha uthibitisho kinachotakiwa na sheria.

Kiwango cha uthibitisho kinachotakiwa na sheria katika kesi ya jinai kama hii ni uthibitisho usioacha shaka yoyote ya msingi — Proof Beyond Reasonable Doubt.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Kutoka mahakama kuu ya Tanzania, masjala ndogo jijini Dar es Salaam, kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA dhidi ya Jamhuri inaendelea.

Tayari mshtakiwa Tundu Lissu ameshawasili mahakamani

Kaa tayari kwa updates
huenda leo akanywa lita 30 za maji, kabla hajaanza kusinzia akiwa kasimama anajieleza kizimbani na kisha kuwaomba poo majaji as last time 🐒
 
Back
Top Bottom