Maisha yanaenda kasi sana, inakuaje vijana wa sasa wanakubali kulelewa kama watoto wa kike

Hii nimeishuhudia leo Mlimani city katika mgahawa mmoja maarufu wa chakula, yaani kijana na nguvu zake inakuaje anakubali kununuliwa chakula na mwanamke ili hali angeweza kutumia nguvu na akili zake katika kutafuta pesa.

Na katika uchunguzi nimegundua yule mama atakuwa amemzidi kijana wa watu miaka si chini ya 20.

Sisi kama taifa tunaelekea wapi katika malezi, huyu kijana niliye mshuhudia leo alikuwa amejazia kifua, kachora tatoo kila mahali kavaa nguo zimebana miguu kama skin tight za wadada, au ndio ule msemo unaosema kila mtu hula kwa urefu wa kamba yake.

Vijana wa sasa mnatuabisha wazee wa zamani, nikiweka kumbukumbu sawa kwa miaka yetu hali haikuwa hivi, mambo yalikuwa tofouti sana vijana wa sasa wanatumia muda mwingi katika kioo (kujipodoa) na gym (kutengeneza mwili) badala ya kutumia muda huo kutafuta pesa.

Vijana wa sasa mnatuangusha sana sisi wazee, mbadilike.
Mambo ya Ngoswe, muachie Ngoswe mwenyewe.

Hayo yanakuhusu nini wewe?

Ukitaka kufuatilia ya watu yasiyokuhusu, hutayamaliza.
 
Nyie wazee wakuda sana tukija makazini tukiomba hata kazi za kujitolea hamtaki, halafu nyie wazee wa zama zenu za 50,60 na 70 ni wazinguaji mnataka kila kitu mfanye na mitaji hamtaki kutoa, ila mnahonga mabinti kibao na mnafia guest kila kukicha.

kwa kifupi hatuna pa kuenda madawa ya kulevya hakuna, bangi zimekuwa ngumu kwa kuuza na kuvuta, bado makazini hamtaki tujitolee mnajiweka busy ukitoka ofisini ndani ya gari tunawaonea wapi?

Bungeni kazi yenu kupiga makofi na kupelekea watoto hizo posho ila mambo kama haya ya vijana kutembea na wamama mnayaona yanatokea ni kwa sababu ya uzembe wenu sisi tumekua hatujui lolote.

ilitakiwa muandae mazingira, watu wajiajili kwenye michezo, biashara, ufugaji,makampuni,serikalini , ulimaji tusingejaa mijini ila kazi yenu ni kusema tuu hivi hivi hlf hakuna jithada mnafanya vijana tujikomboe vipi?,.

Nakereka sana ' et hamkua hivyo huoni kama baba zenu walijua mkikua mtafanya nini ? sisi kizazi chetu huwezi kufanya biashara pesa yote inaishia kulipa kodi serikalini na kwa wenye majumba bado hamtaki hata tuwe barabarani sijui tukauzie maporini.

hivi hamjiulizi kwa nini wanafunzi wa vyuo walianza kupewa mikopo ili kuepusha nini?

Nyie wazee mmetupoteza kabisa tupo kwenye shimo ambalo hatukutakiwa kuingia sisi.

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, shetani ndiye kiranja wa Dunia sasa. Ni kupitia Wanawake ndipo agenda zake hutekelezeka.
Na moja ya agenda hiyo ni Haki sawa.
Dunia ilipo na inapokwenda, mwanaume anaenda kubaki jina tu ila majukum yake na uwezo wake unakwenda chukuliwa na Mwanamke.
 
Nyie wazee wakuda sana tukija makazini tukiomba hata kazi za kujitolea hamtaki, halafu nyie wazee wa zama zenu za 50,60 na 70 ni wazinguaji mnataka kila kitu mfanye na mitaji hamtaki kutoa, ila mnahonga mabinti kibao na mnafia guest kila kukicha.

kwa kifupi hatuna pa kuenda madawa ya kulevya hakuna, bangi zimekuwa ngumu kwa kuuza na kuvuta, bado makazini hamtaki tujitolee mnajiweka busy ukitoka ofisini ndani ya gari tunawaonea wapi?

Bungeni kazi yenu kupiga makofi na kupelekea watoto hizo posho ila mambo kama haya ya vijana kutembea na wamama mnayaona yanatokea ni kwa sababu ya uzembe wenu sisi tumekua hatujui lolote.

ilitakiwa muandae mazingira, watu wajiajili kwenye michezo, biashara, ufugaji,makampuni,serikalini , ulimaji tusingejaa mijini ila kazi yenu ni kusema tuu hivi hivi hlf hakuna jithada mnafanya vijana tujikomboe vipi?,.

Nakereka sana ' et hamkua hivyo huoni kama baba zenu walijua mkikua mtafanya nini ? sisi kizazi chetu huwezi kufanya biashara pesa yote inaishia kulipa kodi serikalini na kwa wenye majumba bado hamtaki hata tuwe barabarani sijui tukauzie maporini.

hivi hamjiulizi kwa nini wanafunzi wa vyuo walianza kupewa mikopo ili kuepusha nini?

