Majungu na kukwamishana Buboka Mjini vyamliza Mbunge Byabato. Apiga magoti na kutoa machozi mbele ya wanabukoba

Subiri baada ya miezi sita...mkandarasi yuko site...
Kwanza a big win ni kufanikiwa kuondoa mabus na magari yote kutoka pale...sijui walifanyaje aisee
Maana ilikuwaga mgogoro mkubwa sana...

Sasa leo wako wanajenga na watu wako site
Ukilazimisha mambo yanaenda, miradi ya bukoba haitakiwi kupitia kwa wanasiasa maana wanakaa kubembeleza na mwisho wanakwamishana wenyewe
 
Yes...hata huo mji inabidi daladala zirudishwe...wakijemga hiyo dual carriageway wasisahau kujenga vituo vya daladala
Mambo ya kukumbatia bodaboda ni siasa tu...
 
Mbunge wa Bukoba wa Mjini na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa anaongea na wakazi wa jimbo wakati akikabidhi mkataba wa ujenzi wa Standi Kuu ya Mabasi hilo amelalamikia majungu yanayoendelea Bukoba Mjini ambayo yanakwamisha maendeleo ya manispaa hiyo kwa miaka nenda rudi.

Baadhi ya miradi ambayo imekuwa ikikwamishwa na wanasiasa kwa maslahi binafsi ni pamoja na Stendi Kuu ya Mabasi Bukoba na Barabara ya Nyangoye ambayo imekuwa ikisababisha vifo na vilema kwa miaka nenda rudi.

Akiongea kwa machungu sana mpaka kupelekea kulia na kupiga magoti anadai kusaidia Bukoba kutekeleza hiyo miradi kwanini iwe NONGWA kwake? Kwanini aanze kupigwa majungu. Ameendelea kudai kuwa atahakikisha miradi hiyo inatekelezwa hata akinyimwa Ubunge 2025 lakini wananchi wakiona miradi hiyo watamkumbuka 'Ni Byabato Omsigazi Tukamwima Obubunge, chonka akabikola'(Ni kijana Byabato Tulimnyima Ubunge lakini aliifanya kazi)

Amesema aliomba ujenzi wa barabara ya Nyangoye, wataalamu wakaja wakafanya upembuzi yakinifu na kupendekezwa upanuzi wa barabara njia nne, na kaya 20 zitalipwa fidia ili kutekeleza mradi huo. Anashangaa kwanini anapigwa majungu!

Amesema kama ni Ubunge 2025 wauchukue lakini wanabukoba wasikwamishane bila Sababu. Ili kuonesha msisitizo wa anachokisema, Naibu Waziri huyo aliamua kupiga magoti na kulia, kabla ya kunyanyuliwa na wananchi.

Amezidi kusema wanabukoba tulimpa ubunge miaka mitano basi tumwamini tuache afanye kazi, hawezi kuacha kujenga Stendi, Barabara na Soko kisa atakosa Ubunge 2025. Anasema bora atekeleze hiyo miradi ili akose ubunge 2025 lakini atakumbukwa na wanabukoba. Kama shida ni ujenzi wa Stendi nzuri Bukoba Mjini.

View attachment 2784184
Upuuzi tu, maigizo haya, wakirudi Bungeni wanapitisha sheria za ovyo dhidi ya wananchi huku wao wakijiongezea kinga.
 
Ni vilaza tu...ona walivyofeli kuendesha nchi...BRT, SGR, umeme, maji kote pameoza...kwa nini tusiwaite vilaza?
Wewe ni mzima kichwani?
Screenshot_20231010-090014.jpg
 
Bukoba kuna majungu sana miaka na miaka. Sina hakika kama Byabato atarudi 2025. Cha msingi akomae atukamilishie hiyo miradi
Kiukweli Kuna Majungu, Misifa, kuharibiana na kupenda Kesi Mpaka Siyo Poa. Kule Mtu anaenda kusoma Sheria ili tu ashinde mahakamani kubishania kesi; anaweza akatengeneza Mgogoro wa kimpaka ili tu mfikishane mahakamani ili mkaoneshane uwezo wa Kisheria. Hawa Watu Wanajua kuumba Majungu yenye mpaka ushahidi wa Uongo. Mfano unaweza ukawa Kwenye Kijiwe cha kahawa unakunywa Kahawa lakini wakakuzushia kuwa kwenye Kijiwe cha kahawa unakunywa Gongo.
Hawa Inshomile ni laana kila Kona na Usipmbe hata kufanya kazi nao lazima Ujute kuzaliwa lazima akuharibie tu😂😂😂😂.
NB: Hata Hapa Mtandaoni Mtu anaweza akatafuta Kesi kutengeneza Kosa la Kimtandao wacha nikimbie nikajifiche😎😎😎
 
