Hahaha... asingenipa heshima yangu bila ya kufanya hivyo. Unajua Nakadori sina maana mbaya ya kusema hivyo lakini, mambo ya mahusiano baina ya mwanaume na mwanamke, ni kama mchuano baina ya jinsia hizo mbili. Na atakayetumia akili vizuri atamuwin mwenzake na kuwa in-control. Ndiyo maana hata mfunguaji thread, kama ni mwanaume anaweza kuja kulia kwamba amepigwa tukio, na member mwanamke pia anaweza kuja kulia kwamba amepigwa tukio, hiyo inamaanisha alizidiwa akili na mwenzake. Kwa hiyo alivyotaka kunipiga tukio, nikasema huyu lazima nimu-outsmart ili asije akanidharau.