Maharage Chande aondolewa TANESCO, apelekwa TTCL. Gerson Msigwa awa Katibu Mkuu Wizara ya Michezo
WAKUU WA TAASISI
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan,
Amemteua Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Aidha aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Bw. Omar Issa ataendelea na majukumu mengine aliyopangiwa katika Ofisi ya Rais - Tume ya Mipango.
19. Amemteua Ndugu Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Chande alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Ujio wa Major General Kisesa Simuli ulete TIJA kubaini ikiwa palikuwa na hujuma kusababisha nyufa katika Bwawa JNHP.
 
Bwana makeke atakuwa anasema" kutoka ikulu magogoni mimi Salimu Kipepe na prado langu jeusi mtanikoma😂😂
 
Walau sasa Nishati kutatakata kidogo..

January na Maharage walikuwa virusi na wahujumu wa taifa..

Naona ziara ya Mtwara imefyeka watumishi wengi sana. Madudu yalikuwa mengi bila shaka.
TaNesCo ni dude kubwa linalotisha sana mkuu
 
Yawezekana ukawa na hoja but nakuhakikishia matatizo ya umeme nchi hayatakoma bila kufanya uwekezaji kweny sekta ya nishati ya umeme!! CCM washafeli kitambo san na tanesco yao, nakuhakikishia hata bwawa likianza uzalishaj umeme utakua ni changamoto tu!!
Uwekezaji so ni huo wa Kinyerezi na Bwawa la Mwalimu Nyerere?
 
Anaweza asiwe kati ya hao mnaohisi watakuwa WASEMAJI

KIKEKE na KITENGE.

Atateuliwa mtu mwingine kabisa....
 
Tatizo la utendaji hafifu ni kuteuana makada kufanya kazi za kitaaluma.
Ndio maana mna shindwa ku perform mna baki kuiba tuu.
Yaani pesa ina toka hazina na kupelekwa halmashauri nila maelekezo. Baadae mna zipiga . Sisi tuna ongezewa kodi.
Mungu ana waona maCcm
 
Sio msikivu, watu wamepiga kelele muda mrefu.

Rais alithubutu kumwambia Makamba..." mwanangu wanataka nikutumbue wewe piga kaxi"

Huu sio uongozi bali hisani na sio msikivu hadi yaharibike
Wewe ulitaka kelele moja tu amtoe ? ulitaka ukipiga kelele tu asijiridhishe kwa namna yake?, kama ulitaka Rais wa kukurupuka kwa namna hiyo basi vuta subira …sio Samia Suluhu Hassan

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom