Sioni demokrasia hapa kwa sababu waamuzi ni wananchi.
 
Kushinda haikua rahisi swala hapa ni kupata political mileage ya uchaguzi inayofuata..
Huyu jamaa sio maskin kivile na anashule maarufu dom.
Mkuu yani unataka achukue mtaji wa shule akaweke sehemu ambayo hajui return yake itakuwaje?
 
Sasa unategemea ACT ishinde Dodoma kweli?

Huyo kauza jimbo, kaona kuliko nisubiri aibu ya kushindwa bora nibebe hii milion 5 niendelee kula maisha.

Mtu huna hata mia ya kampeni ya nini kupimana ubavu na mwenye nazo?
Ni vyema kama ameamua kujiongeza.
 
Usiseme waliopita bila kupingwa hawa ni WABUNGE WA VITI MAALUM
 
SASA sikilizia Kula za urais zitakavyokua nyingi kutoka majimbo hayo....CCM hodari Sana...yaani Diamond alivyoimba ule wimbo ndio nilijua ni either anakipaji cha kuona mbali au aliletewa mashairi na waona mbali kuwaandaa watu kisaikolojia.
Unamaanisha wimbo wa Baba lao.
 
Watu wanatakiwa wajiulize, mbona wabunge ambao wana uwezo Wa kushinda kama kina Lema, Halima, Sugu, kina Msigwa, Nyalandu, Zitto wao hawakutekwa?

Kwa nini hawa ambao hawana uwezekano Wa kishinda ndiyo wanatekwa?

Akili mukichwa
 
"MAAGIZO TOKA KWA MWENYEKITI-UFIPA STREET':

"Chama hakitapoteza fedha kugharamia wagombea ktk Majimbo ambayo kwa asilimia 99 ni ngome za CCM , Wagombea wote mna wajibu wa kujigharamia wenyewe na hata kutengeneza Matukio na mizengwe mbalimbali itakayowaondoa kushiriki uchaguzi ili tupate Platfom ya Uminywaji wa Demokrasia Kimataifa.

Zingatieni Mbinu 13 alizokuja nazo Lissu, Hatuwezi kutumia Ruzuku au fedha za Sponsors wetu kwa kuzitupa ,hivyo tujiandae kutumia Majimbo hayo ktk kupata Matukio ya kujijenga kisiasa kuliko kujitoa moja kwa moja kwa kutokufanya kitu kabisa" - MWENYEKITI MBOWE

Kama kuna bavicha alitegemea kumshinda Mgombea wa CCM kwa majimbo kama Ruangwa, Morogoro mjini nk basi hiki chama kimejaa watoto wa siasa
 
Watu wanatakiwa wajiulize, mbona wabunge ambao wana uwezo Wa kushinda kama kina Lema, Halima, Sugu, kina Msigwa, Nyalandu, Zitto wao hawakutekwa?

Kwa nini hawa ambao hawana uwezekano Wa kishinda ndiyo wanatekwa?

Akili mukichwa
Wamepiga mpunga kuliko kusubiri kuingia gharama za uchaguzi ambazo makao makuu ya vyama visingelipa.Upinzani bado sana nchi hii
 
Wapinzani kuweni makini! Dodoma na Morogoro itakuwa njia ya kupitisha kura zisizo rasmi za wale majamaa! wana majimbo mengi eti wamepita bila kupingwa
Hivi wewe bado una matumaini ya Lissu kushinda, subiri mapigo matatu yanakuja hadi mtapoteana, wananchi wameshawagundua nyie ni madalali wa nchi yetu, tunakoelekea wagombea wenu watakimbia mechi
 
Sasa unategemea ACT ishinde Dodoma kweli?

Huyo kauza jimbo, kaona kuliko nisubiri aibu ya kushindwa bora nibebe hii milion 5 niendelee kula maisha.

Mtu huna hata mia ya kampeni ya nini kupimana ubavu na mwenye nazo?
Sasa naelewa kwanini wabunge wa ccm pale Bungeni kazi yao ni kuitetea serikali,kumbe ubunge wenyewe wanaupata kwa style hii?
 
Hivi wewe bado una matumaini ya Lissu kushinda, subiri mapigo matatu yanakuja hadi mtapoteana, wananchi wameshawagundua nyie ni madalali wa nchi yetu, tunakoelekea wagombea wenu watakimbia mechi
inavyoonyesha huwa ukilala saa 12 jioni unaamka saa mbili asubuhi- watu wameshaamka mapema hebu amkaa
 
Sasa naelewa kwanini wabunge wa ccm pale Bungeni kazi yao ni kuitetea serikali,kumbe ubunge wenyewe wanaupata kwa style hii?
Sasa kama washindani wao ni njaa kali na ni mambumbumbu kwanini isiwe hivyo
 
Sasa kama washindani wao ni njaa kali na ni mambumbumbu kwanini isiwe hivyo
Sawa mkuu basi acha wakaiwakilishe hiyo serikali,sisi wanyonge acha tuendelee kutazama tu mkuu from distance. Naamini wewe mkuu uko high table na ni miongoni mwa watu wanaowakikishwa na wabunge wa aina hiyo pale mjengoni.
 
Wagombea wa upinzani kuna uwezekano mkubwa wameuza hizo fursa za kugombea. Kwanza kampeni inatakiwa wajigharamie wakati wagombea wenyewe ni maskini. Pili hata kura zikipigwa katika maeneo hayo ni hakika CCM ingeshinda na wao wana uhakika wa hilo.

Kama wakati wa kuchukua fomu walisindikizwa iweje wakati wa kurudisha mgombea aende peke yake? Kama kule Gairo wagombea wa upinzani wamechelewa kurudisha fomu inawezekanaje? Hivi unaamini mtu kama Devotha kule Moro mjini hajui kuwa picha inatakiwa? Je aliwasiliana mwenzake kama Haule wa Mikumi ili kuona kama fomu yake iko sawa? Uongozi wa jimbo na mkoa ulihakiki fomu za wagombea wao kabla ya kuwaruhusu kuzirudisha?

Tatizo la rushwa lipo vyama vyote na ni maamuzi binafsi ya mtu bila kutumwa na chama chake. Hivi kama hao wanaokula rushwa vyama vyao ingetokea vishinde na wao kuteuliwa katika nyadhifa mbalimbali si wangekuwa wala rushwa wakubwa?

Membe jimbo analotoka ACT hawakuweka mgombea makusudi je kama akishinda huo urais anaouota anategemea wabunge toka majimbo mengine?

Kipindi hiki cha uchaguzi kwa wengine ni kipindi cha kuvuna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…