Maharage Chande aondolewa TANESCO, apelekwa TTCL. Gerson Msigwa awa Katibu Mkuu Wizara ya Michezo
Naona Kikeke au Kitenge akipewa nafasi ya usemaji ila hasa hasa anaweza kupewa Kitenge kwa sababu amesimama sanana udhalimu wa Liliondo akifanya coveragw kubwa sana kuwafunika wauaji.
Nimekaa pale
Kitenge hana Elimu yakuwa msemaji wa Gavoo! Hapo ni Kikeke
 
Walau sasa Nishati kutatakata kidogo..

January na Maharage walikuwa virusi na wahujumu wa taifa..

Naona ziara ya Mtwara imefyeka watumishi wengi sana. Madudu yalikuwa mengi bila shaka.
Kadi za CCM zilirudishwa kwa wingi sana huko kusini
 
Tutaona Sasa kama umeme utawaka.

Na hizi lawama ziendelee hivi hivi kwa mkurugenzi mpya Tanesco ngao ukiendelea
Unajua watz ni watu wa ajabu sana!! Hivi tatizo la umeme la nchi hii ni la mkurugenzi? Wanasiasa ndio wachawi wenyewe, Hata huyo anayeingia sidhani kama kuna jipya atakalolifanya ili tatizo hili la umeme liishe!! Sema huyo bwana maharage alikuwa na maneno ya shombo sana
 
Sasa nimekubali mitandao ya kijamii ina nguvu kuliko Tv na magazeti.

Mitandao imemng’oa Maharagwe na makamba wake.
So what? Naye anayeingia hawezi kuondoa tatizo hili la kukatika katika umeme, wanasiasa wameona kutuliza hali ya hewa ni kufanya hivyo tu, ila halina tija.
 
Maharage Chande sio tatizo, watu wa business kama yule anafaa huko alikopelekwa TTCL akaongeze mapato sio kwenye public utilities kunakohitaji uzalendo na kulinda wananchi maskini.

Hata January Makamba, huko aliko kunamfaa na ata perfom vizuri maana anapenda sana diplomasia. Diplomasia kwenye energy sector utapigwa na kuumiza wananchi.

wewe ndio umeongea na mtizamo wako ni sahihi kabisa.
 
Walau sasa Nishati kutatakata kidogo..

January na Maharage walikuwa virusi na wahujumu wa taifa..

Naona ziara ya Mtwara imefyeka watumishi wengi sana. Madudu yalikuwa mengi bila shaka.
Yetu macho! Muda ni mwalimu!
 
Nimesoma toka mwanzo wa uzi mpaka hapa nilipofikia nilichoona ni tuhuma tuu kwa MC na hakuna aliyeweza kujibu hata baada ya kuulizwa na kutakiwa waorodheshe makosa na matatizo ambayo MC ameyafanya kwa umma na taifa kwa ujumla kupitia au akiwa Tanesco au mabaya aliyoyafanya kwa Tanesco ktk kulididimiza hilo shirika na taifa kwa ujumla

Hakuna shutuma bila tuhuma basi nyie mnaomshutumu tupeni na tuhuma zake
 
Walau sasa Nishati kutatakata kidogo..

January na Maharage walikuwa virusi na wahujumu wa taifa..

Naona ziara ya Mtwara imefyeka watumishi wengi sana. Madudu yalikuwa mengi bila shaka.
Tatizo ni pale viongozi wanapowekeza upande mmoja wa nchi au Kanda Fulani Kwa manufaa ya kisiasa.

Mwanza,Arusha,mbeya, Kilimanjaro ziara 14 ndani miaka 2 halafu Mtwara ziara 1 ndani ya miaka 2.


Suala la utawala wa Majimbo liwepo ktk KATIBA MPYA
 
Walau sasa Nishati kutatakata kidogo..

January na Maharage walikuwa virusi na wahujumu wa taifa..

