Maisha ya ufungwani/ mahabusu ni machungu ndugu zanguni

Maisha ya ufungwani/ mahabusu ni machungu ndugu zanguni

Mkuu yule alisema kabisa sikuachii hii kesi yangu, nikikuacha hapa kituoni wengine nikikabidhi shift mtamalizana.
Chagua moja unipe changu nikuruhusu au niandike sammans we wa kufungwa tu ili tukose wote.
Namwambia sina hela hapa.
Anasema nyumbani je?nikazuga sina, huna mtu unamjua ukakope ndo ikawa twende.
Nikampa mambo yakaisha.
Ni njaa tu
Ndo maana narudia ulitishiwa, polisi hana uwezo wa kukufunga kwa kutengeneza kesi.
Wanaweza endapo serikali itaamua
 
Siku hapo msimbazi center ilala nakunja kona wale jamaa wa boda na mabunduki yao hawa hapa wanapiga mkono, paki pembeni vp kunani?
"We umetuchomekea siku ya usalamabarabarani, "
hata sijui mi nimekunja kona yangu niendelee na safari.
Hapo nimepaki africenter ikabidi niwashtue "e bwana mi nna kiu tupate japo moja moja huku tukiongea.
Wakavua magwanda zama bar.
Mule kuelewana nikawapa walichotaka, tunatoka wamevaa migwanda yao wako "si tutazuga gari yako ilikua mbovu tunacheck usalama 🤣🤣🤣e bana fungua bonet,check oil nawakasukuma ile gari🤣,
gari chaser ilikua one kick drive automatic haina ubovu wowote service nimefanya full siku 5 tu zimepita
Mind you hapo nimepigwa buku 40 tayari bila kosa,
Sukuma kidogo nikawasha imewaka eeh?
Mimi yaah asante sana maafande.😂😂😂
Bongo nyoso sana full comedy
Huyo Naondoka tunapungiana mkono km hakuna lililotokea.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Mungu ibariki Tanzania 🙏
Mkuu umenichekesha,mkanza kuigiza na hela umetoa nikuwa mpole tu..
 
Jela ni kubaya, kugumu usijempeleka mtu kwa kumwonea/kumbambikia kesi ni laana. Pia kama kuna kesi yeyote ambayo unahisi itakupeleka jela jitahidi sana mmalizane uraiani usijepelekwa huko.
Angalau namfahamu mtu wa karibu na mimi ambaye amekuwa akifanya huu upumbavu kwa mtoto wake wa kumzaa mwenyewe; kwa motive ambayo inaonekana kuwa ni mali. Lengo ni kumtoa kafara mtoto ili aweze kupata mali. Unajua dizaini ya watu ambao mwili ni sawa na kopo tu ambalo huwa linabaki tupu baada ya kutolewa bidhaa liliyokuwa limehifadhi
 
We hujaotewa ,
mume wa Kajala mpk leo sijui kaishia wapi, na yule wa Wema?
Mramba aliyesema tule majani ndege inunuliwe jiwe kacheza nae kadance kule mpk kakubali kufagia muhimbili.
Kuna yule mwamba wa kaskazini TRA Enzi zake humgusi sijui wamemalizana nae au vp.
Ameongea bila kutafakari.
Kuna kesi zinazotokana na mazingira mengi.
1. Kesi inayotokea katika mazingira ya maeneo yako ya kujidai. Ndani ya wilaya yako. Unakuta unajuana na mahakimu,OCD na hata PRC pia. Hapo utasema jela ni kwa maskini na wasio na connection.
2. Kuna kesi inatokea nje ya maeneo yako ya kujidai. Pamoja na pesa zako na umaarufu wako lakini lazima itakusumbua mpaka ukae sawa.
3. Kuna kesi zinatokea/zimeshikiliwa na wakubwa. Aisee kesi ya namna hii njoo na pesa zako,umaarufu wako wote unaojua wewe lazima utachezea jela tu.
Kesi ifike kwa Rais,M/Rais au Waziri Mkuu. Fanya unuavyo lazima upoteane aisee.
Mfano kesi ya wale polisi walioua then ikatua kwa W/Mkuu na Rais mwenyewe,Yusuph Manji na wengine wengi.
 
Back
Top Bottom