Nyie wazee mmetupoteza kabisa tupo kwenye shimo ambalo hatukutakiwa kuingia sisi.

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
kidume unapambana utoke unasikia tamko linalogusa issue yako, unaingia jamii forum unakutana na masimango eti vijana wavivu wanakera hawajui tu.
 
Fata mambo yako mzee usitake kila mtu afanye unavyofanya wewe. Bobrisky huko kajibadilisha kutoka kuwa mwanaume awe mwanamke kwasababu ameona wanawake wana fursa zaidi ya kupiga hela kuliko wanaume.
 
Nyie wazee wakuda sana tukija makazini tukiomba hata kazi za kujitolea hamtaki, halafu nyie wazee wa zama zenu za 50,60 na 70 ni wazinguaji mnataka kila kitu mfanye na mitaji hamtaki kutoa, ila mnahonga mabinti kibao na mnafia guest kila kukicha.

kwa kifupi hatuna pa kuenda madawa ya kulevya hakuna, bangi zimekuwa ngumu kwa kuuza na kuvuta, bado makazini hamtaki tujitolee mnajiweka busy ukitoka ofisini ndani ya gari tunawaonea wapi?

Bungeni kazi yenu kupiga makofi na kupelekea watoto hizo posho ila mambo kama haya ya vijana kutembea na wamama mnayaona yanatokea ni kwa sababu ya uzembe wenu sisi tumekua hatujui lolote.

ilitakiwa muandae mazingira, watu wajiajili kwenye michezo, biashara, ufugaji,makampuni,serikalini , ulimaji tusingejaa mijini ila kazi yenu ni kusema tuu hivi hivi hlf hakuna jithada mnafanya vijana tujikomboe vipi?,.

Nakereka sana ' et hamkua hivyo huoni kama baba zenu walijua mkikua mtafanya nini ? sisi kizazi chetu huwezi kufanya biashara pesa yote inaishia kulipa kodi serikalini na kwa wenye majumba bado hamtaki hata tuwe barabarani sijui tukauzie maporini.

hivi hamjiulizi kwa nini wanafunzi wa vyuo walianza kupewa mikopo ili kuepusha nini?

Nyie wazee mmetupoteza kabisa tupo kwenye shimo ambalo hatukutakiwa kuingia sisi.

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
Daa comment bora kabisa, umepiga kwenye mshono kabisa yani kila kitu cha moto sahivi.
 
Ukifanya kazi ngumu unazeeka mapema na kwa kuchakaa kwa mwili wako mademu watasema hawataki wanuka jasho

Usimlaumu jamaa huenda machale yalimcheza mapema
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Msenge wewe nitakuoa uwe unacheza na paka wangu 😅😅
Ungekuwa mzee ungekuwa na busara ya kuelewa kuwa unayetaka kumuoa anaweza kuwa kijana wako in fake id.
 
Kwa kipindi hiki n kawaida kumkuta binti mzuri kabisa anatembeza uji,matunda au mboga mboga na kijana mwenye nguvu zake kabisa hawezi hata kufanya baadhi kazi kwa kujitoa angali elimu Hana kwa kuhofia kushushwa cheo.,anaona Bora ashinde kituo Cha bajaji&boda kusubiri deiwaka na akikosa ndo basi siku imepita atashindwa kuchangamkia ZALI kama hilo MKUU!!😁😁..miaka inavyozidi kwenda pesa naona inahamia kwa wanawake maana nowdays wamekua wapambanaji kutuzidi na wengi wao pesa yao inafanyiwa mambo muhimu(FUTURE PLANS)
nasikia wengi wa wauza uji wanauza na mambo mambo Mkuu, ila wauza uji wengi wana lile jambo pendwa sijui ndio kivutio cha biashara yao, 'Ai donti no'
 
Hii nimeishuhudia leo Mlimani city katika mgahawa mmoja maarufu wa chakula, yaani kijana na nguvu zake inakuaje anakubali kununuliwa chakula na mwanamke ili hali angeweza kutumia nguvu na akili zake katika kutafuta pesa.

Na katika uchunguzi nimegundua yule mama atakuwa amemzidi kijana wa watu miaka si chini ya 20.

Sisi kama taifa tunaelekea wapi katika malezi, huyu kijana niliye mshuhudia leo alikuwa amejazia kifua, kachora tatoo kila mahali kavaa nguo zimebana miguu kama skin tight za wadada, au ndio ule msemo unaosema kila mtu hula kwa urefu wa kamba yake.

Vijana wa sasa mnatuabisha wazee wa zamani, nikiweka kumbukumbu sawa kwa miaka yetu hali haikuwa hivi, mambo yalikuwa tofouti sana vijana wa sasa wanatumia muda mwingi katika kioo (kujipodoa) na gym (kutengeneza mwili) badala ya kutumia muda huo kutafuta pesa.

Vijana wa sasa mnatuangusha sana sisi wazee, mbadilike.
sasa ulijuaje kama anatumia hela za huyo mama kama mtu wake? kama ni mama, shangazi au dada ake utajuaje? nauliza tu
 
Wazee wa zamani mnajikuta mlikua perfect sana wakati nyie ndo mlikua mnawakata viharage bibi zetu.
 
Back
Top Bottom