Maisha ya mahabusu/ mfungwa ni magumu na mabaya ila siyo kwa ubaya ule unaovumishwa mitaani kwamba kule kuna
- Kupigwa na wababe
- Kunyang'anywa chakula
- Kuteswa
- Kubakwa n.k ni hapana
Maisha yanaenda kawaida ikiwa kwa upande wa burudani
- Television ipo
- Draft/bao lipo
- Mpira wa miguu upo
"Kwaya kwa waimbaji n.k
Vile vile watu wanapiga ibada kila siku jioni na asubuhi dini zote kuu mbili kwa muda wao. Na pia baadhi ya watu wanasali/swali haswa kwakuwa tegemeo lao lililobaki ni Mungu tu kuwatoa huko.
Changamoto kubwa ni kisaikolojia
- Kukosa uhuru
- Kutoona familia/marafiki
- Papuchi hakuna
- Msosi ni ugali mwaka tena ni mchana tu hakuna supper[emoji23]
- Asubuhi uji bila sugar mwaka
Ile hali ya kupangiwa kila kitu kula, kulala, kuamka, kazi ngumu, adhabu, kuhesabiwa inakera sana unaweza rukwa na akili. Maisha ya mahabusu/ ufungwani ili uishi kwa amani fuata taratibu na sheria zao bila shuruti. Ujuaji na ubishi utabondwa/ utataabika sana[emoji23][emoji23]
Jela ni kubaya, kugumu usijempeleka mtu kwa kumwonea/kumbambikia kesi ni laana. Pia kama kuna kesi yeyote ambayo unahisi itakupeleka jela jitahidi sana mmalizane uraiani usijepelekwa huko.
Mtu anaonesha ubabe mtaani na kusema "jela siogopi nimeshakaa kwani jela kitu gani??" Ujue huyo mjinga hajawahi pelekwa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
NB: Ni machache niliyojua kwa jela hii na kila jela kuna mambo yake
MWISHO
Kule ni nyumbani kwa wote wakati wowote, omba Mungu akuepushe na kule kuzimu ndogo.