Mahojiano ya BBC na Waziri Tax yalipokwenda mrama

Mahojiano ya BBC na Waziri Tax yalipokwenda mrama

Nimekaa MFA for several years kabla ya kwenda viwanja na huyo mama ni mbobevu mzuri tu. Kumtendea haki nakushauri isikilize ile clip ya dakika 7 kabla ya kufanya conclusions.
mkuu kwenye clip kahojiwa maswali mazuri sana na amejibu vizuri but hapo mwishoni amemaliza vibaya!..hao waandishi wa TV za kimataifa ni wabobevu sana hakuna ukanjanja kama locals..the best way kudeal nao ni kuwa focused na calm na kutotoa majibu ya kukariri.

..na pia hiyo interview ukisikiliza kwa umakini mwanahabari ameongea kwa utulivu kabisa..kuna vipindi vya BBC kama hardtalk wanahabari wanawahoji watu powerful zaidi ya mh waziri na maswali very provocative but wanajibiwa bila shida..angeweza kufanya better than that!
 
Huyo mama vyema ikumbukwe alikuwa waziri wa ulinzi, bado hajazoea kazi mpya.
 
Mkuu bado kuwa Civil Servant na kuwa Diplomat ni vitu viwili tofauti.

Huwezi kumfananisha Dr Tax na mzee Membe mmoja ni Civil servant na mwingine ni top diplomat.

Mimi nimeangalia conlusion ya maongezi, na madiplomat huwa hawamalizi kwa namna hiyo kwa kuzingatia hadhira ni dunia nzima.

Ukizingatia kuna ugeni mwingine ulikuwepo kutoka Russia.

Kwenye duru za kidiplomasia huwa kuwakuwa na masuala mengi ya kutaka kuyasikia kutoka kwenye hizi interviews.

Izingatiwe interviewer kasema wazi kuwa bado alikuwa na maswali zaidi. Pia kaulizia kama Waziri hakuwa tayari kujibu lolote tena. Ingekuwa hard talk vibao visingeweza kurushwa?

Ukipenda boga penda na ua lake ila Mh. Waziri kachemsha!
 
Why calling darling? Unanijua?
We Lusungo na wewe unakuwa kama hujui hata JF members ni human beings!, baada ya kuitwa darling, unaitwa bebi, mtu anakushukia pm, mwishowe...
We vipi vitu vidogo hivi huelewi!. Mimi mwenzako nimeisha kirimiwa sana na wana jf!, kuna wana JF wenye roho nzuri huwezi kuamini!, ukiitwa darling, just respond the same!, faida ni nyingi kuliko hasara!.
P
 
Vituko vyake nini? Katika majibu yote ya huyo mama kakosea nini?

Kituko ni kula Kona na kuvunga kufa kwa kumshukuru mtangazaji kwa kuwa naye kana kwamba interviewer alikuwa yeye.

Jingine ni kula Kona bila Taarifa Hadi kufikia kuulizwa hutaki Maswali zaidi?

La mwisho ni interviewer kuifahamisha dunia kwamba alikuwa Bado na maswali zaidi.

Kwani kupata nafasi za kuiuza nchi kimataifa siyo fursa kuliko Hata royal tour.

Hii ni fursa imepotea.
 
Hii ilikuwa interview ikisikilizwa duniani kuhusu ujio wa makamu wa rais wa Marekani:

View attachment 2571442

Ama kwa hakika shughuli ipo.

Labda itabidi kuomba mwongozo kufahamu ni sehemu ipi kama ipo kktunayofanya vizuri.
Ya CAG nani hajayasikia? Mama amejizungushia viongozi vilaza ili aonekane ni bora kumbe anajiabisha. Fedha kaweka wezi, nje kaweka wasiojua kazi zao, utalii wakweze, mno ya ndani Uzanzibari baada ya weledi, ulinzi n
 
Gulwa ninaiunga mkono na hoja Yako;

"Mama amejizungushia viongozi vilaza ili aonekane ni bora kumbe anajiabisha. Fedha kaweka wezi, nje kaweka wasiojua kazi zao, utalii wakweze, mno ya ndani Uzanzibari baada ya weledi, ulinzi nk"

Una hoja nzito.
 
