DOKEZO Maji ya kuoshea maiti yanayo lalamikiwa kutumika kuhifadhia samaki yanauzwa kwenye maduka ya dawa za asili, Serikali imulike huko

DOKEZO Maji ya kuoshea maiti yanayo lalamikiwa kutumika kuhifadhia samaki yanauzwa kwenye maduka ya dawa za asili, Serikali imulike huko

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ziwa lenyewe limeshakuwa polluted na madini zebaki.
 
Hio biashara ya mochwari ngumu Sana kuidhibiti.
Hakuna mfanyabiashara anaejali afya yako bali pesa zako. Huko kwenye migahawa mbona tunalishwa uchafu mwingi tu
 
Hii itamkost Philip mpango na sio ajabu akaondolewa maana itatafsirika ni hujuma dhidi ya uchumi wa taifa.
 
Acha kujifanya msomi uchwara wewe.

Serikali yako inawalisha watu sumu za migodini halafu wanasingizia maiti.
Mimi sijajifanya msomi uchwara, hizo ni fikra zako kama ulivyo kiasili.
Bado elimu yahitajika kwa jamii na serikali kwa ujumla kwa faida ya wote.
Sumu za migodini kuathiri wananchi ni matokeo ya ujinga na upumbavu kwa walio serikalini na pia raia.
Raia wana uwezo wa kudhibiti serikali kwa namna moja au nyingine.
 
Kuepusha hii biashara ya maji bora ukaoshee nyumbani. Maadamu waganga wapo, mitume na manabii wa uongo wapo, hii ni biashara endelevu yenye kuwaneemesha wauzaji na wanunuzi in blacks market
 
Je, wanaijua zebaki au kwa lugha ya malkia inajukana kama Mercury hii ni moja ya kemikali hatari inayosababisha saratani na ndio inayotumika hasa kwenye shughuli za migodini kusafishia dhahabu.
 
This is a very cheap argument, maji ya kuoshea maiti yana uhusiano gani na kutokea saratani.......do you have any mechanism behind.
Labda tuseme unamaanisha kemikali inayotumika kuhifadhi maiti, mfano formalin......hivi inaingia akilini utumie formalin kwenye samaki na isilete usumbufu kwa watu wanaohusika na wateja kwa kupiga chafya au kuwashwa machoni? Hizo kemikali are very pungent ukiifungua kidogo tu hapawezi kukalika.

Kama swala ni saratani inasabbishwa na hivyo vitu kutumika kuhifadhia samaki, logic inaonyesha kwamba case za saratani zingekuwa nyingi mikoa ya mbali na Mwanza maana ndo watatumia zaidi samaki waliohifadhiwa kuliko Mwanza ambako tutategemea watu wengi wanatumia samaki fresh ambao hawajahifadjiwa na kitu chochote.
Hawa watu wanajaribu kupotosha kiini cha saratani kuwa juu huko Mwanza sijui kwa maslahi ya nani. Wafanye utafiti wenye mashiko, tatizo la saratani kuwa juu kanda ya ziwa ni kutokana na kemikali za migodini zinazoelekezwa kwenye vyanzo vya maji ikiwemo mito na kuishia ziwani. Haya ndo yaleyale ya tume ya Manyere kwamba samaki wa mto Mara walikufa kutokana na kuzidiwa na kinyesi na mikojo ya ng'ombe. Pathetic!!
Mkuu, naomba nikunukuu: "Hawa watu wanajaribu kupotosha kiini cha saratani kuwa juu huko Mwanza sijui kwa maslahi ya nani. Wafanye utafiti wenye mashiko, tatizo la saratani kuwa juu kanda ya ziwa ni kutokana na kemikali za migodini zinazoelekezwa kwenye vyanzo vya maji ikiwemo mito na kuishia ziwani."
Naunga mkono hoja hii na Ingefaa wabobezi wa Utafiti (Scientific Researchers) waanzie hapo na kupanua wigo pia kuhusisha dhana (Hypothesis) nyingine ili kupata/kugundua kiini halisi cha Tatizo. Wasijali sana maneno ya mitaani bali wao wajikite kwenye utafiti wa kisayansi. Huku mitaani perepeche ni nyingi sana.
 
Story za vijiweni zinamsumbua
To some extent inawezekana ni kweli, Binafsi niliwahi kusikia kwa jamaa yangu ambaye kaka yake anafanya kazi mortuary kwamba moja ya vitu vinavyowaingizia kipato ni maji ya maiti, I was little shocked, na nikapuuzia.
 
