Majungu na kukwamishana Buboka Mjini vyamliza Mbunge Byabato. Apiga magoti na kutoa machozi mbele ya wanabukoba

Majungu na kukwamishana Buboka Mjini vyamliza Mbunge Byabato. Apiga magoti na kutoa machozi mbele ya wanabukoba

Mbunge wa Bukoba wa Mjini na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa anaongea na wakazi wa jimbo wakati akikabidhi mkataba wa ujenzi wa Standi Kuu ya Mabasi hilo amelalamikia majungu yanayoendelea Bukoba Mjini ambayo yanakwamisha maendeleo ya manispaa hiyo kwa miaka nenda rudi.

Baadhi ya miradi ambayo imekuwa ikikwamishwa na wanasiasa kwa maslahi binafsi ni pamoja na Stendi Kuu ya Mabasi Bukoba na Barabara ya Nyangoye ambayo imekuwa ikisababisha vifo na vilema kwa miaka nenda rudi.

Akiongea kwa machungu sana mpaka kupelekea kulia na kupiga magoti anadai kusaidia Bukoba kutekeleza hiyo miradi kwanini iwe NONGWA kwake? Kwanini aanze kupigwa majungu. Ameendelea kudai kuwa atahakikisha miradi hiyo inatekelezwa hata akinyimwa Ubunge 2025 lakini wananchi wakiona miradi hiyo watamkumbuka 'Ni Byabato Omsigazi Tukamwima Obubunge, chonka akabikola'(Ni kijana Byabato Tulimnyima Ubunge lakini aliifanya kazi)

Amesema aliomba ujenzi wa barabara ya Nyangoye, wataalamu wakaja wakafanya upembuzi yakinifu na kupendekezwa upanuzi wa barabara njia nne, na kaya 20 zitalipwa fidia ili kutekeleza mradi huo. Anashangaa kwanini anapigwa majungu!

Amesema kama ni Ubunge 2025 wauchukue lakini wanabukoba wasikwamishane bila Sababu. Ili kuonesha msisitizo wa anachokisema, Naibu Waziri huyo aliamua kupiga magoti na kulia, kabla ya kunyanyuliwa na wananchi.

Amezidi kusema wanabukoba tulimpa ubunge miaka mitano basi tumwamini tuache afanye kazi, hawezi kuacha kujenga Stendi, Barabara na Soko kisa atakosa Ubunge 2025. Anasema bora atekeleze hiyo miradi ili akose ubunge 2025 lakini atakumbukwa na wanabukoba. Kama shida ni ujenzi wa Stendi nzuri Bukoba Mjini.

View attachment 2784184Ni

View attachment 2784184
Nimewahi kufanya kazi bk na meya Dkt. Anatory Amani , nayajua Majungu ya bk vizuri

Sijashangaa
 
Kwa mfumo wa utawala wa nchi yetu ni ngumu sana kwa mbunge kufanya kazi yake vizuri bila majungu!! Mbunge ukipishana mtizamo kidogo na Ded wa Halmashauri yako, ujue lazima atakukwamisha mipango yako na huna la kufanya maana nae ni mteule wa rais, ambae unakuta uyo Rais ndio mwenyekiti wa chama.

Ukipishana mtazamo na mwenyekiti wa chama chako wa wilaya ujue lazima akuundie zengwe la kukukwamisha kwa kushirikiana na wapinzani wako ndani ya chama hata nje ya chama.

Ukipishana mtazamo na mkuu wa mkoa au wilaya hao wana mpaka mamlaka ya kukukamata na kukuweka ndani! Bado wananchi matatizo yao hata ya kibinafsi utaletewa wewe uyatatue na usipo yatatua utakuwa umejenga chuki na uyo ulieshindwa kumsaidia matatizo yake ivyo tegemea kukosa kura yake.

Ndio maana wabunge wachache wenye ukwasi hawana hata muda wa kufanya sijui mikutano na wananchi wanachofanya ni kukusanya pesa kwa njia wanazojua wao ukifika wakati wa uchaguzi ni kumwaga pesa ya dona kwa wajumbe na wapiga kura ambao wengi wao ni masikini au ni wajinga inakuwa ndio tiketi yake ya kurudi bungeni chaguzi zote,ikitokea ded,sijui dc,rc, au mwenyekiti wa chama akaleta usumbufu anatumia pesa zake kuongea na mamlaka ya uteuzi inamtengua au kumuhamisha kituo cha kazi.

Nimeishi Bukoba,nikili ukitoa kabila la warangi na wanyakyusa kabila linalofatia makabila hayo kwa fitna,majungu,uzandiki na ujinga ni wahaya!! Hawa ndugu ni komesha!! Kila mtu wa hilo kabila ni mjuaji, mfitinishaji,wivu na hawapendi maendeleo ya mtu na ni wavivu mno, hivyo uyo bwana mdogo Byabato hana kazi kubwa sana hapo bukoba.
 
Yani wahaya wasikie tu kwa jirani usiombe kuishi nao au kufanya Kazi nao!!
Ni wanakera unaweza kimbia ofisi hasa kilugha Chao wakija ofisini kama huongei kihaya haki wanakuona kama takataka na Wana majungu na roho mbaya mpaka shetani anapiga salute
 
Alitakiwa kupiga mkwala tu na siyo kulia.
Ni kweli hakutakiwa kulia. Kafanya kosa kubwa. Kaonyesha udhaifu. Na hasa kwa mila za kihaya, mwanaume kulia mbele za watu, ni udhaifu.

Ila imemsaidia ametoa ya moyoni. Anapouliza umati "Rwamishenye waitu?"maanake kama siyo ubunge, upanuzi wa barabara ya Nyangoye angependa uwe Nshambya inayopita kwake.

Nirudi kwa wana Bukoba. Shida ya mji wa Bukoba na Kagera kwa ujumla ni umaskini. Si stendi nzuri wala barabara pana vitakavyoongeza mzunguko wa pesa. Kwa hiyo mnakosea kwenye priorities. Kumbuka kuna stendi nzuri Dodoma lakini hata fremu za maduka hazina watu wa kuzikodi. Pale Nyegezi, ila bado walala hoi wanauza mandazi na mihogo nje ya stendi kwenye vumbi.

Zamani, kulikuwa na mlundikano wa watu, myaka ya nyuma, uliokuwa unasababishwa na abiria wanaosubiri meli jioni, kwa sasa haupo tena. Mkusanyiko huu, wasafiri walikuwa wanalazimika kukaa siku nzima wakitumia pesa hapo mjini. Kitendo cha barabara ya lami Bk to Mz, kimevunja mzunguko wote.

Pia, hapo zamani, Kilimo cha kahawa kilikuwa ni utajiri wa kila kaya. Sasa kahawa haipo kwa kiasi kikubwa kwenye familia nyingi. Hivyo hakuna chanzo cha kuaminika kwenye familia nyingi. Watu wanadandia vanila na parachichi ambavyo haijaonyesha ufanisi.

Kuna wahaya wengi wenye hela, lakini ukosefu wa mzunguko unawapa hofu ya kuwekeza nyumbani.
 
Ni wanakera unaweza kimbia ofisi hasa kilugha Chao wakija ofisini kama huongei kihaya haki wanakuona kama takataka na Wana majungu na roho mbaya mpaka shetani anapiga salute
Nakupata vizuri sana mkuu hawa watu ni nyokko! 🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌!
 
Back
Top Bottom