Makampuni ya Marekani ya kutengeneza semiconductors waitaka serikali ya Marekani kuiondolea vikwazo China

Makampuni ya Marekani ya kutengeneza semiconductors waitaka serikali ya Marekani kuiondolea vikwazo China

17 July 2023,
Washington

View attachment 2691456


Umoja wa makampuni ya kutengeneza semiconductor (chips) nchini Marekani US-based Semiconductor Industry Association (SIA), umeitaka serikali ya Biden kuondoa vikwazo ilivyoiwekea China katika kuiuzia baadhi ya semiconductors na katazo la kutoruhusu makampuni ya Marekani kuwekeza katika uzalishaji wa chips nchini China.

Viongozi wakuu wa makampuni hayo wameutaka uongozi wa Biden kuiondolea vikwazo China kwa sababu China ndilo soko kuu la semiconductors duniani.

Viongozi wakuu wa makampuni makubwa ya Marekani ya kutengeneza chips ya Intel Inc, Qualcomm na Nvidia wamekutana leo Washington na maafisa wa biashara, uchumi na ulinzi wa serikali ya Marekani ili kuzungumzia athari wanazopata kutokana na sera ya Marekani kwa China dhidi ya kuiuzia chips.

Hizi ni sababu kuu mbili za viongozi wakuu wa makampuni hayo kutaka serikali ya Marekani kuondoa vikwazo kwa China;

(1)Kushuka kwa mauzo ya semiconductors kadiri Washington inavyozidi kuiwekea Beijing vikwazo. Hivyo wanashindwa kuelewa hatma ya biashara hiyo.

(2)China kuweka vikwazo vya kuiuzia Marekani madini ya gallium na germanium ambayo ni muhimu sana katika utengenezaji wa semiconductors
.

Baada ya kutathmini changamoto hizo viongozi wakuu wa kampuni hizo kubwa za utengenezaji wa chips kwa pamoja wameutaka uongozi wa Biden kuondoa vikwazo kwa China.

Hii ndio ile inaitwa mwaga mboga namwaga ugali AU unapigana na mtu unamkaba koo yeye anakamata huku kwa chini katikati ya miguu...
 
Hii ndio ile inaitwa mwaga mboga namwaga ugali AU unapigana na mtu unamkaba koo yeye anakamata huku kwa chini katikati ya miguu...
Hatari sana. Hapa kwa maneno mengine sera ya Biden ya kutoiuzia China chips imekosolewa na watengenezaji chips wa Marekani, wametumia lugha ya kidiplomasia kupunguza makali kulinda heshima ya mzee
 
Insikitisha kuona serikali inaweka sera au sheria za kibiashara ambazo zinaumiza wazalishaji wa ndani. Sijui kama Pro-NATO wanatambua hilo
Humo USA hakuna wataalam wa kuliona Hilo mapema?

Haya mambo hata na Urusi wamefanya hivi hivi kuhusu nishati na nafaka,,Leo wanalia
 
Naona wakubwa wanabanwa MBUPU mchina kamkazia Blaza USA huku Urusi akiwamwagia uji wa motomoto Ulaya hakika ni fahari kuyashuhudia haya ktk kizazi hiki na msije mkadhani pro USA hawajaiona hii thread.
 
NIlikuwa nawaambia watu humu kuwa wafanyabiashara wa Marekani hawapendezwi na sera za nchi yao za kibishara dhidi ya China ukizingatiaChina ni soko kubwa sana duniani
Daah!! Kumbe China inahitajika Sana na marekani sikujua hili, wote wanahitajiana sasa sijui marekani wataidhibiti vipi China kiuchumi
 
Wataalam hawakufanya research kabla ya kuweka katazo hilo? Nashangaa mbona!
 
Changamoto wanazokumbana nazo ni kubwa kwa sababu haya tuseme mzigo mnao kwenye stock unadoda kwa sababu soko lenu kubwa limepigwa pin. Mtalipaje gharama za operating cost

Ok haya wakisema wafanye uzalishaji wamepigwa pin na China kupata madini muhimu

Ndio maana mwisho wa siku hao viongozi wanabaki kusema hawaelewi hatma yao
Na baada ya miaka 5 .China atakitosheleza kwa chip. Hizo za marekenai watakaangia mayai chips

[emoji630]
 
Yule mpiga punyeto wa kimataifa atasema hizi ni propaganda za Urusi
 
Back
Top Bottom