Maisha ya bongo ni magumu mnoo vijana wa kiume wanapitia pagumu...Hasa bodax2

Wakuu kuna wakati mawahurumia sana vijana wetu, wanapitia hali tete sana.
Nililazimika kutoka saa 8.30 na kurudi saa 9.30.
Kila kijiwe cha boda boda nakuta vijana wamelala chali usingizi juu ya boda boda zao hata hawasikii hata mlio wa gari.

Mji umetulia hautii matumaini yoyote kwao angalau hata kuokota abiria hata mmoja.
Kijana huyu:
1. Huenda pkpk ni ya mkataba au
2. Anadaiwa rejesho na mmiliki
3. Huenda ana familia inasubiria apeleke chochote
4. Ana deni mahali

Ooh Mungu saidia vijana wetu hii hali sio kabisa...

Mama Abdul wakumbuke vijana wetu wenye elimu na hawana ajira
Ila boda boda hawa hawa wakiona sket wanachanganyikiwa ili hali wana wake majumbani
 
Na kuna bodaboda hadi leo anamilki boda zake tatu, moja anatumia na mbili amewapa watu wanamletea 10k kila mmoja.

Maisha hayajawahi kuwa rahisi hata kidogo, hiyo sekta unayoona kuna ugumu Sana wa maisha, kuna watu wanalaza 40k+ kwa siku, wanalea, wanasomesha na wanajenga.
Hili nalijua sana lkn inategemea uko wp
 
Wakuu kuna wakati mawahurumia sana vijana wetu, wanapitia hali tete sana.
Nililazimika kutoka saa 8.30 na kurudi saa 9.30.
Kila kijiwe cha boda boda nakuta vijana wamelala chali usingizi juu ya boda boda zao hata hawasikii hata mlio wa gari.

Mji umetulia hautii matumaini yoyote kwao angalau hata kuokota abiria hata mmoja.
Kijana huyu:
1. Huenda pkpk ni ya mkataba au
2. Anadaiwa rejesho na mmiliki
3. Huenda ana familia inasubiria apeleke chochote
4. Ana deni mahali

Ooh Mungu saidia vijana wetu hii hali sio kabisa...

Mama Abdul wakumbuke vijana wetu wenye elimu na hawana ajira

Mkuu maisha ni chain.

Hata wengine waliokuzidi wanaona na wewe unateseka while wewe unaona normal.

Huenda wewe una ki-Raum chako unaamka asubuhi saa 12 unaenda ofcn kwenye A/C lakini Mwingine Fogo anaamka saa nne LC 300 inamsubiri nje ,mtu huyo na yeye anakuonea huruma unateseka.

Huyo bodaboda na yeye akipita barabarani anaona jamaa mbavu wanachimba zege na sululu kuanzia asubuhi mpaka saa 12 jioni na yeye anaona wanateseka.

Kama unapata kipato kwenye shughuli yeyote siyo mateso.
 
Boda ni janga la taifa,wanalala kwasababu wamelewa chochote kwao halal,mirungi,bangi,gongo na wanawake wanaopakia wa nakopwa.
Sasa hapo unamuonea huruma ya nini wakati hata abiria ukipanda hizo boda anaweza kukuangusha popote akakuvunja miguu.
 
Wakuu kuna wakati mawahurumia sana vijana wetu, wanapitia hali tete sana.
Nililazimika kutoka saa 8.30 na kurudi saa 9.30.
Kila kijiwe cha boda boda nakuta vijana wamelala chali usingizi juu ya boda boda zao hata hawasikii hata mlio wa gari.

Mji umetulia hautii matumaini yoyote kwao angalau hata kuokota abiria hata mmoja.
Kijana huyu:
1. Huenda pkpk ni ya mkataba au
2. Anadaiwa rejesho na mmiliki
3. Huenda ana familia inasubiria apeleke chochote
4. Ana deni mahali

Ooh Mungu saidia vijana wetu hii hali sio kabisa...

Mama Abdul wakumbuke vijana wetu wenye elimu na hawana ajira
Na ndio hawahawa wanatucheka na kutukejeli wabeba boksi hatuna kitu tunaishi maidha magumu tunalala nje.
 
Back
Top Bottom