Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini hapa.

Msafara wa Samia umefika hospitalini hapa saa 11.43 jioni akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana.

Mwananchi lililokuwapo hospitalini hapo wakati Mama Samia, Balozi Chana na maofisa wengine wakiwasili hospitalini hapo.

Lissu amelazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 aliposhambuliwa Septemba 7 akiwa nyumbani kwake, Area D mjini Dodoma.

Makamu wa Rais amefika hospitalini akiwa njiani kurudi Tanzania baada ya asubuhi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta.

Samia anakuwa kiongozi mkuu wa kwanza wa Serikali ya Tanzania kumtembelea Lissu hospitali tangu alipolazwa usiku wa Septemba 7.

 
  1. Nasikia kuna mtu Mwenye frastruation jumapili alimwambia Polisi likubwa pale Bandarini " Kama mtu anakunanihii mtwange".!!!
  2. Lissu YUpo hospitali baada ya kutwangwa risasi kadhaa na watu wasiojulikana
nawaza tu japo nimelewa pombe kali ....... akili za pombe sio nzuri
 
Mmhhhh,
Tusubiri arudi tuone itakavyokua
 
weka picha ili tuamini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…