Maisha bila korodani (Testes) hayana umuhimu kwa ulimwengu huu wa familia

Maisha bila korodani (Testes) hayana umuhimu kwa ulimwengu huu wa familia

Shukuru Mungu tu kuna wengine wana testes zote lakini hawana uwezo wa kuzalisha,kuna wengine wana watoto lakini watoto hao hao wanakuja kuua wazazi wao
 
Shukuru Mungu tu kuna wengine wana testes zote lakini hawana uwezo wa kuzalisha,kuna wengine wana watoto lakini watoto hao hao wanakuja kuua wazazi wao
Ukiwa na Testes unaweza toa mbegu zako wakampandikizia mwanamke ukapata dume lako la mbegu likakujari uzee ila siyo mimi....😪😪😪😪
 
Sasa lengo lako la kusimulia vipisi vipisi pasipo kumaliza ndio nini?;unakera Hata kama ni mgonjwa.
Pole ila mimi ni mvivu kuandika na pia natumia simu hivyo nahofia kuandika uzi mrefu na baadae ukafutika nikaanza upya....ni ndefu kidogo vumilia....😪😪😪
 
Inaendelea ...

Baada ya kutoka hospital ndipo ugumu wa maisha na majuto ndipo yanaanza.....

-Mwili kuwa na uchovu wa muda mrefu ata pale nikipumzika au kushinda muda mrefu bila kufanya kazi,nachoka bila sababu..

- Kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa muda mrefu ( naweza kukaa ata mwezi mzima bila kumuwazia mwanamke )...mwanamke ndiye anayeniomba kufanya mapenzi kila mara...

-Kuwa na Hasira za ghafla na za mara kwa mara tena zisizoisha kirahisi...mfano unaweza nikosoa kidogo huenda kwa nia njema nikakupandia juu tena kwa lugha mbaya na yenye kejeri ila zikipoa najishangaa kama ni mimi niliongea na kufanya vitendo hivyo...

-Kuwa kwenye wimbi la maswali ya muda mrefu yasiyo na majibu, kuongea mwenyewe barabarani tena kwa sauti bila kujijua nakuja shituka watu wananitizama navunga kama naimba...😟😟😟..

-Kuwa na mshtuko na mfedheheko wa moyo ghafla kwa suala dogo mfano kupata hasara ya pesa kidogo kwa mfano hasara ya shilling mia na hapo nina laki ya matumizi ya siku na siyo kawaida yangu nilikuwa mtoaji wa pesa ila sasa ni tofauti...

-Napenda kujitenga maana nahofia kuchukizana na marafiki zangu nikifahamu kuwa wakiniudhi kidogo tu mimi ni dakika tano mbele urafiki unakufa tena kwa matusi na vitisho vya maisha nikituliza akili najishangaa nilikuwa mimi kweli huyo??......

Ila kuna kifungo cha matibabu kinaitwa therapy haijalishi ni ya vidonge,sindano na mafuta ambayo nahofia nikiingia huko yaani hadi UMAUTI UTAKAPONIKUTA...

MWISHO
 
Najitahidi ila ninapokuwa pekee yangu haya maswali yanakua magumu kujibu

1:-Nahangaika kutafuta mali namtafutia nani.?
2: -unapokosa korodani kuna homoni zinapungua na utendaji kazi unapungua ....
Sasa namuangaikia nani..?
3:-Je naweza kurudisha korodani hizo?

Ukiishi kwa kujilinganisha na, watu wengine itakuwa ngumu kwako kujiona una thamani yoyote duniani

Jiulize, kwani ukifariki na mali ukamuachia mtoto ambaye atazitawanya au la mtoto afariki kabila yako, zitakuwa na faida gani

Sumu kubwa tunayolishwa ni kuamini kuwa thamani zetu zipo attached na vitu au watu na pale tunapowakosa tunaona chochote tulichonacho hakina faida.. Ila huu ni uongo

Wewe ndiye mtu wa kwanza anaestahili kuinjoi na kufurahia jasho lako kabla ya yoyote yule

Jipende na ujithamini kwa kila kitu ulichonacho lakini kwa kuwa wewe unaona thamani yako ni watoto

Bhasi jaribu uende hata kwa watoto yatima au wagonjwa wasiojiwwza, watolee chochote ulichonacho, zile shukrani pamoja na maombi yao pamoja na kukutegemea, sidhani kama kuna mtu huwa anatoka nje yao bila kujihisi significant kwenye dunia hii

Kiufupi jitahidi utengeneze system ya maisha ambayo itakidhi mahitaji yako na kukufanya ushukuru na kutumia kile ulichobarikiwa nacho. Kuwa na system itakayokuchukulia ww kama ww na sio unavyotamani uwe

malizia story pia 😁😁.. All the best
 
Mi korodani zangu naona hata hazina kazi, mzigo tuu.
Usiseme hivyo korodani ndizo zinakupatia hizo nguvu ulizo nazo (siyo za uanaume pekee) yaani za kufanya kazi zina homoni inaitwa testosterone ndiyo kila kitu kwa mwanaume
 
