Makanisa yanalipa sana! Pastor Tonny Kapola anunua eneo kwa dola milioni tatu Mwenge kwa ajili ya kujenga Kanisa

Makanisa yanalipa sana! Pastor Tonny Kapola anunua eneo kwa dola milioni tatu Mwenge kwa ajili ya kujenga Kanisa

Ni biashara poa sana, maana wengi wetu bado wajinga,kama Mungu kakupa kipaji cha kuongea, upo charismatic, eloquent, una ka degree, na uelewa kidogo, fungua kanisa tu, watu kama Dokta Mwaka, Masoud Kipanya, Oskar Oskar, Sugu,wakifungua makanisa, mpunga nje nje,
Huwa nawasikiliza Kuhan Musa, na Mwamposa, nabaki natabasamu tu!
Tangu kipindi hicho, cha miaka ya, 90,mikutano ya injili ilipoanza pale Jangwani, Sijawahi kukutana na kilema, aliyepona ninaye mjua kitaa nilipokuwa naishi, wengi tunaowaona wakitupa magongo, na kunyooka viungo, kwa sababu moja au nyingine huwa sio wakazi wa kitaani eneo Hilo!
Ukiwa dar, utaaambiwa wametoka kigoma, kagera, mkutano ukienda singida, watoa ushuhuda, watatoka mtwara! Miujiza hii!
Hata mimi hili nimeshajiuliza sana. Mfano hakuna mkazi kutoka pale pale Kawe amewahi kutoa ushuhuda wa kupona. Wakienda Mbeya wanaopona wanatoka Dar au Moro, wakija Dar wanaopona wanatoka Mbeya au Songea
😂😂😂😂😂😂
 
WANAPIGA HELA KWA SABABU

1. HAWALIPI KODI YOYOTE KWA SERIKALI HIVYO KIBUNDA CHOTE KINAINGIA MFUKONI

2. WATU WAKUBWA WANAWATUMIA KUTAKATISHA PESA ZAO WANASIASA PAMOJA NA WAUZA UNGA

NYONGEZA: Misikiti na Makanisa Hayalipi Kodi yoyote ile kwa Sirikali Hivyo watu washenzi hutumia huko kusafisha Pesa ZAO. 😁
 
Mkuu acha kujidanganya.

Unakumbuka Alex Msama?

Kuandaa Tamasha mashuhuri ina cost 100 to 200M.

Amefanya hiyo kazi kwa miama kibao. Alishafiriska.

Unatumia 300M kuandaa tamasha na watumishi maarufu au waimbaji lakini Return za michango na harambee zinaangukia kwenye 250M unakula hasara ya 50.

Jamaa ana kesi mpaka leo za madeni.

Kuwa realistic hutawaza hivyo.

Nikuombe tu mfahamu Prophet Bushiri then ukasome Makala ya Uchunguzi wa kiintelijensia " The Gold Mafia" ya Aljazeera.

Utaelewa na uache kupaniki.

Vijana mtaangamia kwa kukosa maarifa.

Hii makala itakupa insights pia kwa nini Vita ya Congo haiishi
Kuna mchungaji mmoja alikuwa na kanisa lake bongo, alikuwa mnigeria
Sasa kuna jamaa mmoja alikuwa anasali kwake kila nkiongea naye jamaa alikuwa anamsifia sana
Akitaka na mm nihidhurie,mm nkamwambia huyo mchungaji magumashi kwanza anauza ngada...jamaa akanijia juu sana
Kwani alimaliza miezi 2 alipigwa mshindo akakamatwa akakutwa na mzigo na jamaa wawili wazungu panda anajianda kuwaingiza ulaya
Yule jamaa sasa akantafuta akanipigia sim maneno kibao
Ohh ulijuuaje 😄
Nkamwambia watu mjini kitambo
Kumsoma mtu dk 0 tu
Yule mnigeria nahisi mpk leo yuko ngome 😄 waumini wote wamepot3anaaaa

Ova
 
Hata mimi hili nimeshajiuliza sana. Mfano hakuna mkazi kutoka pale pale Kawe amewahi kutoa ushuhuda wa kupona. Wakienda Mbeya wanaopona wanatoka Dar au Moro, wakija Dar wanaopona wanatoka Mbeya au Songea
😂😂😂😂😂😂
Mipango tu ile utapeli

Ova
 
Lengo lao litakuwa limetomia, yaani kukutana kwa pamoja kumuabudu Mungu.

"Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao." - Mt. 18:20
Yohana 4:23
[23]Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
But the hour cometh, and now is, when the true worshippers shall worship the Father in spirit and in truth: for the Father seeketh such to worship him.
 
Hata mimi hili nimeshajiuliza sana. Mfano hakuna mkazi kutoka pale pale Kawe amewahi kutoa ushuhuda wa kupona. Wakienda Mbeya wanaopona wanatoka Dar au Moro, wakija Dar wanaopona wanatoka Mbeya au Songea
😂😂😂😂😂😂
Hongera, maana Kawe ni kubwa sana. Umefanya kazi kubwa sana ya kuchunguza watoa ushuhuda wote na kugundua hakuna hata mmoja anayetoka Kawe 😂
 
Dogo alikuwa kajichokea, dini imebadilisha kabisa maisha yake. Ana tembelea Gari, Mercedes Benz G Guard ya zaidi ya bilioni moja.

Sasa kaja kivingine, anahama pale Millennium Tower Phase 2 na kuhamia rasmi Mwenge alikonunua eneo kwa mabilioni ya FEDHA, pale ilipokuwa Century Cinema.

Washikaji, tutafute upako ili tutoboe
Anzisha nawewe usinisahau hata kuwa Mzee kiongozi wa kanisa lako
 
Biashara ya Dini inalipa kinoma,

Ndo maana ROMAN CATHOLIC wanapesa kuliko Serikali yoyote Ile duniani

Roman Catholic wanamiliki Robo ya kipande Cha ardhi yote ya hii dunia
Wameizidi hata serikali ya TRUMP????
Sikuwahi sikia hilo
 
Back
Top Bottom