Maisha ya ufungwani/ mahabusu ni machungu ndugu zanguni

Maisha ya ufungwani/ mahabusu ni machungu ndugu zanguni

Nakumbuka nilingia mahabusu ijumaa..siku ambayo mahakama inafanya KAZI mwisho saa9..barua za waeka dhamana Wang wawil zote zilikua zimekosewa kdgo..Hakim akasema zikarekebishwe..MDA huo ni saa nane..mpk warud wakakuta nshapelekwa mahabusu teari..nakumbuka siku iyo watuhumiwa wote tulikua wapya Yani tunaingizwa mahabusu mara ya kwanzA baada ya kukosa mdhamana..Yule askar magereza alietupokea siku iyo alikua kalewa kshnz
Anatukana ovyo asa mtuhumiwa mmoja akaulizwa unaitwa nan..akusikia vzur askar bila kupotza MDA alimtoa wenge wa mambata mpk wafungwa na mahabusu wote waligeuka kuangalia nn kimetokea mana lile mbata lilikua kama bomu😁😁..
Kingine kilichoniboa ni Ile biashara ya kuvuliwa nguo zote unabak uchi mnakaguliwa msiingie na vitu vya kuzuru wengne..kingine ni kupimwa Ngoma taka usitake kama unayo unaanzishiwa doz apoapo
Maliwaton Hamna faragha unakata Gogo uku mnaona..nashukuru nlitoka j3 kuanzia siku iyo niliaapa kuwa mtiifu mtaan nisije rud tena mule..kesi yangu ulikua ni Traffic case..
 
Dem mmoja angesababisha niendege huko, ndo maana nayaogopa mahusiano.... Makosa ya mwanamke, Mtu unajizuia hasira hadi point ya mwisho alafu Mwanamke unamtuliza asiongee shombo kwa kumzaba kibao, unazani yameisha unashtukia kakubamiza na fimbo la kichwa limekuvunjikia alafu kwa bahati mbaya unamtia mikononi.... Asee acha mahusiano yakae na wenyewe bana.
Kwamba Demu mmoja tu apelekee kukufanya uungane na kikundi cha wahuni wa "kataa ndoa (Waoga wa maisha, Wavulana, Mashoga)"?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Maisha ya mahabusu/ mfungwa ni magumu na mabaya ila siyo kwa ubaya ule unaovumishwa mitaani kwamba kule kuna
  • Kupigwa na wababe
  • Kunyang'anywa chakula
  • Kuteswa
  • Kubakwa n.k ni hapana
Maisha yanaenda kawaida ikiwa kwa upande wa burudani
  • Television ipo
  • Draft/bao lipo
  • Mpira wa miguu upo
"Kwaya kwa waimbaji n.k

Vile vile watu wanapiga ibada kila siku jioni na asubuhi dini zote kuu mbili kwa muda wao. Na pia baadhi ya watu wanasali/swali haswa kwakuwa tegemeo lao lililobaki ni Mungu tu kuwatoa huko.

Changamoto kubwa ni kisaikolojia
  • Kukosa uhuru
  • Kutoona familia/marafiki
  • Papuchi hakuna
  • Msosi ni ugali mwaka tena ni mchana tu hakuna supper😂
  • Asubuhi uji bila sugar mwaka
Ile hali ya kupangiwa kila kitu kula, kulala, kuamka, kazi ngumu, adhabu, kuhesabiwa inakera sana unaweza rukwa na akili. Maisha ya mahabusu/ ufungwani ili uishi kwa amani fuata taratibu na sheria zao bila shuruti. Ujuaji na ubishi utabondwa/ utataabika sana😂😂

Jela ni kubaya, kugumu usijempeleka mtu kwa kumwonea/kumbambikia kesi ni laana. Pia kama kuna kesi yeyote ambayo unahisi itakupeleka jela jitahidi sana mmalizane uraiani usijepelekwa huko.

Mtu anaonesha ubabe mtaani na kusema "jela siogopi nimeshakaa kwani jela kitu gani??" Ujue huyo mjinga hajawahi pelekwa 😂😂😂😂😂

NB: Ni machache niliyojua kwa jela hii na kila jela kuna mambo yake

MWISHO
Kule ni nyumbani kwa wote wakati wowote, omba Mungu akuepushe na kule kuzimu ndogo.

Siyo kuwa kuelekea katiba mpya tutasikia mengi.

Tukiogopa jela au mahabusu ieleweke katiba mpya haipo karibuni.
 
Siyo kuwa kuelekea katiba mpya tutasikia mengi.

Tukiogopa jela au mahabusu ieleweke katiba mpya haipo karibuni.
Ww kama unaona huko ni pazuri nenda kila mtu na maisha yake, katiba mpya inahusiana nn na kwenda jela?
 
Upo Sahihi Kaka Yesu Atusaidie Aise Maana Jela Za Kipepo Hazina Chakula Yani Unakauka Mzima mzima ndio mana Wengi wanao Pitia Hizi mahabusu unakuta mtu anakonda tu maradhi wengine hayaishi Yani mtu ndio Anakufa mdogo mdogo na Kama Sio wa Maombi Ndio Imeisha Hiyo

Maombi,Zaka,Sadaka Vinanguvu Sana Katika Hizi mAhabusu ambazo zinatisha na hazina huruma USIOMBE UANGUKIE KWENYE JELA ZA KIROHO UNAWEZA KUTA UNAPIGA NGUMI UPEPO KAMA UPO KIMWILI NA KUANZA KUONGEA PEKE YAKO.

Unakuta Mtu Kawekwa Kwenye Mahabusu Ya Kupenda Wanawake Yani Mpaka Anapata Ukimwi Na Haachi Mpaka Mnasikia Amekufa.
Natamani siku Mtu akipata muda aje atolee ufafanuzi kuhusu Jela ya Kiroho maana mziki wake si wa kitoto wawezakuta ni mara 10 ya Jela ya Kimwili.

Mungu atusaidie tuwe wenye hekima siku zote za maisha yetu hapa duniani...[emoji120]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Ww kama unaona huko ni pazuri nenda kila mtu na maisha yake, katiba mpya inahusiana nn na kwenda jela?
Usichojua ni kuwa katiba mpya haitapatikana bila kupiganiwa. Kuipigania lazima mahabusu na jela zitahusika.

Kwenye mchakato huo mada kama hizi za kutisha watu tunazitegemea sana. Ila ukweli mchungu mtadanganyana wenyewe.
 
Nilisikia ushuhuda wa jambazi sugu mstaafu anasema.
Jela ni roho, na jela Ina wenyewe, kama kwenye familia yenu hapajawahi mtu kuingia jela ni ngumu kuingia na kama alishawahi possibility ni kubwa kwa members yeyeto wa familia YAKO kuingia.
Aisee hii kweli mshua aliwekwaga ndani ...nilopowekwa na mm siku bamdogo alipokuja kunicheki akanambia hata mshua ashakaa mwaka ndani hivyo nisiwaze
 
Mi nataka kuolewa mwaka huu,Mimi nina mtoto ...je niolewe na mwenye mtoto pia au asiye nae....embu nishauri...usijali kuhusu kuwapata maana mie huwa natongoza ivo nitapata tu
Uache kwanza kupiga, olewa na yeyote kikubwa ni upendo.
 
Back
Top Bottom