Ukiishi kwa kujilinganisha na, watu wengine itakuwa ngumu kwako kujiona una thamani yoyote duniani

Jiulize, kwani ukifariki na mali ukamuachia mtoto ambaye atazitawanya au la mtoto afariki kabila yako, zitakuwa na faida gani

Sumu kubwa tunayolishwa ni kuamini kuwa thamani zetu zipo attached na vitu au watu na pale tunapowakosa tunaona chochote tulichonacho hakina faida.. Ila huu ni uongo

Wewe ndiye mtu wa kwanza anaestahili kuinjoi na kufurahia jasho lako kabla ya yoyote yule

Jipende na ujithamini kwa kila kitu ulichonacho lakini kwa kuwa wewe unaona thamani yako ni watoto

Bhasi jaribu uende hata kwa watoto yatima au wagonjwa wasiojiwwza, watolee chochote ulichonacho, zile shukrani pamoja na maombi yao pamoja na kukutegemea, sidhani kama kuna mtu huwa anatoka nje yao bila kujihisi significant kwenye dunia hii

Kiufupi jitahidi utengeneze system ya maisha ambayo itakidhi mahitaji yako na kukufanya ushukuru na kutumia kile ulichobarikiwa nacho. Kuwa na system itakayokuchukulia ww kama ww na sio unavyotamani uwe

malizia story pia 😁😁.. All the best
Sijilinganishi na mtu....ila hakuna raha duniani kwa mwanaume kama kupambana mtaani kuzisaka halafu ukirudi umechoka mke anakupokea mizigo mtoto wako anakukimbilia kwa furaha na shibe ya kile unachomtafutia......
 
Attachments

  • images.jpg
    images.jpg
    6.9 KB · Views: 10
Sija-complicate sehemu mimi nilikuwa mtoto nisiye na ufahamu wowote kuhusu hili kuja kujitambua it's too late...
Ok ata hivyo hakuna namna ni kuishi tu kama vile sikuwahi exist.....
Mie naona umekata tamaa....Mungu ndo jibu...tulia...kama hakuna tatizo siku isiyo na siku huenda ukafunguliwa kimaajabu
 
Pole sana mkuu, castration ina madhara mengi sana, najua unachokipitia ni kigumu, nilishawahi kusoma hiyo kitu, jaribu kuwa mvumilivu tu, maisha ni vita kwa kila mtu, hivyo kila mtu yupo kwenye vita yake.
Unaonekana upo depressed sana na umekata tamaa, trust me your life could be worse.
 
Sijilinganishi na mtu....ila hakuna raha duniani kwa mwanaume kama kupambana mtaani kuzisaka halafu ukirudi umechoka mke anakupokea mizigo mtoto wako anakukimbilia kwa furaha na shibe ya kile unachomtafutia......
Mkuu hapa watu wanajaribu kukupa moyo na tumaini kuwa sio wote waliozaliwa walipata watoto. Na kama tatizo limeshatokea na hakuna jinsi toa hayo mawazo ya watoto ishi maisha yako na kwa sasa endelea kujisaidia kuondoa zile outcomes zitokanazo na hilo ttz mfano hasira kukosa hamu ya tendo n.k n.k kwa kutafuta therapy. Pole sana sana
 
Sijilinganishi na mtu....ila hakuna raha duniani kwa mwanaume kama kupambana mtaani kuzisaka halafu ukirudi umechoka mke anakupokea mizigo mtoto wako anakukimbilia kwa furaha na shibe ya kile unachomtafutia......

Hiyo furaha umewahi kuihisi wapi kama si kwa kusikia au kuona vile watu wengine wanavyoielezea

Furaha ya kuona sex ni kila kitu duniani kiasi kwamba ukikosa uwezo wake unajiona huna ulichobakiza duniani

Furaha ya kuona mtoto ni kila kitu

Ina maana wewe ulipozaliwa hadi unafikia umri wa kupata mtoto, uwepo wako duniani ulikuwa useless kwa sababu hukuwa na mtoto???...

Mkuu nakuelewa unavyojihisi na una sababu zote za kujihisi hivyo Ila nachojaribu ni kukuambia usijione kama maisha yako ni worthless

Bado kwa nafasi yako kuna watu unaoweza kujitolea kwao na ukawa ni baba na mkombozi kwao kiasi cha kukupenda na kukuthamini hadi ukajiona una maana kubwa duniani

Cha msingi ni kutengeneza system ya maisha itakayokupa furaha wewe mwenyewe na sio kusubiri kutimiza standards za jamii zetu ili ujihisi na wewe ni binadamu wa kawaida

Ulishawahi kujiuliza walemavu au watu walioodhoofu huwa wanaishi vipi wakati jamii inawachukulia tofauti. Wale matasa wanaishije na wengine hata neema ya pesa wamekosa. Wanawezaje ku_survive kwenye dunia katili namna hii

Jibu ni moja, wamejikubali na kuishi na wanaowakubali na mawazo ya wengineo yasiwaathiri. Sikuambii hakutakuwa na time utawaza lakini ukifanikisha kujikubali bhasi utaihisi furaha zaidi kuliko huzuni
 
Back
Top Bottom