Naona ziara ya Mtwara imefyeka watumishi wengi sana. Madudu yalikuwa mengi bila shaka.
Wameshasaini miktaba ya kuliuza shirika na nishati yote wewe unadhani Kuna Nini. Kasaini lile dili la hewa ya helium aka hewa baridi la karibia dola 30 billioni. Umeme wa bwawa la NYERERE lingeshusha Bei ya umeme Ila unaendwa kuuzwa nje like msumbiji, Uganda si uliona kijana wa maza akaonana na mu7 eti anayo kampuni ya kuuza solar,Kama madini yote yameshauzwa. Mama anauza bandari na mbuga unadhani tutabakia na Nini ,labda wananchi tu ndio waliobakia.
So yule dogo March sijui June akaingia pale kufanikisha miktaba ya dili nene Nene na sijui why jpm hakusaini huu mktaba nadhani Taifa lingefaidi kuliko genge la watu fulani wachache
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na utenguzi wa Viongozi mbalimbali kama ifuatavyo:
  1. Amemteua Ndugu Said Othman Yakubu kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Yakubu alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
  2. Amemteua Ndugu Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
    Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huo, Ndugu Msigwa alikuwa Mkurugenzi wa Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali. Nafasi
    iliyoachwa wazi ya Mkurugenzi wa Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali itatangazwa baadae.
MAKATIBU TAWALA MKOA
  1. Ametengua uteuzi wa Ndugu Abdallah Mohamed Malela, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara. Badala yake amemteua Bi. Bahati Ibrahim Geuzye kuwa katibu Tawala Mkoa wa Mtwara. Kabla ya uteuzi huu, Bi Bahati alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
  2. Amemteua Ndugu Mohamed Jumanne Gombati kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Geita. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Gombati alikuwa Mkurugenzi Msaidizi
    Sehemu ya Maafisa Waandamizi katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
WAKUU WA TAASISI
  1. Amemteua Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Aidha aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Bw. Omar Issa ataendelea na majukumu mengine aliyopangiwa katika Ofisi ya Rais - Tume ya Mipango.
  2. Amemteua Ndugu Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Chande alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
    Anachukua nafasi ya Mhandisi Peter R. Ulanga ambaye atapangiwa kazi nyingine.
  3. Amemteua Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Kabla ya uteuzi huu Ndugu Nyamo - Hanga aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
  4. Amemteua Dkt. Erasmus Fabian Kipesha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Kipesha alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (TEA).
WAKUU WA WILAYA
  1. Ametengua uteuzi wa Ndugu Hanafi Msabaha, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini na badala yake amemteua Bi. Mwanahamisi Mkunda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini. Kabla ya uteuzi huo Bi. Mkunda aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.
  2. Amemteua Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Mariam Chaurembo atapangiwa kazi nyingine.
WAKURUGENZI WATENDAJI WA HALMASHAURI (MA -DED)
  1. Amemteua Ndugu Hassan Bakari Nyange kuwa Mkurugenzi (DED) wa Mtwara TC. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Nyange alikuwa DAS Wilaya ya Namtumbo. Aidha, aliyekuwa Mkurugenzi (DED) wa Wilaya ya Mtwara TC, Kanali Emmanuel Mwaigobeko atapangiwa kazi nyingine.
  2. Ametengua uteuzi wa Bi. Tatu Said Issike, Mkurugenzi wa Mtwara DC na kumteua Ndugu Abeid Abeid Kafunda kuwa Mkurugenzi (DED) wa Mtwara DC. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Kafunda alikuwa Mwanasheria katika Ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali.
  3. Amemteua Ndugu Reuben Sixbert Jichabu kuwa Mkurugenzi (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndugu Erica Yegella atapangiwa kazi nyingine.
KATIBU TAWALA WILAYA
Amemteua Ndugu Francis George Mgoloka kuwa Katibu Tawala wa Wilaya
(DAS) ya Namtumbo. Kabla ya uteuzi huo Ndugu Mgoloka alikuwa Katibu Tarafa Mswaki - Kilindi Handeni.

Katibu Mkuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wataapishwa siku ya Jumanne saa sita mchana Ikulu, Dar es Salaam.
View attachment 2759138
View attachment 2759139
View attachment 2759157

Hii issue kuwa mtu aki underperform mahali anahamishwa badala ya kuwekwa pembeni wapewe candidates wanaoweza hii kazi , ina tu cost sana hii nchi
 
Sawa,ila hana ufanisi.
Ni miongoni mwa akina mama ninaowakubali sana hapa jukwaani kwa michango unayotoa na kuchangia ila kwa hili naona kabisa kuwa unaelekezwa na nafsi kuliko ukweli ulivyo japo haijabadili muono wangu kwako

Wengi inawezekana ni kwa kuangalia nasaba za kiimani kwa jina lake bila kuangalia utendaji wake kuanzia mwanzo mpaka hapo pa kupewa ttcl na hata alipotokea pale tanesco wabaya wanaangalia ukatikaji wa umeme ktk msimu huu(kuna sbb nyingi ambazo zipo nje ya uwezo wake)ila pale kafanya makubwa ya kukumbukwa na kusifiwa kama alivyofanya kwenye mashirika na taasisi nyingine za kiserikali na binafsi alizopitia ktk safari yake ya kitendaji
 
Back
Top Bottom