Nikuulize swali fupi tafadhari...
Kwanini unaishi...?
Ni swali ambalo nimejiuliza mara nyingi sana japo sijawahi kuyafungulia thread jf 🙏🙏
Ninaishi kwa sababu nina uhai ambayo ni zawadi kubwa kuliko zote maana kama kuna kitu ambacho billion ya watu waliolala kaburini wangepewa nafasi bhasi wangeomba pumzi hata ya dakika tano tu ili wajirekebishe au warekebishe kitu flani maana uhai ni fursa ambayo kila binadamu anapewa ONCE
Ninaishi kwa sababu nimeijua impact yangu kwenye maisha ya watu wengine, sio watoto maana sina japo umri ni sahihi kuwa nao Ila watu ambao nimejitolea kwao. Professionally na kikawaida kiushauri hata kuwasaidia wasiojiweza. Nipo naturally selfless na hakuna kitu nainjoi kama kusaidia watu, kwa kila tumaini na tabasamu nalolisababisha kwao, it means a world to me
Ninaishi kwa sababu nimeijua nafasi yangu na kujiangalia katika uhalisia wangu. Kuzimiliki na kuzikubali kasoro zote nilizonazo,
magumu hote niliyopitia na ninayopitia pamoja na makosa makubwa niliyoyafanya
Yote hayo yamenifanya kuwa mimi na kuna viatu ambavyo navivaa kwa sasa, ninaamini nisingekuwa hivi nilivyo nisingeweza, labda ningekuwa na kazi serikalini, nimeoa nina watoto na maisha yameishia hapo
Ila kwa utofauti wangu ndio umenipa nafasi ya kuyaona maisha katika angle tofauti ambayo wengi hawaioni, maisha yamenipa jukumu ambalo si kila mtu analo and in sha allah, siku moja nitafanikisha
Hiyo ndio core ya maisha yangu, sio watoto , sio mke, sio ndugu, sio familia but MYSELF 🙏🙏🙏