Mbona story zenu zimeegamia kwenye kutisha tu no hope kabisa unataka kusema sehemu za madini hakuna vitu vizuri vya kujivunia?
Hapa tunaelezea risk zilizopo kwenye machimbo ili kutoa mwanga kwa watu ambao hawajawahi kufanya shughuli kama hizo na wanataka kujaribu.
Unajua wengi wasiojua, wakisikia neno dhahabu wanajua ni kitu simple na kinapatikana kirahisi?
Upande mzuri kuhusu madini pia upo ila upande huo ili uweze kuona neema zake basi hakikisha unakuwa na mtaji mkubwa.
In short ni kwamba kwenda kuchimba dhahabu ukiwa huna hela kwa lengo upate hela ni worse idea.
Kwasababu utalazimika kufanya kazi katika mazingira magumu na ya hatari kwa guarantee ya kipato kidogo.
Ukiwa huna hela itakulazimu tu uchimbe machimbo yasiyohitaji mtaji, labda kuokota mawe au ukasambaze (kubinuka)
Ambapo huko kwenye mawe ili angalau upate pesa ya kueleweka itakubidi upate sehemu yenye mawe yenye dhahabu nyingi.
Mfano kule kuna kipimo cha makadirio kujua kiwango cha dhahabu kilichopo kwenye mawe.
Hicho kipimo kinakadiliwa kupitia idadi ya ujazo wa mawe kwenye kile kiroba cha jumla cha sabuni ya unga. Kule ujazo huo unafahamika kwa neno "dumu"
Sasa ili at least uonekane upo kwenye malengo basi walau kila dumu liwe na possibility ya kutoa point 2.
Ambapo point 1 sawa na 10,000 and this is high maximum approximation. Sio rahisi dhahabu ya kutoka karashani kuuzwa bei hiyo labda ichomwe na chemicals iwe pure.
Na mind you, the more you melting it to get it pure, the more weight decreasing.
So ni msala hakuna nafuu.
Sasa angalia hali ya sasa ilivyo pamoja na kwamba unaona pointi 2 ambayo value yake ni sawa na 20,000 (kwa makadirio ya juu) unaweza kuona kama sio kubwa hiyo pesa ukilinganisha na upatikanaji wake.
Lakini katika hiyo hela kumbuka kila dumu kuna percent utakuwa unakatwa kwa ajili ya kulipia huduma ya kusagiwa mawe kwa mwenye karasha.
Angalia sasa hali ilivyo, ni kwamba ni vigumu sana kupata eneo ambalo utapata mawe yenye sample ya point 2 kwa dumu moja.
Sehemu ambayo utakuta kuna mawe yenye sample yenye kutoa point zaidi ya 2 kupanda juu. Mara nyingi hiyo sio sehemu salama.
Mfano kuna kijiji kimoja kinaitwa "Shoga" huko ziliwahi kufunguka yani dumu moja lilikuwa linatoa hadi Gram kasoro lakini usalama wake ulikuwa mdogo.
Watu walikuwa ni wengi, na penye wengi kuna mengi, watu wako ladhi kukuua ili wakupore gema.
Ndugu yangu kama una ndoto ya kwenda kwenye madini jaribu kuangalia hizi changamoto na uzipime kama unaweza kuzimudu.
Ukiona unaziweza basi unaweza kwenda, ila usije ukaenda ukategemea kitu tofauti na hiki nilichokiandika kwa kudhani mambo ni simple.
Unaweza ukakutana na makubwa mengine ambayo hata hapa mimi sijayaandika.