We Lusungo na wewe unakuwa kama hujui hata JF members ni human beings!, baada ya kuitwa darling, unaitwa bebi, mtu anakushukia pm, mwishowe...
We vipi vitu vidogo hivi huelewi!. Mimi mwenzako nimeisha kirimiwa sana na wana jf!, kuna wana JF wenye roho nzuri huwezi kuamini!, ukiitwa darling, just respond the same!, faida ni nyingi kuliko hasara!.
P

Mnaweza kulalama ila kujitoa ufahamu kutetea lisilowezekana linakuwa na ule ukakasi wa kuhusianishwa na teuzi.

La kuvunda halina ubani.

"Ukionejana unakomaa kufukiza ubani usingependa mtu asijirishe kama si jitihada binafsi za kusaka fursa?"
 
Nadhan Mhe. Tax ni mzoefu sana kwenye platforms za kimataifa. Atakuwa alinusa maswali yanayofuaya... Kama Upunga..akaamua kukwit
 
Sifa kuu ya kwanza kwa mwana diplomasia ni kuwa diplomatic!.
One doesn't have to be rude without just cause!. Being very confident is always good in diplomatic relations.
P
Maskini alitaka kukwepa swali la ushoga! Huwezi kuwa diplomat bila kujua kukwepa mishale! Diplomat huwa ni mnafiki hatoi jibu la kuangukia upande mmoja! Majibu ya diplomat huwa ni may be, tutaona, tutajadiliana etc. Tunasema JPM hakuwa diplomat kwa vile alisema anachokiamini ila JK alikuwa diplomat. Huwezi kujua msimamo wake, unafiki mwingi. Tax anatakiwa kuwa kama JK katika meza ile, asisahau kuwa alianza kazi kama secretary
 
Huyo muuliza maswali alionesha utoto wa hali ya juu sana licha ya huyo waziri kuwa calm na very focused kwenye alichoulizwa.

Mtu anafanya repetition zisizo na msingi na anaukiza maswali katika njia ya kutaka kusikia unayopenda au uliyopanga!

Waziri ni mtu mzito sana huwezi kumwekea maneno mdomoni.. huyo mama alifikia hadi kumwambia hawezi predict boss wake angejibu nini bado akaendelea kufanya utoto mbaya zaidi ni kama alikua akifanya mashindano flani na kudhamiria kumu outsmart waziri. Hivi waziri alivyo na ishu nyingi za kushughulikia unamfanyia utoto kiasi kile?

Huyo mwandishi ni wa hovyo sana
Huyu maza yupo very smart
 
Kazingua kinoma, nawaza kwa mtu calibre yake aliyepata kushika nafasi kubwa SADC.
Lakini unategemea makubwa gani from SADC experience, mkusanyiko wa nchi kama Tanzania, anapata exposure gani ambayo hapa Tanzania hakuna ?

..... Madagascar, Malawi, Zambia, Eswatini, Msumbiji, Angola, Lesotho, Congo, Zimbabwe, ....

I am not in the least surprised, most of these states ni mi dictatorships ambayo hakuna free press ya kusema spokespeople watanolewa kuweza kuchambua mambo, kujieleza, na kwenda toe to toe na mwandishi kutoka nchi huru za Ulaya.... hawawezi....

Ameshindwa kumwambia hata sababu ya kukatisha interview, anabaki kusema ahsante ahsante ahsante....

Hizi kazi za kuongea kifua mbele na kutetea misimamo ya Afrika walikuwa wanaziweza kina Waziri Ben Mkapa, Oscar Kambona, kidogo Salim Salim na baba yao Kambarage.
 
Huyo mtangazaji wa BBC huwa namkubali sana hasa pale anapofanya mahojiano, sauti yake, utulivu kwenye kuongea na aina ya maswali pia kiufupi hachoshi kuendelea kumsikiliza.

Focus on Africa ndio kikikuwa kipindi changu pendwa
 
Back
Top Bottom