Maisha ya ufungwani/ mahabusu ni machungu ndugu zanguni

Maisha ya ufungwani/ mahabusu ni machungu ndugu zanguni

Kuna jela za kiroho, hizo hutesa zaidi kuliko jela za serikali
Hizo Ni Ngum balaa na nzito sana(narudia tena nzito sana) na ndio zinawapeleka wengi jela Za KIMWILI ANAZOZIZUNGUMZIA HUYU.

ULIMWENGU WA ROHO NDIO UNAOENDESHA ULIMWENGU WA MWILI HAMNAGA BAHATI MBAYA.

Unakuta Mtu Yupo Kwenye kifungo cha Magonjwa Yani Mpaka Anakufa yupo hospital Au nyumbani.

Mwengine Kifungo Cha Ukichaa Yani Ni Balaa Tupu mtu mpaka Anakufa ni kichaa tu.

Yesu Atusaidie Aise USIOMBE Uangukie Jela Za Kipepo

Sent from my A37fw using JamiiForums mobile app
 
Kwa kweli tuombe tu tusiingie sehemu hiyo. Siyo nzuri kabisa kabisa, hakunaga mjanja kule.l
 
Kuna jera za kiroho hizo ndio unaweza kuwa chizi mana alie Kufunga humuoni na hujui utatoka lini na kama Ndio Sio Muombaji Ndio Imeisha Hiyo Utamaliza Waganga.

KUTOKA JELA HII YA KIROHO NI RAHISI UKIMUOMBA YESU NA USIOMBE KWA KUBIP HAMNAGA JAMBO JEPESI NDUGU.

Sent from my A37fw using JamiiForums mobile app
Utoaji wa zaka, sadaka na sala ya toba kwa dhati vyaweza kukurahisishia njia ikawa nyepesi kufunguliwa ingawa kwa Mungu hakuna tambarare.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Hizo Ni Ngum balaa na nzito sana(narudia tena nzito sana) na ndio zinawapeleka wengi jela Za KIMWILI ANAZOZIZUNGUMZIA HUYU.

ULIMWENGU WA ROHO NDIO UNAOENDESHA ULIMWENGU WA MWILI HAMNAGA BAHATI MBAYA.

Unakuta Mtu Yupo Kwenye kifungo cha Magonjwa Yani Mpaka Anakufa yupo hospital Au nyumbani.

Mwengine Kifungo Cha Ukichaa Yani Ni Balaa Tupu mtu mpaka Anakufa ni kichaa tu.

Yesu Atusaidie Aise USIOMBE Uangukie Jela Za Kipepo

Sent from my A37fw using JamiiForums mobile app
AMINA

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Utoaji wa zaka, sadaka na sala ya toba kwa dhati vyaweza kukurahisishia njia ikawa nyepesi kufunguliwa ingawa kwa Mungu hakuna tambarare.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Upo Sahihi Kaka Yesu Atusaidie Aise Maana Jela Za Kipepo Hazina Chakula Yani Unakauka Mzima mzima ndio mana Wengi wanao Pitia Hizi mahabusu unakuta mtu anakonda tu maradhi wengine hayaishi Yani mtu ndio Anakufa mdogo mdogo na Kama Sio wa Maombi Ndio Imeisha Hiyo

Maombi,Zaka,Sadaka Vinanguvu Sana Katika Hizi mAhabusu ambazo zinatisha na hazina huruma USIOMBE UANGUKIE KWENYE JELA ZA KIROHO UNAWEZA KUTA UNAPIGA NGUMI UPEPO KAMA UPO KIMWILI NA KUANZA KUONGEA PEKE YAKO.

Unakuta Mtu Kawekwa Kwenye Mahabusu Ya Kupenda Wanawake Yani Mpaka Anapata Ukimwi Na Haachi Mpaka Mnasikia Amekufa.
 
Umenikumbusha, kuna jamaa kazini kwetu alikuwa mjuaji sana mixer mbabe. Siku isiyo na jina kajaa kwenye mikono michafu na bonge LA kesi aisee,,,jamaa alikaa Siku 21 tu ila alivyorudi anakwambia "ukiskia mtu anamwambia mwenzake kwamba nitakuua nikafungwe, nenda pembeni muombee sana hajui anachokitamka"
 
1.Milo Ni miwili uji asubuhi na Chakula ni saa 10 jioni hicho ndo chakula Cha mchana na usiku

2.Ukiitwa na afande unaenda unakimbia ukimkaribia hatua 5 unachuchumaa chini huruhusiwi kusimama afande akiwa anaongea, na ukipewa maelekezo hutakiwi kuitika kwa kusema sawa au nimekuelewa unatakiwa kuitika kwa kusema Ndiyo bwana mkubwa.

3.Ukiitwa jina ni marufuku kuitika naam au abee, mfano unaitwa Mussa Issa utaitwa kwa jina moja Mussaaa na unatakiwa uitikie Issaaa ukiitika naam au abee utachezea bonge la banzi.

