Maisha ya ufungwani/ mahabusu ni machungu ndugu zanguni

Ndo maana narudia ulitishiwa, polisi hana uwezo wa kukufunga kwa kutengeneza kesi.
Wanaweza endapo serikali itaamua
 
Mkuu umenichekesha,mkanza kuigiza na hela umetoa nikuwa mpole tu..
 
Jela ni kubaya, kugumu usijempeleka mtu kwa kumwonea/kumbambikia kesi ni laana. Pia kama kuna kesi yeyote ambayo unahisi itakupeleka jela jitahidi sana mmalizane uraiani usijepelekwa huko.
Angalau namfahamu mtu wa karibu na mimi ambaye amekuwa akifanya huu upumbavu kwa mtoto wake wa kumzaa mwenyewe; kwa motive ambayo inaonekana kuwa ni mali. Lengo ni kumtoa kafara mtoto ili aweze kupata mali. Unajua dizaini ya watu ambao mwili ni sawa na kopo tu ambalo huwa linabaki tupu baada ya kutolewa bidhaa liliyokuwa limehifadhi
 
Ameongea bila kutafakari.
Kuna kesi zinazotokana na mazingira mengi.
1. Kesi inayotokea katika mazingira ya maeneo yako ya kujidai. Ndani ya wilaya yako. Unakuta unajuana na mahakimu,OCD na hata PRC pia. Hapo utasema jela ni kwa maskini na wasio na connection.
2. Kuna kesi inatokea nje ya maeneo yako ya kujidai. Pamoja na pesa zako na umaarufu wako lakini lazima itakusumbua mpaka ukae sawa.
3. Kuna kesi zinatokea/zimeshikiliwa na wakubwa. Aisee kesi ya namna hii njoo na pesa zako,umaarufu wako wote unaojua wewe lazima utachezea jela tu.
Kesi ifike kwa Rais,M/Rais au Waziri Mkuu. Fanya unuavyo lazima upoteane aisee.
Mfano kesi ya wale polisi walioua then ikatua kwa W/Mkuu na Rais mwenyewe,Yusuph Manji na wengine wengi.
 
Kule ndani ya selo unakunywa maji kwa kuchuchumaa na kukojoa pia kwa kuchuchumaa!!! πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…