Mahakamani 28 Septemba: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Mahakamani 28 Septemba: Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Kutoka mahakama kuu ya Tanzania, masjala ndogo jijini Dar es Salaam, kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA dhidi ya Jamhuri inaendelea.

Tayari mshtakiwa Tundu Lissu ameshawasili mahakamani

Kaa tayari kwa updates
We bwege saa ngapi unafanya kazi? Ndiyo uje ulalamike serikali ya CCM imekufanya maskini? We ni hasara kwa mamako na kwa Taifa
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI.

SEHEMU YA 2.
Lissu: Hicho ndicho kiwango cha uthibitisho kinachotakiwa na sheria kwa kesi ya jinai kama hii, kwa mujibu wa Kifungu cha 3(2)(a) cha Sheria ya Ushahidi.

Hicho ndicho walichotakiwa kuthibitisha upande wa mashitaka: uthibitisho wote bila kuacha shaka yoyote ya msingi.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, katika maswali saba niliyouliza/niliyopendekeza Waheshimiwa Majaji muyatafakari, kwenye maswali yote saba upande wa mashitaka umeshindwa.

Na kwa ushahidi uliopo hapa Mahakamani, hauwezi kuthibitisha maswali yote saba.

Waheshimiwa Majaji, swali la kwanza lilikuwa kama mshtakiwa ndiye aliyeitisha/kuandaa mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025, ambapo maneno yanayolalamikiwa yanadaiwa kusemwa.

Kwenye swali hili, Waheshimiwa Majaji, upande wa mashitaka umeshindwa.

Na kwa ushahidi uliopo Mahakamani, hauwezi kuthibitisha kwamba mshtakiwa ndiye aliyeitisha au kuandaa huo mkutano.

Waheshimiwa Majaji, swali la pili lilikuwa kama mshtakiwa ndiye aliyewaalika waandishi wa habari kwenye huo mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025.

Hilo ndilo lilikuwa swali la pili.

Waheshimiwa Majaji, kwenye swali la pili vilevile upande wa mashitaka umeshindwa, na kwa ushahidi uliopo Mahakamani hauwezi kuthibitisha kwamba mimi ndiye niliyealika waandishi wa habari.

Hawawezi kuthibitisha kwa ushahidi uliopo.

Waheshimiwa Majaji, swali la tatu lilikuwa kama mshtakiwa aliunda nia ya kuchochea mtu au kikundi cha watu kuzuia Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa lengo la kutishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Waheshimiwa Majaji, kwenye swali la tatu upande wa mashitaka umeshindwa kabisa, na kwa ushahidi uliopo Mahakamani hauwezi kuthibitisha tuhuma zinazohusu swali hili.

Kwamba mshtakiwa alitengeneza nia ya kuchochea mtu yeyote au kikundi cha watu kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Waheshimiwa Majaji, swali la nne lilikuwa kama maneno yanayodaiwa kutamkwa na mshtakiwa yanatengeneza kosa lolote linalojulikana na sheria za Tanzania.

Waheshimiwa Majaji, kwenye swali hili la nne, upande wa mashitaka umeshindwa kabisa, na kwa ushahidi uliopo Mahakamani hauwezi kuthibitisha kwamba maneno yaliyotamkwa na mshtakiwa yanatengeneza kosa lolote lile linalojulikana na sheria ya nchi hii.

Waheshimiwa Majaji, swali la tano lilikuwa kama maneno yanayodaiwa kutamkwa na mshtakiwa ni matendo kwa mujibu wa Kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu.

Waheshimiwa Majaji, kwenye swali la tano, upande wa mashitaka umeshindwa kabisa, na kwa ushahidi uliopo Mahakamani hauwezi kuthibitisha kwamba maneno ni matendo kwa mujibu wa Kifungu cha 39(2)(d).

Kwamba maneno siyo matendo.

Hawajathibitisha, na hawawezi kuthibitisha kwamba maneno ni matendo.

Waheshimiwa Majaji, swali la sita lilikuwa kama mshtakiwa ndiye aliyechapisha maneno yanayolalamikiwa kwenye mtandao wa YouTube wa Jambo TV.

Waheshimiwa Majaji, kwenye swali la sita, upande wa mashitaka umeshindwa kabisa, na kwa ushahidi uliopo Mahakamani hauwezi kuthibitisha kwamba mimi, mshtakiwa, ndiye niliyechapisha hizo video kwenye mtandao wa YouTube wa Jambo TV.

Waheshimiwa Majaji, swali la saba lilikuwa kama Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika kutokana na maneno yanayodaiwa kuwa ya kihaini na yanayodaiwa kuyatoa kwenye mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025.

Waheshimiwa Majaji, kwenye swali hili la saba, upande wa mashitaka umeshindwa kabisa, na wala hawakujaribu kuthibitisha kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishika kwa hayo maneno.

Na kwa ushahidi uliopo Mahakamani, hawawezi kuthibitisha tuhuma hizo.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, kwenye maswali yote saba, upande wa mashitaka umeshindwa kabisa, na kwa ushahidi uliopo hawawezi kuthibitisha tuhuma yoyote waliyotoa dhidi ya mshtakiwa kwa kiwango kinachotakiwa cha uthibitisho usio na shaka yoyote ya msingi.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, je, ni hayo tu?

Ni hayo tu?

Ni hayo tu ambayo upande wa mashitaka umeshindwa na hauwezi kuthibitisha?

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 3.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nataka niseme kwamba kwa ushahidi uliopo Mahakamani kuna masuala mengine yaliyojitokeza na ambayo yametolewa ushahidi, na yanathibitisha uwepo wa mashaka makubwa na ya msingi juu ya kesi yote ya upande wa mashitaka.

