Nihilist
JF-Expert Member
- Jun 11, 2022
- 226
- 353
Ni miaka 36 imepita tangu pale mvulana huyu azaliwe kwa furaha ya wazazi iliyoje kupata mtoto wa kiume wakifahamu wameleta mwana wa kuwaongezea ukoo na kuwafanya wajivunie kwa kupata wajukuu na huenda vitukuu na vilembwe, masikini pasina kufahamu kuwa mtoto huyo ana mapungufu makubwa ambayo kama wangeliwahi kushughulikia kijana wao katika umri huu angelikuwa na wajukuu wao na kwa furaha wangelizeeka kwa furaha ya kusumbuliwa na vitukuu vikicheza pembeni yao na kuwasumbua huku na huko, wakijiona sura zao za utotoni kwenye nyuso za wajukuu wao..
Kijana alizaliwa na tatizo linalojulikana kitaalamu kama "Undescended Testes".
Hili ni tatizo linalotokea kwa mtoto wa kiume baada ya kuzaliwa na korodani kutokutokea kwenye eneo lake huenda ni korodani moja au zote mbili (kwa mujibu wa daktari).
-Tatizo hili hufanyiwa matibabu mara tu linapogunduliwa kati ya mwezi mmoja hadi mwaka mmoja tangu mtoto kuzaliwa na siyo zaidi (alisema daktari).
-ikipitiliza katika muda huo huweza kuleta hatari ya kupata kansa na kusababisha kifo.
Tuendelee....
kwa kutokulifahamu hilo wazazi walimwacha mtoto wao kukua wakiamini hakuna tatizo linalomsibu litakalo muhuzunisha maishani milele..
Kasheshe imeanza pale kijana kakua na kujitambua ujanani kakutana na wasichana wa kila aina warefu wafupi weupe weusi bado bila bila hakuna ata mtoto wa kusingizia.....mmmh awapo shuleni akafanya siri maana ni kinyume na maadili na sheria za nchi mwanafunzi kuwa na mahusiano na tena chini ya umri under 18....
Baada ya kuhitimu masomo na kurudi mtaani kupambana akapata kazi nzuri kajenga na ana miradi ya kuweza kumuingizia pesa ya kuweka milo mitatu mezani, anakumbuka kuna jambo haliko sawa wapi mtoto wapi mke..?
itaendelea