4.Ukifanya kosa lolote la utovu wa nidhamu ili uonekane kuwa wewe ndo mwamba ukigundulika unapigwa pingu miguu na mikono mbele ya wafungwa wenzako unaning'inizwa sehem unachezea kichapo ambacho wafungwa wenzako wakiona hawatajaribu kuvunja sheria ya jela kwa muda wa miezi 6 wataendelea kukumbuka kichapo walicho kiona kwako

Kuhusu kubakwa jela huo ni uongo labda uende na tabia zako za kishoga na uamue kuliwa kwa ridhaa yako kwasbabu ya ushoga wako, ila ukigundulika unafanya vitendo vya ushoga utachezea kichapo kitakatifu Hadi utatangaza kuokoka
 
Zamani niliendaga police kuchukua loss report kabla hizi za kidijitali hazijaja,
Mahabusu wamejazana humo zaidi ya kumi kwenye hicho kichumba nawaona,
Kikaletwa chakula cha flani, flani anaitwa na askari haitiki, hadi mahabusu wakawa wanaita jamani flani, kimya,
Mmoja alikuwa mbele muda wote akasema ni mimi hapa nakiomba,
Askari akasema sio wewe,
Mahabusu wengine wakawa wanacheka,
Mara wataniane na askari,
Inshort tangia nimeingia pale hadi natoka kulikuwa na vibe flani hivi you'd think they're having a good time in there 😅😅
 
Maisha ya mahabusu/ mfungwa ni magumu na mabaya ila siyo kwa ubaya ule unaovumishwa mitaani kwamba kule kuna
  • Kupigwa na wababe
  • Kunyang'anywa chakula
  • Kuteswa
  • Kubakwa n.k ni hapana
Maisha yanaenda kawaida ikiwa kwa upande wa burudani
  • Television ipo
  • Draft/bao lipo
  • Mpira wa miguu upo
"Kwaya kwa waimbaji n.k

Vile vile watu wanapiga ibada kila siku jioni na asubuhi dini zote kuu mbili kwa muda wao. Na pia baadhi ya watu wanasali/swali haswa kwakuwa tegemeo lao lililobaki ni Mungu tu kuwatoa huko.

Changamoto kubwa ni kisaikolojia
  • Kukosa uhuru
  • Kutoona familia/marafiki
  • Papuchi hakuna
  • Msosi ni ugali mwaka tena ni mchana tu hakuna supper[emoji23]
  • Asubuhi uji bila sugar mwaka
Ile hali ya kupangiwa kila kitu kula, kulala, kuamka, kazi ngumu, adhabu, kuhesabiwa inakera sana unaweza rukwa na akili. Maisha ya mahabusu/ ufungwani ili uishi kwa amani fuata taratibu na sheria zao bila shuruti. Ujuaji na ubishi utabondwa/ utataabika sana[emoji23][emoji23]

Jela ni kubaya, kugumu usijempeleka mtu kwa kumwonea/kumbambikia kesi ni laana. Pia kama kuna kesi yeyote ambayo unahisi itakupeleka jela jitahidi sana mmalizane uraiani usijepelekwa huko.

Mtu anaonesha ubabe mtaani na kusema "jela siogopi nimeshakaa kwani jela kitu gani??" Ujue huyo mjinga hajawahi pelekwa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

NB: Ni machache niliyojua kwa jela hii na kila jela kuna mambo yake

MWISHO
Kule ni nyumbani kwa wote wakati wowote, omba Mungu akuepushe na kule kuzimu ndogo.
Kuna brother mmoja mtaan kwetu alikua mbishi, mgumu na anaogopwa sana mtaan, aliwahi kumchoma kisu mtu mchana kweupe na hakuna aliyetoa msaada.

Yule akikwambia takukata panga hatanii anakukata kweli. Sasa alikamatwa akakaa butimba miaka 2 akaja kutoka.

Maisha yakaendelea baadae akapata msala mwingine akakaa butimba kama mwaka akatoka.

Sasa badae alikuja kuwa msela wangu sana yule bro, alikua ananikubali sana ananiita dogo janja. Nilikua naenda nae sehem tofaut kwa wahuni watu wamepinda ila wanamuheshimu.

Nimemuelezea hivo kuona ni mtu wa aina gn, kiufupi ni mbishi sana... sasa siku moja ulitokea ugomvi mkubwa pale kitaa huyu brother akawa anajiepusha kugombana akawa anaamua anasema mambo ya kupelekana jela saiv siyataki acheni hizi mambo.

Kuna siku moja nikawa namuliza kuhusu jela akawa ananiambia mdogo wangu kule apafai ni pàbaya akaniambia mambo mengi yalipo huko. Sasa nikamuliza mbona ww mgumu alafu unakuwa kama unapaogopa akasema kule hakuna mgumu utanyooshwa na utanyooka.

Kuanzia hapo najiepusha sana na mambo yanayoweza kunipeleka huko japo inawezekana kuingia huko.
 
Dem mmoja angesababisha niendege huko, ndo maana nayaogopa mahusiano.... Makosa ya mwanamke, Mtu unajizuia hasira hadi point ya mwisho alafu Mwanamke unamtuliza asiongee shombo kwa kumzaba kibao, unazani yameisha unashtukia kakubamiza na fimbo la kichwa limekuvunjikia alafu kwa bahati mbaya unamtia mikononi.... Asee acha mahusiano yakae na wenyewe bana.
 
Ukiisoma hii post imekaa kimasihara, ila naamini imegusa wengi na kujitafakali upya mienendo yao uraiani.
 
Back
Top Bottom