Maisha yetu ni mafupi sana

amn mzee pia tumuombe mungu atupe mwisho mwema
 
Huenda kweli,eti?
 
Dah mkuu leo niliamka nikaanza kutafiti kama Tukifa consciousness nayo inakufa ...sijapata majibu ..

Nimeamua kutupilia mbali ... Ni mambo ya kuogofya ...

Mimi nashawishika kuikumbatia hii hoja ya kwamba tukifa kila kitu kinaishia hapo. Hii japokua nayo inatisha lakini kwavile ukishakufa hautajua chochote, basi kunakua na afadhali.

Hii naiona ina mantiki kuliko ile hoja ya kwamba ukifa kuna kinachoendelea hasahasa ikikazia swala la adhabu kali hata kwa tumakosa tudogo tudogo hutu twa kibinadamu..
 
Hakuna,waliandika hayo Ili kupunguza makali ya dhambi la sivyo tungekuwa tumechinjana wote
 
Ni Africa na Nchi zingine maskini.Ulaya uhakikika wa kufika 70 yrs na kiendelea probability ni kuwa.

Ila sisi nadhani maisha yetu ni mafupi zaidi ya jamii zingine duniani.

Just imagine mtu mpaka unagonga 25 bado hata shule hujamaliza! Uje umalize, uanze kutafuta cha kufanya 30 hii hapa. Uanze sasa kujipanga mara kujenga sijui familia sijui nini 40 imeshabisha hodi! Hapo kama Mungu kakubariki ndio unaanza kuishi ishi angalau kidogo japo majukumu nayo watoto kusomesha, wazazi wameshazeeka, extended family, magonjwa nyemelezi, nk wakati huo ukichungulia life expectancy inasoma 50! Dah.. sasa apo mtu unaishi saa ngapi?
 
Maisha ni kuanzia ulipozaliwa wangu
 
Huenda kweli,eti?
Tunasema kifo ni kibaya sababu tumepakubali hapa duniani tulipo na hatujui uhalisia wa huko tunapokwenda.

Katika maisha hujawahi shawishiwa kwenda sehemu huku ww unataka kubaki halafu ukalazimishwa kwenda ila ulipofika ukafurahia kweli uwepo wako hapo ulipokuwa hupataki?
 
Yalikua yanatia naniliu saana
 
Kwangu minni vice versa,maisha ni adhabu na kufa ni zawadi,sijawahi kuona umuhimu wa kuishi kuna wakati nasema bora nisingezaliwa,sioni kipya duniani
Umenena vizuri sana. Niboreshe kidogo kwa kusema maisha yawe kumpendeza Mungu kwanza (si watu), ili kifo kiwe faida (zawadi kama ulivyosema) kwa kuurithi Ufalme wa Mungu pindi roho imtokapo mtu. Wakristo tunasema "kuishi ni Kristo, na kufa ni faida."
 
Kwani zamani kulikuwa na kujipangia umri wa kuishi?
 
Pole sana, tena sana!
 

Ukiwa hai acha legacy yako iishi, acha uzazi utaoendeleza kizazi chako/chenu...

Vinginevyo hakuna namna nyingine ya kukwepa huo wasiwasi wako...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…