Mahojiano ya Mkurugenzi Mkuu TANESCO ni usanii mtupu

Mahojiano ya Mkurugenzi Mkuu TANESCO ni usanii mtupu

Hawa kina Maharage Chande kazi imewashinda kabsaa,wameandaa slide kuhadaa umma hatua za JNHP,wakati si kweli,
Kigoma wamezima majenerata,umeme mdogo, unakatikakatika na kusuasua, katoa majibu ya kibabaishaji akimuingiza Ndalichako kutafuta huruma, nonsense kabisa.

Mkurugenzi hilo la kigoma ni jipya kwakwe,kweli?,pia gesi imeshindwa kusaidia upungufu wa umeme, hapo tanesco wamebinafsisha customer care services, hivi kweli walishindwa kupata watanzania competent kureplace wazembe waliokuwepo customer care?,wakawaboreshea maslahi na mikataba mizuri?, wakaamua kubinafshisha kitengo?,wizi huo,

Hawa acha wamuingize chaka rais Samia,au pengine n na yeye ni mnufaika,

Magufuli aliwezaje?,hawa mbona visingizio vingi sana na kujifanya eti wao hawataongopa,ni wakweli, nonsense!,porojo na lugha laini,wananchi wanateseka,

Hii nchi mpaka mapinduzi ya uongozi yatokee tena ni lazima kabisa , vinginevyo tunasindikiza kundi la wahuni kwa woga wetu.
Mtu anaitwa Maharage kweli?
 
Maharage ni smart guy
Tulitakiwa kuona huo usmart kwenye field as long as umeme una katika hivyo wote waliopo kwenye field hiyo kuanzia mfanya maamuzi Rais hadi kwa mtendaji wote ni matatizo.

Huwezi mtoa MTU huko alikuwa anasambaza masidishi ya DSTV na kumleta kuongoza shirika ambalo ndio nguzo ya uchumi Tanzani.Mbaya zaidi watu wote tunakaa kuwaangalia tunategemea walete majibu-poor us.
 
18 November 2022
Mradi wa Line Kubwa ya Umeme KV400 Wasuasua

Kampuni yenye makao yake bara la ulaya ya kusini nchini Bosnia-Herzegovina yamkasirisha mkuu wa mkoa wa Arusha baada ya kampuni hiyo kuchelewesha mradi wa njia kubwa ya umeme KV400 toka Singida kwenda Arusha hadi Kenya na ungesaidia kukunua umeme wa ziada toka Kenya na Ethiopia hivyo kupunguza makali ya mgao wa umeme


Source : wasafi media

Mradi wa Kenya – Tanzania Power Interconnector Project (KTPIP) kukamilika mwezi February 2020
Mradi huo wa kusafirisha umeme wa kV400 kutoka Singida hadi Namanga utaunganisha nchi za Tanzania na Kenya na unafahamika kama (Kenya – Tanzania Power Interconnector Project), (KTPIP).

Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu alisema hayo alipotembelea eneo la kuhifadhia vifaa vya mradi huo (yard) katika kijiji cha Nangwa wilayani Hanang mkoani Manyara, mwishoni mwa wiki, ili kukagua vifaa hivyo vitakavyotumika katika ujenzi wa miundombinu ya umeme.

Mgalu alisema kuwa, kazi za awali za utekelezaji wa mradi huo zilikwishaanza na kinachosubiriwa sasa ni kukamisha zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha mradi husika ili wakandarasi waanze rasmi kazi ya ujenzi.

Mgalu aliweka wazi kuwa, katika utekelezaji wa mradi huo, vijiji 14 vilivyopitiwa na mradi vitapata umeme ambapo vijiji 7 ni vya Mkoa wa Singida, 2 kutoka Mkoa wa Manyara na 5 ni vya Mkoa wa Arusha.

Alisema kuwa, mradi huo, pia utawezesha ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme mjini Arusha na kupanua kituo cha kupoza umeme mkoani Singida.

Alisema kukamilika kwa mradi huo kutatimiza azma ya Serikali ya kuwa na umeme mwingi na wa kutosha ifikapo 2020, na pia kuuza umeme katika nchi za Afrika Mashariki zitakazokuwa zina uhitaji, kupitia Ushirikiano wa pamoja katika Sekta ya Nishati ujulikanao kama East African Power Pool, (EAPP) unaoshirikisha nchi za Uganda, Ethiopia, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini pamoja na Kenya.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya na Hanang, John Mkirikiti alisisitiza kuwa utekelezaji wa mradi huo uzingatie na kutoa kipaumbele cha ajira kwa vijana wenye nguvu walio katika maeneo yanayopitiwa na mradi.