Mashaka makubwa na ya msingi.

Waheshimiwa Majaji, eneo la kwanza linaloonyesha mashaka makubwa na ya msingi ni kwamba kesi hii yote imetengenezwa na mtu mmoja au pengine wawili. (Underline: mtu mmoja.)

Waheshimiwa Majaji, ushahidi unasema kuhusu hili. Na huyo mtu ni nani?

Ushahidi wake ukoje?

Waheshimiwa Majaji, huyo mtu ni Shahidi Na. 1, George Bagyem.

Waheshimiwa Majaji, George Bagyem ndiye aliyeamua kwamba hayo maneno yanatengeneza kosa la uhaini. Ni yeye peke yake.

Waheshimiwa Majaji, nawaalikeni muangalie rekodi za Mahakama, ukurasa wa 145 mpaka ukurasa wa 146.

Waheshimiwa Majaji, kwenye hizo kurasa, PW1 anazungumzia tarehe 8, siku ya nne baada ya kuonyeshwa video ya mkutano wangu.

PW1: “From 08 April 2025, I instructed Assistant Inspector Michael to open two different files, one for the treason and the second for the publication of false information.”

The treason file was opened and marked Case No. 727/2025.

Yeye ndiye aliyemwamuru Assistant Inspector Michael kufungua faili la kesi ya uhaini.

Na hilo alilifanya siku nne tu baada ya kuonyeshwa ile video.

PW1 hakufanya yafuatayo:

PW1 hakuomba maelekezo/mwongozo kutoka kwa wakubwa wake juu ya kufungua kesi ya uhaini. (Kosa kubwa namba 1.)

Hakuomba guidance from his superiors.

Nilimuuliza, Waheshimiwa Majaji, kama mtakumbuka: “Ulitoa taarifa kwa ZPC?” Akasema, “Hapana.”

ZPC ndiye Boss wake wa Kanda.

Hakuomba maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Kazi yake, Boss wa Kanda, ambaye kwa utendaji ndiye Boss wake katika Kanda.

Je, aliomba guidance kutoka kwa DCI Kingai?

Jibu lake ni, Hapana.

Hoja yake katika ukurasa wa 146 inasema kwamba baada ya kufungua faili la uhaini:

PW1: “I formed an investigation team to make follow-up. I then communicated DCP Ng’azi about the team I formed.”

Baada ya kuwa amefungua faili, ndiyo akawajulisha kwamba nimefungua faili la uhaini.

Kwa shitaka kubwa kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
TUNDU LISSU ANAFANYA MAJUMUISHO YA MWISHO MAHAKAMANI

SEHEMU YA 4.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, kuhusu kutotoa taarifa wala kuomba mwongozo kwa ZPC, ushahidi huo upo katika ukurasa wa 148 wa rekodi.

Jambo la pili, Waheshimiwa Majaji: PW1 hakuomba wala hakupata ushauri wowote wa kisheria kabla hajafungua faili na baada ya kufungua faili.

(Before and after opening the file, the treason file.)

Na hilo, Waheshimiwa Majaji, nitalirudia: hakuomba wala hakupata any legal advice.

Ushahidi unasemaje? Kwenye ukurasa wa 159:

Kuanzia tarehe 4, siku aliyoonyeshwa video, mpaka tarehe 8 Aprili, anasema alitoa taarifa kwa DPP kuhusu kufunguliwa kwa kesi.

Na katika ukurasa wa 162 anasema hakumtaarifu DPP kuhusu kufunguliwa kwa kesi.

PW1 anatambua sheria inataka nini.

Sheria inataka Mwendesha Mashitaka ajulishwe kwa kesi yoyote inayohusu adhabu ya kifo.

Anasema, “Sikumjulisha.”

Halafu anasema anatambua kwamba Ofisi ya DPP ndiyo inayoratibu upelelezi wa makosa ya namna hii.

Anasema DPP alikuwa anapata taarifa mtandaoni.

Je, alikuwa anapata taarifa namna gani mtandaoni kama hawakumjulisha?

Na, Waheshimiwa Majaji, katika ushahidi wa Mashitaka 17, mimi sikumbuki DPP Mwakitalu au msaidizi wake aje kuthibitisha kwamba alijulishwa kuhusu mashitaka ili aweze kuratibu upelelezi.

Jambo la tatu, Waheshimiwa Majaji, ni kwamba hiyo timu ya wapelelezi wote haikuwa na mwanasheria hata mmoja.

Ilikuwa na polisi tu.

Hawakuwa na mwanasheria wa kuwawezesha kujua kama wanavunja sheria.

Walikaa polisi ambao hawakuwa na uelewa wa sheria.

Ushahidi unasemaje?

Ukurasa wa 158, PW1 ametaja majina ya timu yake ya upelelezi.

Ukiangalia hiyo timu, wote ni polisi na hakuna mwanasheria hata mmoja.

Anasema, ukurasa wa 158:

PW1: “I then formed a team of investigation: Assistant Inspector Michael Kyumi, Assistant Inspector Ibrahim, Assistant Inspector Ruben Mwakabonga, D/Corporal Ibrahim, D/Corporal Ramadhani and myself.”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
huenda leo akanywa lita 30 za maji, kabla hajaanza kusinzia akiwa kasimama anajieleza kizimbani na kisha kuwaomba poo majaji as last time 🐒
Drinking enough water each day is crucial for many reasons: to regulate body temperature, keep joints lubricated, prevent infections lastly makes him hard as energizer when ***’n with akina Katuga
 
Back
Top Bottom