Salaam,

Tafiti zinaonesha kwamba wagonjwa wengi wa Saratani wamekuwa wakitokea Kanda ya Ziwa jambo ambalo linapelekea Serikali kuhangaika kutafuta sababu kwanini Kanda ya Ziwa?

Jana nimeona Mh Makamu wa Rais akiwa hospitali ya Bugando ameeleza moja ya sababu inayopelekea takwimu za saratani kuwa juu Kanda ya Ziwa ni watu wanaotumia maji ya kuoshea maiti kuhifadhia samaki.

Nimeona niijulishe Serikali kwamba moja ya wateja wakubwa wa maji haya ni waganga wa kienyeji na maji haya yanauzwa kwenye maduka ya dawa asili.

Ili Serikali ifanikiwe kudhibiti usambaaji wa biashara hii nashauri wahakikishe masoko yote pamoja na mochwari ambapo ndipo yanapotoka wanadhibiti vinginevyo tatizo hili litaendelea.

Asante.
Tatizo ni chemicals za mining kuingia kwenye water system! Samaki anaifadhiwa asioze ,akiwekewa hajo maji ayana chemical ya kuua bacteria
 
Kansa inaenea zaidi kwa matumizi ya vyombo vya plastic kupakulia vyakula vya moto, matumizi ya nailoni kufunga vyakula vya moto, magazeti na makaratasi yenye wino kufungia vyakula.

Kifaa chochote cha plastic kupatapo moto ni lazima kichuje rangi na zile rangi ni sumu. Na mwili hauna uwezo wa kupambana na kemikali za sumu.

Angalia wenzetu Kenya mamlaka zao zinachukua hatua ukikutwa na vyombo vya plastic, magazeti au nailoni ndo umegeuza sahani.

Unakuta mpumbavu anaweka chai au chakula cha moto kafungiwa kwenye mfuko wa nailoni.
 
This is a very cheap argument, maji ya kuoshea maiti yana uhusiano gani na kutokea saratani.......do you have any mechanism behind...​
Lakini yakisemwa na wakubwa usipuuze labda wana taarifa.
 
Tuachane na samaki wa Mwanza tu

Nyama za watu ??? !!
Ni Kweli bt ni hiari Yako kuamini, unalipia pesa ya kilo ya nyama bt unapewa ya binadamu, mambo hayo ni ktk Ulimwengu wa Roho wa Giza .

Ni muhimu kuombea vyakula unavyonunua ktk masoko au butchers Mungu anaweza kuvizuia visibadilishwe kuwa uchafu huo nilisema maana Kuna madhara makubwa usipoomba kutakasa.

Ameeen
 
Ni Kweli bt ni hiari Yako kuamini, unalipia pesa ya kilo ya nyama bt unapewa ya binadamu, mambo hayo ni ktk Ulimwengu wa Roho wa Giza...
Ndio maana mimi nilishaamua kuwa vegetarian !! Maharagwe kwa sana and the like !
 
Wamekuset umejaa, tatizo ni kubwa kuliko unavyofikiri.

Mfanya biashara yeyote wa samaki au butcher duniani kote anaenda Kwa mganga hutumia maji hayo,...
Naona na wewe unazidi kuniset ili niendelee kujaa aisee

Dah
 
Salaam,

Tafiti zinaonesha kwamba wagonjwa wengi wa Saratani wamekuwa wakitokea Kanda ya Ziwa jambo ambalo linapelekea Serikali kuhangaika kutafuta sababu kwanini Kanda ya Ziwa?

Jana nimeona Mh Makamu wa Rais akiwa hospitali ya Bugando ameeleza moja ya sababu inayopelekea takwimu za saratani kuwa juu Kanda ya Ziwa ni watu wanaotumia maji ya kuoshea maiti kuhifadhia samaki.

Nimeona niijulishe Serikali kwamba moja ya wateja wakubwa wa maji haya ni waganga wa kienyeji na maji haya yanauzwa kwenye maduka ya dawa asili.

Ili Serikali ifanikiwe kudhibiti usambaaji wa biashara hii nashauri wahakikishe masoko yote pamoja na mochwari ambapo ndipo yanapotoka wanadhibiti vinginevyo tatizo hili litaendelea.

Asante.
Kwakuwa yanatoka kwenye hospitali za serilali waanze kudhibiti huko.
 
Utakwepa sumu kwa kutokula samaki utakutana na sumu ya kuhifadhia mahindi kuzuia wadudu kwenye ugali wa dona, maana tumezoea unataka sembe au dona, nipe dona.

Dona wanasaga bila kuosha mahindi, wanasaga matani huo mda wa kukuoshea mahindi wautoe wapi.
 
Back
Top Bottom