Majibu Kwanini Wasanii Wetu Hawaitwi Kwenye Steji Kubwa Duniani


You missed the point, ili Burna boy ajaze huo uwanja hao promoters wanaompa hiyo show are more than likely kuwa ni wanigeria wenyewe au wanaangalia mtu gani ambaye tayari ana fanbase besides the locals. I believe unajua wanaija wapo kila kona.

Wanigeria wapo in the boardrooms. Wakati wa maoni ya nani aitwe kutumbuiza kwenye shows mbalimbali duniani wao ni part ya watoa maamuzi hence wanapeana mashavu. Ndo maana nimesema unashangaa vp mnigeria kutumbuiza kwenye NBA All-stars mchezo ambao tayari una watu wenye asili ya Nigeria kibao from players, makocha hadi presidents wa timu. Nikianza kuorodhesha execs wenye asili ya Nigeria kwenye kampuni mbalimbali kubwa duniani sitamaliza hapa.

Back to your point; Wakati bongo flava ina identity ilifika wapi? Au bongo flava ya 2000s nayo haikua na identity?

Unaujua mziki wa Uganda? Kuna nchi conservative kama Uganda when it comes to music? Nenda clubs za Uganda husikii mziki wa nje zaidi yao na wanaimba strictly mziki wao kwa identity yao, leo hii waganda wapo wapi? Wamefika wapi? Umewaona huko grammys (ambako dayamondi alipafomu online), BET (ambayo Rayvanny anayo), UEFA au World cup?

Wakongo na bolingo yao wapo wapi au nao hawana identity?

Mziki ni kama products zingine unakua exported na natives wenyewe sio lazima wote wawe exces hata wananchi wa kawaida wana mchango wao. The bigger your network, the bigger your success. Hamna mtu anfanya everything by themselves.
 
Technically uzi umegeuka wa Diamond. Kwa nini?
Sababu ni msanii mkubwa sana na hana mpinzani unapokuja uwakilishi.

No doubt. Nimejaribu kuchambua vikwazo anavyokutana navyo pamoja na juhudi zake zote, kimsingi Samaki ndani ya aquarium hawezi kuwa mkubwa zaidi ya aquarium yenyewe.
 
Hakuna cha wanaijeria kwenye boardroom sijui kuamua nani apewe show nani asipewe,
Haya ni mawazo ya mediocre yanayokwepa uhalisia kuwa wasanii wa Tz hawana mziki wa maana wenye kukubalika internationallykwasababu ni copy and paste musician na watanzania mmezoshwa kulishwa hayo matango pori.

Yani unataka kutuambia Rema/Wizkidi/Burnboy/Davido wanaenda kufanya Show O2 Arena na kuuza tiketi zote baada tu ya wanaijeria kushauri kwenye boardroom kuwa huyo ni msanii bora???
Yani wazungu ni wajinga kiasi hicho cha kushindwa kutazama kwenye Billboards na kuona ni nyimbo ya msanii gani wa africa inayotamba kwenye charts za dunia eti mpaka wanaijeria kuumpigia chapuo kwenye boardrooms????
Hell no. Acheni kutafuta justification za kivivu.
 

Ambazo sio copy kwanini hazifiki? 2000s bongo flava ilikua copy ya wapi na ilifika wapi?
 
Nashangaa sana watu wanaposema eri vijana wa sasa ni wa hovyo....wakati ukweli ni kwamba baba zetu na mama zetu ndio wa hovyo.
Wakati wenzao wanatimba ulaya na marekani wao walikuwa wanademka tuu
 
Ambazo sio copy kwanini hazifiki? 2000s bongo flava ilikua copy ya wapi na ilifika wapi?
Hebu tafuteni kichaka kingine cha kujificha ila sio eti kusingizia wanaijeria wapo wengi Abroad ndiyo maana mziki wao unatamba Abroad.
Fanyeni assignments zenu vizuri watz mnapenda sana kutoa excuse za kuwafanya mjifiche kwenye comfort zone.

Mjiulize why Remmy Ongala/ Bi. kidule walikua wanapata show nyingi za Ulaya lakini Afande Sele yupo anafanya show kwa kiingilio cha bia huko uswekeni????
 
Pia Lugha inachangia Sana.Mi nafikiri masanii ukianza fanikiwa nenda British Council kasome kingereza ukisha jua Kingereza tunga na nyimbo za kingereza.English Ni International language.
 

