Makinda abadili gia angani, asema kuhesabiwa ni siku saba

Nimekaa nyumbani mpaka saa 12 jioni na karani hakuja.... Kwa hiyo kesho naendelea na mishe zangu....
 
Tuliambiwa siku ya sensa ni tar.23/8/2022, baada ya hapo watu waendelee na mishe zao. Na Mimi nazingatia hilo, kesho tusitafutane.
 
Tatizo mnafuatilia mambo juu juu...Hao wanahesabiwa kwenye dodoso la makundi maalumu Yaani waliolala stendi, lodge, masokoni, watoto wa mitaani etc Kazi ilianza usiku ya kuhesabu makundi hayo

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Tatizo mnafuatilia mambo juu juu, hao wanahesabiwa kwenye dodoso la makundi maalumu...Wasiokuwa na makazi maalumu, waliolala stendi, masokoni,lodge, kwenye makambi, watoto wa mtaani. Ambapo kazi ilianza tangu saa 6 usiku kwajili ya makundi hayo

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Kama mtu alikesha kwenye shughuli za ulinzi kuamkia tarehe 23 ya sensa then hakuhesabiwa sehemu alipokesha na hakulala nyumbani, huyo atahesabiwaje kwasababu tunaambiwa ni watu waliolala ndani ya nyumba husika usiku wa kuamkia sensa ndiyo tuwatolee taarifa zao.
 
Uko sahihi, hebu nisaidie hili. Leo niko Mwanza kikazi na sijahesabiwa hapa, narudi alhamisi Dar ambako ndiko makazi yangu yalipo. Je sintokuwa na sifa ya kuhesabiwa huko Dar maana sikuamkia huko tarehe 23/8/22?
Maswali mengine bwana!! Kuna watu hata vyombo vya habari huwa hamsikilizi..Suala hili lishazungumziwa sana hadi mitandaoni humu...Kwamba utaacha taarifa zako ulipolala usiku wa kuamkia tarehe 23. Endapo watahitaji kufahamu zaidi utapigiwa simu

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Wasiokuwa na makazi maalumu, waliolala stendi, masokoni,lodge, kwenye makambi, watoto wa mtaani. Ambapo kazi ilianza tangu saa 6 usiku kwajili ya makundi hayo
Zoezi limeanza leo, kuna watu wamesafiri usiku kucha w barabarani, wao wenyewe wamekiri kutohesabiwa wala kukutana na makarani wewe unalazimisha kuwa wamehesabiwa huko ulikotaja mbona unabishia jambo lililowazi!
 
Kuna watu walidandia fuso jana Kiomboi wamesafiri usiku kucha kwenye gari, mtazungukia magari yote kusaka taarifa zao?
 
Wamekula Bill 900. Wame hujumu idadi ya Makarani. Mm licha ya kushinda nyumbani sija hesabiwa. Hivyo tusimbuane tena!!
 
Kweli Usilolijua ni sawa na usiku wa giza.Nakuhakikishia hayo unayoyazungumzia yalishatambuliwa na yalishapatiwa ufumbuzi na namna ya kukabiliana nalo. Hata ukiwa safarini wiki nzima au hata ukiwa huko migodini lazima utahesabiwa tu
 
Wacha uzushi. Nani alikwambia hayo maneno? Watu milioni 60 Kwa siku moja?! Imetokea wapi Dunia hii?
 
Kuna madodoso ya makundi maalum mfn wasafiri waliolala guest house watoto wa mitaani makahaba wanaojiuza waliolazwa mahospitalini walio kwenye mabweni mahotelini n.k kwa kifupi hakuna atakayeachwa usidhani hilo halikuwekwa katika consideration
 

Kwahiyo niache taarifa zangu guest house niliyolala jana wakati mimi sio mkazi wa huku?
 
Kwahiyo niache taarifa zangu guest house niliyolala jana wakati mimi sio mkazi wa huku?
Ndio, huko kwenye magesti kuliachwa fomu ambapo mtu yoyote aliyeamkia hapo guest au hotelini atajaza na baadae karani atazichukua na kuingiza taarifa zao kwenye mfumo. Japo maswali yataphngua sio kama ya watakao hojiwa kwenye kaya binafsi
 
Faida ya kutofanya maamuzi kiweredi!...wangejiri makarani wengi..kupunguza siku na gharama( waliosoma project planning wataelewa namaanisha nn)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…