Pia aliahidi kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa mradi huo hususan kuimarisha ulinzi na usalama, na kuwataka vijana watakaopata fursa ya kufanya kazi katika mradi kuwa waaminifu na wakazi wa maeneo ya mradi kuwa walinzi wa miundombinu hiyo ya umeme.

Akizungumzia ujenzi wa mradi huo, Meneja Msimamizi mkuu wa Utekelezaji wa Mradi huo, kutoka Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) Mhandisi Oscar Kanyama alisema kuwa upande wa Tanzania mradi huo utajengwa kwa urefu wa kilometa 414 na kwa upande wa Kenya utajengwa kwa urefu wa kilometa 96 kutoka kituo cha kupoza umeme Isinya hadi Namanga.

Mhandisi Kanyama alisema mapema mwezi ujao kazi za kuchimba mashimo pamoja mitaro kwa ajili ya kujenga misingi ya mradi huo itaanza.

Aliweka wazi kuwa mradi huo umefadhiliwa na Serikali ya Tanzania iliyotoa Dola za Marekani milioni 44, Wadau wa Maendeleo ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) iliyotoa Dola za Marekani milioni 258 na Shirika la Mandeleo la Japani ( JICA) lililotoa Dola za Marekani milioni 89, mradi huo unatarajia kukamilika mwezi Februari 2020. Source: TANESCO - Wananchi waliopisha mradi umeme wa kV400 kutoka Singida hadi Namanga waanza kulipwa fidia.
 
Mwaka 2014 haijafika bado ili tuuze umeme nje.
1668805251664.png
 
Projects ni priority with time...
1. Ajira zimetolewa ( miaka 5 hakukua na ajira)- afya+ elimu
2. Mashule+ hospitali zimejengwa kila kijiji
3. Mbolea za ruzuku+ masoko kwa wakulima
Hivyo vyote visingeweza kusubiri bwawa likamilike....
Hizo zimeanza kufanyika kuanzia awamu zilizopita.
 
Nimelipia kuunganishiwa Umeme tangu 25/2/2022 Hadi Leo naambiwa hakuna vifaa. Hii nchi mzaa mwingi
Halafu hii nchi nimegundua wanapenda maneno matamu sio kazi na utekelezaji wa majukumu mkurugenzi wa hovyo kabisa kwenye shirika nyeti kwa taifa
 
Tulitakiwa kuona huo usmart kwenye field as long as umeme una katika hivyo wote waliopo kwenye field hiyo kuanzia mfanya maamuzi Rais hadi kwa mtendaji wote ni matatizo.

Huwezi mtoa MTU huko alikuwa anasambaza masidishi ya DSTV na kumleta kuongoza shirika ambalo ndio nguzo ya uchumi Tanzani.Mbaya zaidi watu wote tunakaa kuwaangalia tunategemea walete majibu-poor us.
Mapinduzi muhimu sana kawa west afrika
 
una
Upezi San watolewe nduki akauze vingamuzi za DStv

Mkp huyu jamaa anaondoka taifa litakuwa maskini kuliko vipindi vyote
Nilidhani una point kumbe una chuki zako tu binafsi na maharage chande.

Kiufupi kwangu mimi nimemuelewa na yuko vizuri kimipango na kiutekelezaji
 
Ukiwasikiliza unaweza dhani watu wa maana kweli.

Mie niliukuta mdahalo kati wakati natafuta taarifa ya habari ITV YouTube.

Niliposikia tu analalama unit cost wanauza 33% chini ya production costs, halafu hapo hapo wanawekeza kwenye vyanzo ambavyo unit costs zake ni kubwa mwanzoni, na uwekezaji wenyewe ni private (ndio ubia wenyewe) halafu anasema TANESCO ni 100%, nikaona sina sababu ya kusikiliza upuuzi unaofuata.

Hivi wanadhani Magufuli alikuwa mpuuzi kutoipa miradi mingine yeyote kipaumbele na ku focus kwenye mmoja tu ambao ukiisha ni mwarobaini kwa miaka kama kumi ijayo, wengine waongeze vyanzo vingine ndani ya huo muda wakati tunajimudu.
Tupe ushahidi kuwa gharama za kuzalisha umeme ziko chini kuliko gharama za kuuza umeme. Acha kubwabwaja
 
Back
Top Bottom