Mahusiano yako hayana afya kama unaishi na mtu anayeombaomba hela


Na haupo CHAPUTA mkuu? 😁
 
Watu wanatoa pesa bwana wewe!!
 
Hamna mama mchungaji, tatizo tunachagua sana. Hutaki kuishi na mwanamke anayeonesha kukupenda unamtaka yule pisi kali anayetafutwa na mtaa mzima.
Mtumishi si mlisema hao mnajipigia tu mnaoa sisi we ye sura za baba zetu? Mwanamke akikupenda unaenjoy eti? Pisi za mtaa zitawaponza na yutiyai za kimbwaa!!
 
Surely, Hii ni elimu wanapaswa kufahamu wengi wetu...lakini pia inategemea na akili ya huyo Mwanamke again
Kweli inategemea ila kwa sasa wanawake wengi wanazichangamkia fursa , kuliko umpe hela ya chips kila siku ,mpe mtaji wa kufuga kuku wa mayai mzipike hizo chips nyumbani na muuze mayai , hawezi kosa hela ya kusuka , kuweka kucha rangi , kununua pochi mpya na abaya lake.

Wengi mnaogopa mwanamke awe na uhuru wa kipato mkifiria wanawapanda kichwani ndio maana mnawapa hela za matumizi na sio za hela za wazo la biashara.

Ni vile tu sipendi kuongelea mambo ya mahusiano sana, ningewapa njugu mshindwe mwenyewe tu kutafuna vijana😁😁😁
 
Option ya kununua ni nzuri japo ina ukakasi sana mkuu. Napiga story na vijana wengi, nao wanaona ni heri kununua kuliko kujibebesha mizigo. Kibubu kikijaa unatafuta 10k unapata shots zako mbili umemaliza.

Mimi kununua siwezi, nitatafuta tuu yule ambae hajawa fisi kupindukia, tutaenda nae kimtindo, mahitaji ya msingi nitampa kadiri ya bajeti, ila akianza utapeli napiga chini.
Wanawake wenye fikra nzuri bado wapo wakulungwa, japo ni shida kuwapata.
 
sema kuishii nao kwa akili, maana huwezi ishi bila kuwa ndinya 😁
 
Hahaha kwamba unakuta kwa mashoo zake anatamba kuna boya anamchuna?🤣🤣🤣💔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…