Glenn ,naona umetumia hisia kuliko uhalisia.
Sawa,ni vizuri kwanza kuwa na moyo wa kuwapazia sauti wenzako.
Ila,swali moja,ulilinganisha na vijana wa wapi uone wanavyohangaika na kuteseka?
Kuna nchi jirani kama mbili,waendesha pikipiki hao,ni wahitimu wa vyuo vikuu. Na pikipiki,za mkataba. Bora hao ni wanaume. Umewahi jiuliza wanawake aanapitia wakati gani?
Kosa kubwa la vijana,wanahitaji maendeleo ya hapo hapo. Na huwa wakikuta mambo ni tofauti na wanavofikilia,ndo yanakuwaga hivyo.
Fursa zilizopo ni nyingi sana. Tena sana.
Ningekuelewa au kukubaliana na wewe,ungesema serikali imewatelekeza.
1. Kwanza kabisa,kwenye ngazi za serikali,kuna watu wanajua machimbo hasa ya vyakula na vitu vingine,na wao hawapeleki chochote,na wana uwezo wa kufanya connection. Unajua mfano tikiti maji lina bei gani ulaya au uarabuni? Unajua parachichi kilo ni bei gani? Uliwahi kuuliza ndizi sukari?
Hivi vitu vipo tena kwa wingi nchini. Serikali ingewahimiza kilimo na kuwatafutia soko la uhakika,achana na sasa tikiti kubwa linachukuliwa kwa elfu 3 linaenda kuuzwa 15k,mkulima ana faida gani hapo?
Uliza watu wa Shinyanga. Nyanya wakulima wanawauzia Rwanda na DRC. Na hazitoshi. Je,wangekuwa wanapeleka wakulima wenyewe?
Mfano wa nyama. Unajua DRC nyama ina bei gani? Kwa vile huwezi safilisha mifugo hivi hivi,wakiweka standard za nyama,na magari ya reflegeration,hiyo pesa wataiweka wapi?
2. Vijana wenyewe,wanachagua kazi. Na ukiangalia waliokamaa na kilimo mfano,miaka 5,wamejenga,wanaweza kutatua shida zao,wana akiba,na pikipiki zao za kutembelea. Wamejenga wanaishi kwao na familia zao.
Sasa watu kama wewe,kuliko kulalamika,mngetafuta hata taasisi husika,msaidizane kuwapa semina na mitaji muone kama hawatoboi.