Huo mkoa haufai.Si wanawake si wanaume wote ni wanafiki na ni wapiga Majungu.Mkoa hauendelei miaka nenda rudi uko vile vile hata mh mchengelwa alipoutembelea mkoa huo aliushangaa ulivyo duma.hao ndo akina nshomile bwana.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Eti hauendelei labda ungetuambia Kagera inazidiwa nini na mikoa mingine??
 
Wahaya na majungu, unafiki, umbea wa mambo yasiyowahusu ni pete na kidole.

Bado wanaamini kwenye kusomesha watoto wapate ajira sio wajiajiri, bukoba mtoto kufika chuo kwao bado ni ufahari pasipo kuwaza what next after chuo.

haya LAND Mhaya Mhaya wa mjini badilikeni ndugu

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Nahisi kuna waislamu wengi zaidi ya wakristu.Huyo atakuwa anapigwa majungu sababu mojawapo ni udini.
 
Mbunge wa Bukoba wa Mjini na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa anaongea na wakazi wa jimbo wakati akikabidhi mkataba wa ujenzi wa Standi Kuu ya Mabasi hilo amelalamikia majungu yanayoendelea Bukoba Mjini ambayo yanakwamisha maendeleo ya manispaa hiyo kwa miaka nenda rudi.

Baadhi ya miradi ambayo imekuwa ikikwamishwa na wanasiasa kwa maslahi binafsi ni pamoja na Stendi Kuu ya Mabasi Bukoba na Barabara ya Nyangoye ambayo imekuwa ikisababisha vifo na vilema kwa miaka nenda rudi.

Akiongea kwa machungu sana mpaka kupelekea kulia na kupiga magoti anadai kusaidia Bukoba kutekeleza hiyo miradi kwanini iwe NONGWA kwake? Kwanini aanze kupigwa majungu. Ameendelea kudai kuwa atahakikisha miradi hiyo inatekelezwa hata akinyimwa Ubunge 2025 lakini wananchi wakiona miradi hiyo watamkumbuka 'Ni Byabato Omsigazi Tukamwima Obubunge, chonka akabikola'(Ni kijana Byabato Tulimnyima Ubunge lakini aliifanya kazi)

Amesema aliomba ujenzi wa barabara ya Nyangoye, wataalamu wakaja wakafanya upembuzi yakinifu na kupendekezwa upanuzi wa barabara njia nne, na kaya 20 zitalipwa fidia ili kutekeleza mradi huo. Anashangaa kwanini anapigwa majungu!

Amesema kama ni Ubunge 2025 wauchukue lakini wanabukoba wasikwamishane bila Sababu. Ili kuonesha msisitizo wa anachokisema, Naibu Waziri huyo aliamua kupiga magoti na kulia, kabla ya kunyanyuliwa na wananchi.

Amezidi kusema wanabukoba tulimpa ubunge miaka mitano basi tumwamini tuache afanye kazi, hawezi kuacha kujenga Stendi, Barabara na Soko kisa atakosa Ubunge 2025. Anasema bora atekeleze hiyo miradi ili akose ubunge 2025 lakini atakumbukwa na wanabukoba. Kama shida ni ujenzi wa Stendi nzuri Bukoba Mjini.

View attachment 2784184

Mbunge Mzuri Sana lakini anaoponzwa Sana na kubebwa na magufuli. , alikuwa wa nne kwenye kura za maoni …Huyu kazidi pengine anamkaribia Phillip Mulogo ambaye yeye aliamua kugalagala .
UKIACHA waliopiga Magoti kama Yule wa karagwe ……

Ni wazi wabunge ambao walibebwa na magu wana kazi Ngumu Sana kama hawatakubali kusimama wenyewe kwa Miguu Yao na kutegemea kubebwa
 
Back
Top Bottom