Mahusiano Mapya ya Mara kwa Mara ni Umalaya au Safari ya Kumtafuta Mtu Sahihi?"

Mahusiano Mapya ya Mara kwa Mara ni Umalaya au Safari ya Kumtafuta Mtu Sahihi?"

Kuna watu wanaohesabu hii kama umalaya

Kuna wengine wanaamini ni sehemu ya kujaribu mpaka umpate yule mtu ambaye mnaendana

Mimi binafsi naona kuwa na mahusiano mapya mara kwa mara sio tatizo sana

Nadhani hii hutokea pale unapokutana na mtu, mkajenga ukaribu, halafu ukagundua kwamba kumbe hamwendani

Mara chache sana utagundua hilo mwanzoni

Mara nyingi linajitokeza baada ya mazungumzo ya mara kwa mara na kuanza kujuana kwa undani

Ukikaa makini utaanza kugundua akili ya mtu kupitia maongezi yake

Namna anavyoongea akiwa na hasira, akiwa na huzuni, akiwa na furaha au akiwa kwenye changamoto mbalimbali

Hapo ndipo unaanza kuona huyu mtu ni nani hasa

Kosa ambalo naona linawagharimu wengi ni kufanya sex mapema

Sex ya mapema ikishafanyika halafu baadaye ukagundua kuwa hamwendani kwenye mambo mengi, ndipo watu huanza kujilaumu

Wengine hujihisi kama walijitoa kwa mtu ambaye hakuwastahili, wakaanza kuona kama waliji-expose kwa mtu ambaye asingepaswa kuwafikia

Lakini kama baadhi yetu tungekuwa tunapeana muda wa kujuana kwanza, hata kama si mrefu sana, naamini majuto yangepungua

Pia kila mmoja angeweza kulinda heshima yake na kufanya maamuzi akiwa na uhakika zaidi

Lakini sasa kujuana leo kesho jigijigi 😎

Kwa upande wangu, sioni tatizo kuwa na mahusiano mapya ikiwa lengo ni kumpata mtu ambaye mnaona mnaweza kwenda naye sawa

Maana unaweza kumdate mtu, halafu kadiri muda unavyokwenda unaanza kushangazwa na matendo yake, na namna anavyofikiri Mwishowe unajikuta unauliza, Hivi huyu kweli kwa akili hizo hakuna kitu hapa sioni kama kuna tatizo ukiachana nae kuliko kupandisha maji mlima

Swali la mjadala:👇

Wewe unaonaje? Ni vibaya kuanzisha mahusiano mapya mara kwa mara?

Na kama ni vibaya kwa nini?

Au unagubu mwanetu? 😎

ShesRise_1 ✋️
Ni safari ya kutafuta UTI na baadae UKIMWI
 
Ahaa sawa
Mabinti waache kutumia miili yao kama majaribio ya mtu sahihi, kwenye umri wa foolish age hadi kabla ya 30 wengi wao wanapenda wanaume wasiyoeleweka wakija kushtuka na kubadili basi ni namna ileile anayemwona tofaufi. Mahusiano yetu mitikasi ni kama mafuta kwenye bosa, arachakazwa tu

Muda huo wanaompenda hasa hawezi kuwaona na maana sababu wanaeleweka na si kama wanaomuumiza kichwa.

Mtu anapendwa ila kazi kumpa kisogo na kunusanusa kwingine kama paka.
 
Ahaa mabinti wamesikia
Muda huo wanaompenda hasa hawezi kuwaona na maana sababu wanaeleweka na si kama wanaomuumiza kichwa.

Mtu anapendwa ila kazi kumpa kisogo na kunusanusa kwingine kama paka.
Aisee ni hatari sana
Asante mkuu
 
Back
Top Bottom