Aisee hii kali kabisa. Ila Kwa nionavyo Mimi.
1. Wizara ya Nishati arudishwe Muhongo.
2. Maharage Chande hata kama uraiani tunaona hajafanya vizuri Ila ndani Tanesco aliwanyoosha Sana wezi. Yaani zile njia za wizi zote alikomesha na Shirika hata mahesabu yake yakaanza kuwa mazuri. Na ninajua kwa kuwanyoosha basi wafanyakazi wakaanza kuhujumu ili aonekane hawezi. Ninakuhakikishia Leo wafanyakazi wa Tanesco watafanya sherehe kwa kuwa fursa za ulaji zitarudi. Yaani walibanwa. Mfano wafanyakazi ofisi za kanda, mikoa na Wilaya walikuwa ni wengi na hakuna KAZI ya maana. Yaani kuajiriwa tu kinansmnanamna unaenda tu kukalia viti vya Tanesco kunywa chai na supu na kupiga umbeya. Huo ukawa mzigo mkubwa Sana kwenye payroll mana unakuwa na wafanyakazi wengi ambao hata hawahitajiki. Kwenye emergency na call ndiyo walipiga mno mno na ndiyo akaweka one call centre. Na wako smart kugawa majukumu kwa zone au ofisi husika ila nako wakawa wanafanya kwa hujuma kutekeleza matatizo ya umeme yaliyokuwa Yana repotiwa centre. Yaani unakuta taarifa ya emergence imeletwa say Tanesco Kurasini lakini warakaa siku hata 3 hawaendi kwenye tukio. Mfano mmoja Mimi binafsi nilipiga simu call centre kuhusu nguzo ya umeme ilivyokuwa hatarini kuanguka. Hakika hawakufika mpaka ikaanguka na ikawagharimu Sana. Niliporudi call centre kuwajulisha walishangaa Sana maana taarifa walishapewa Tanesco Kurasini Ila haikutekelezwa kwa siku 7. Yaani ni kama kulikuwa na kamgomo baridi hivi ili kukwamisha utendaji wa Maharage Chande.
Ila pia hata kama ameondolewa tatizo la umeme halitakwisha kamwe. Kuna hujuma nyingi mno. Hivi.mnajua kuna wauza majenereta? Hivi mnajua kuna fisadi mmoja god father wa Mwezi Mosi anamiliki kampuni ya gas tunazotumia kupikia na mambo mengine?. Ambaye ndiye alikuwa anampa kazi Mwezi Mosi kupigia kampeni gas yake nyumba kwa nyumba? Haya mambo ni magumu kuliko mnavyofikiria mtaani kwetu huku.
Mambo yamekuwa si mambo. Mungu tunusuru tuko kwenye lindi la mahangaiko mengi Sana. Yaani tumesongwa na mambo mengi mno.
Yaani nimechoka Sana Mimi
Zogwale.