Chukwu emeka
JF-Expert Member
- Jan 12, 2018
- 24,314
- 38,919
Aacha utoto, kinachohesabika ni tarehe ya 23/8/2022 hata karani akifika kwako mwezi wa 10 atakuuliza waliolala kwako siku ya 23/08/2022
Jiongeze.... ccm wanataka uhalali wa kutanua wigo wa tozo!Maswali kama haya sikuona ulazima wake
- Una simu janja
- Una computer
- Una baiskel, pikipiki
- Una driving licence, card ya nida, kadi ya mpigakura
- Nyumba imesakafiwa kwa material gani
- Una runinga
- Una paka, mbwa, bata, kuku nk
- Choo yako ni ya namna gani
- Umeshawahi kusafiri ndani ya mwezi huu
Hata mimi nimeshangaa anakushambulia wakati zoezi lenyewe lina mapungufu.Hii si changamoto yangu, nimesema nilichokishuhudia , anyway sijui kosa langu ni lipi
Mzee mgumu sana kuelewa? Wewe kuhesabiwa au kutokuhesabiwa hakuwezi kuzuia zoezi kuendelea na kuisha!Uko sahihi, hebu nisaidie hili. Leo niko Mwanza kikazi na sijahesabiwa hapa, narudi alhamisi Dar ambako ndiko makazi yangu yalipo. Je sintokuwa na sifa ya kuhesabiwa huko Dar maana sikuamkia huko tarehe 23/8/22?
Zoezi lote ni la mchongo wa upigaji... kuna watu baada ya zoezi lazima wanunue viwanja, magari, nyumba n.k kwa mchongo huu wa sensaHata mimi nimeshangaa anakushambulia wakati zoezi lenyewe lina mapungufu.
Kupika data naina kuna kaugumu sana. Kwanza tablet wanayotumia imeungwa na GPS. Nyumba utakayofika kuhesabu imeshasajiliwa kuwa ni ya nani. Kama ukirekodi kuwa umemhesabu mtu flani kwenye makazi flani na taarifa zikatofautiana na zilizoko kwenye rekodi, waweza kujitengenezea msala.
Zoezi lote ni la mchongo wa upigaji... kuna watu baada ya zoezi lazima wanunue viwanja, magari, nyumba n.k kwa mchongo huu wa sensa
Tatizo lako wewe unataka usahahi wa mchakato ili kupata taarifa sahihi.Unafahamu kitu inaitwa Recall bias? Nani atakupa taarifa sahihi ya kilichotokea siku 7 zilizopita (ikiwa itaishia siku ya saba?) Bora wangepitisha karatasi zenye kukusanya taarifa katika kaya, ili hii leo raia wangezijaza halafu wakaja kuzikusanya ndani ya siku 7 zao na kuweka marekebisho panapostahili.
Mkuu... Maswali kuonekana wala si tatizo ni haki. Kwa kuwa ni zoezi linalotumia fedha za umma lilitakiwa kuwa wazi sana.Hamna umakini huo ndugu, usitake kuonyesha ni zoezi lenye umakini wa kiwango hicho, wakati hata maswali yenyewe yameanza kuonekana jana kwenye mitandao. Inshort ni zoezi linaloendeshwa kijima sana, na hayo ni baadhi ya maeneo unayoweza kupima uwezo wa watendaji wetu ndani ya serikali.
Kweli hili zoezi nataka nilifananishe na vitambulisho vya nida 🙂 sarakasi nyingiZoezi lote ni la mchongo wa upigaji... kuna watu baada ya zoezi lazima wanunue viwanja, magari, nyumba n.k kwa mchongo huu wa sensa
Ndo hizo hizo hawatapata za kweli sasa na ni loop hole ya wao kupika data!Kwa kifupi ni kwamba, taarifa zinazotakiwa kwenye sensa ni zile za kuamkia tarehe 23.08.2022.
Kwa hiyo, hata kama Karani wa Sensa atakuja kwako tarehe 25 au 28.08.2022, wewe utampa taarifa kama ilivyokuwa tarehe 23.08.2022.
Watu waliolala katika Nyumba yako usiku wa kuamkia tarehe hiyo 23.08.2022.
Mbona taarifa ilitoka kwamba sensa ni siku sita hadi saba, hivyo unapaswa kuweka kumbukumbu za watu waliolala usiku wa kuamkia tarehe 23.Sasa mbona hawakutuambia tuweke kumbukumbu ya tarehe 23 tu. Tuliambiwa sensa inahesabu watu waliolala nyumbani siku anayopita karani na ikibidi karani anaweza kukagua ili kujiridhisha...
Basi wangeongeza vishikwambi na makarani. Au wangepunguza maswali toka 100 ya Sasa na kubakia 3 tu.
Ili ndani ya dakika 10 kaya 5 zihesabiwe.