Maharage Chande aondolewa TANESCO, apelekwa TTCL. Gerson Msigwa awa Katibu Mkuu Wizara ya Michezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na utenguzi wa Viongozi mbalimbali kama ifuatavyo:
  1. Amemteua Ndugu Said Othman Yakubu kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Yakubu alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
  2. Amemteua Ndugu Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
    Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huo, Ndugu Msigwa alikuwa Mkurugenzi wa Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali. Nafasi
    iliyoachwa wazi ya Mkurugenzi wa Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali itatangazwa baadae.
MAKATIBU TAWALA MKOA
  1. Ametengua uteuzi wa Ndugu Abdallah Mohamed Malela, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara. Badala yake amemteua Bi. Bahati Ibrahim Geuzye kuwa katibu Tawala Mkoa wa Mtwara. Kabla ya uteuzi huu, Bi Bahati alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
  2. Amemteua Ndugu Mohamed Jumanne Gombati kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Geita. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Gombati alikuwa Mkurugenzi Msaidizi
    Sehemu ya Maafisa Waandamizi katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
WAKUU WA TAASISI
  1. Amemteua Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Aidha aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Bw. Omar Issa ataendelea na majukumu mengine aliyopangiwa katika Ofisi ya Rais - Tume ya Mipango.
  2. Amemteua Ndugu Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Chande alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
    Anachukua nafasi ya Mhandisi Peter R. Ulanga ambaye atapangiwa kazi nyingine.
  3. Amemteua Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Kabla ya uteuzi huu Ndugu Nyamo - Hanga aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
  4. Amemteua Dkt. Erasmus Fabian Kipesha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Kipesha alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (TEA).
WAKUU WA WILAYA
  1. Ametengua uteuzi wa Ndugu Hanafi Msabaha, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini na badala yake amemteua Bi. Mwanahamisi Mkunda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini. Kabla ya uteuzi huo Bi. Mkunda aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.
  2. Amemteua Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Mariam Chaurembo atapangiwa kazi nyingine.
WAKURUGENZI WATENDAJI WA HALMASHAURI (MA -DED)
  1. Amemteua Ndugu Hassan Bakari Nyange kuwa Mkurugenzi (DED) wa Mtwara TC. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Nyange alikuwa DAS Wilaya ya Namtumbo. Aidha, aliyekuwa Mkurugenzi (DED) wa Wilaya ya Mtwara TC, Kanali Emmanuel Mwaigobeko atapangiwa kazi nyingine.
  2. Ametengua uteuzi wa Bi. Tatu Said Issike, Mkurugenzi wa Mtwara DC na kumteua Ndugu Abeid Abeid Kafunda kuwa Mkurugenzi (DED) wa Mtwara DC. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Kafunda alikuwa Mwanasheria katika Ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali.
  3. Amemteua Ndugu Reuben Sixbert Jichabu kuwa Mkurugenzi (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndugu Erica Yegella atapangiwa kazi nyingine.
KATIBU TAWALA WILAYA
Amemteua Ndugu Francis George Mgoloka kuwa Katibu Tawala wa Wilaya
(DAS) ya Namtumbo. Kabla ya uteuzi huo Ndugu Mgoloka alikuwa Katibu Tarafa Mswaki - Kilindi Handeni.

Katibu Mkuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wataapishwa siku ya Jumanne saa sita mchana Ikulu, Dar es Salaam.
View attachment 2759138
View attachment 2759139
View attachment 2759157
*TANESCO:
Haki imetendeka, anao uelewa mkubwa kwenye masuala umeme. Alitolewa REA kwa uonevu.*
 
Maharage ameboronga TANESCO lakini bado anapewa ukurugenzi kwingine....ina maana hakuna wasomi wengine Tanzania hii wenye weledi!?.
Maharage Chande sio tatizo, watu wa business kama yule anafaa huko alikopelekwa TTCL akaongeze mapato sio kwenye public utilities kunakohitaji uzalendo na kulinda wananchi maskini.

Hata January Makamba, huko aliko kunamfaa na ata perfom vizuri maana anapenda sana diplomasia. Diplomasia kwenye energy sector utapigwa na kuumiza wananchi.
 
Hivi maharage ni mtoto wa Mohamed Chande Othman???
 
Maharage Chande sio tatizo, watu wa business kama yule anafaa huko alikopelekwa TTCL akaongeze mapato sio kwenye public utilities kunakohitaji uzalendo na kulinda wananchi maskini.

Hata January Makamba, huko aliko kunamfaa na ata perfom vizuri maana anapenda sana diplomasia. Diplomasia kwenye energy sector utapigwa na kuumiza wananchi.
Hayo ni matumizi mabaya ya kodi. TTCL ishakufa kitambo na limebaki jina tu.
Laini za TTCL zenyewe hazipo.
Hii nchi inachekesha sana
 
mwamedi amemaliza kazi yake tanesco aliyopelekwa kuifanya tayari shirika letu la Tanesco limeshauzwa sasa anakwenda kuuza TTCL yetu akitoka hapo samia anamuhamishia Air Tanzania, huyu raisi wenu ameletwa kwa mipango maalumu, kumbuka alisema serikali haifanyi biashara wakati Dunia nzima karibia nchi zote kuna state owned enterprise hata huko kwa warabu kila kitu ni state owned hata China imeendelea kwa sababu Serikali inarun mashirika nyeti, kila kitu kimepangwa …
Pole kwa sonona sugu uliyonayo, Mama Samia huyooo anachanja mbuga tu
 
Kwa hiyo TTCL ndo imepelekewa mtu incompétent. Yaani mtu kaharibu Tanesco anapelekwa kuwa mkurugenzi shirika lingine.Samia kweli anatuchezea akili.Sema na sisi sijui namna gani vipi.Maana tatizo la umeme tu,lazima tungeandamana.
 
Back
Top Bottom