Show za Ulaya Kila mtu anapata hiyo sio ishu kabisa ila zina ukubwa gani. Hao wamepata show nyingi abroad kuliko dayamondi au rayvanny aliyeshinda BET na kupafomu MTV? Dayamondi kawania bet as well na kapafomu Grammy's. Bi. Kidude na Remy wameshinda nini? Wamepafomu wapi?

Vp mziki wa Uganda au Congo hauna identity? Umefika wapi? Naona unazunguka mbuyu bila majibu ya hili swali.

Kuna zaidi ya wanigeria laki5 USA pekee achilia mbali vizazi vyao, how can you underestimate their influence. Robo ya hao tu waki-stream mziki wao repeatedly tayari una top the charts. Hapo sijagusa idadi Yao UK let alone the whole of Europe. Hivi Mzungu atakua willing kwenda kwenye show ipi Kati ya mnigeria huku tayari ana jirani mnigeria na wanakutana hapa na pale au ya mbongo wakati hajawahi kabisa isikia nchi ya TZ? Understand the snowball effect.
 
Nimeishia hapo iliposema eti kuwa Diamond ameperform kwenye Grammy πŸ˜‚
Alafu tena unajiuliza eti Bi.Kidude na Remmy Ongala waliperform wapi? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Una miaka mingapi chief??
Yani unauliza mziki wa Congo umefika wapi kwelii ?

Mstari wa kwanza tu unasema show za ulaya kila mtu anapata πŸ˜‚
Huyo kwenye Avatar yako unaweza kutaja show zake 3 za Ulaya?


Hiyo dhana yenu kuwa wazungu ni bongolala hawajui mziki mzuri wa afrika mpaka wawe influenced na wanaijeria wanaoishi Abroad ni dhana potofu na kichaka kwa kukwepa majukumu ya kuwa wabunifu zaidi.

Tafuta sound yako be original utafanya la maana na utasikilizwa na kila race.

Hamkawii kusema hata Selina Gomez amefanya featuring na Rema kwasababu wanaijeria ni wengi duniani πŸ˜‚
 

Magnitude ya hizo shows that's the point. Ukitaka show za Ulaya unapata ila zina magnitude gani.

The burden of proof is on you to prove your case kwa jambo lolote unalolipinga sio Mimi.

Mziki wa Congo umefika wapi? Wameshinda Grammys ngapi? Wameimba UEFA, world cup au all-star? Mcongo gani kajaza O2 arena? Wacongo nao identity Yao imepotea maana siwasikii kabisa siku hizi.

Bi. Kidude na Remy Wana tuzo ngapi internationally? Walijaza stadiums nao kwa nyimbo zao za asili? Walipafomu wapi mega performances?

Remix ya Rema na Selema imefika pale sababu Rema had shoulders to stand on, wimbo ukawa mkubwa Selena akausikia au unadhani Selena alienda Google kusearch any African song ili afanye remix tu for nothing πŸ˜…

Snowball effect is a foreign language to you my friend.
 
Hawa wa_Naija hawafai. Actually Africa nzima hakuna wakuwafikia kwa ku_hustle. Wewe hushangai hadi Bongo wapo kutafuta fursa! Naamini hiyo iko ndani ya DNA yao.

Sisi tushindane tu na Waafrika wengine akina Kenya na wengine.
 
Eti had shoulders to stand on πŸ˜‚

Ur 1st shoulder to stand on must be your own creativity & Identity. Sio hizi copy & paste zinazofanywa na icon wenu mkubwa wa nchi(diamond)mnayemtegemea awawakilishe na matokeo yake ndiyo huyo sasa mko naye wavuvi camp wakati wenzake wakiwa kwenye jukwaa la world cup wanafanya performance.
 

Mrisho Mpoto, Bi. Kidude, Remy Ongala, Mr. Nice, na wote wanaoimba strictly Tanzanian wamefika wapi? Wameshinda nini, wamejaza kumbi gani ughaibuni? This is no knock to them by any means ila najaribu kuelewa. Nitajie mifano concrete.

Tofauti ya diamond na hao ni nini kama wote hawajatoboa? If anything dayamondi kashinda tuzo zaidi na kupafomu kwenye stages nyingi zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…