Makonda ajibu tuhuma za kumpiga risasi Tundu Lissu. Asema Lissu ana matatizo ya akili, aende Milembe

Makonda ajibu tuhuma za kumpiga risasi Tundu Lissu. Asema Lissu ana matatizo ya akili, aende Milembe

si kweli, Lisu naye ana watu wake ndani wanaompa habari

Lissu atakuwa amepewa habari nyingi, na watu wengi. Katika habari hizo zipo habari za kweli, na nyingine sio za kweli. Utetezi wa Makonda una mashiko kwasababu ameeleza jambo mahsusi alilokuwa akifanya siku ambayo Lissu alishambuliwa. Kinachotakiwa kufanyika ni Lissu kueleza ana ushahidi gani wa Makonda kuwepo Dodoma siku ya tukio. Baada ya hapo umma utaweza kujua nani anasema ukweli. Swali linabaki palepale: nani ndani ya serikali alihusika na shambulizi dhidi ya Tundu Lissu?
 
Anasema hataki kumjibu, wakati tayari ameishamjibu na kumtaja jina . Uungwana angekaa kimya. Kama kuna ya ndani zaidi wataanzia hapo alipojitetea nao kuonyesha wanayoyajua. Waungwana walisema kunyamaza ni jibu.
Mtu akupe tuhuma nzito kama hzo ukae kimya kwamba ndo uungwana.Lissu kama ana ushahidi auweke hadharani na wengine tumuamini tofauti na hapo namuona kama mtu mwenye msongo.
 
Mtu akupe tuhuma nzito kama hzo ukae kimya kwamba ndo uungwana.Lissu kama ana ushahidi auweke hadharani na wengine tumuamini tofauti na hapo namuona kama mtu mwenye msongo.
Yawezekana msongo kwa maoni yako yanayoheshimiwa. Lakini uko tayari kujibu maswali muhimu yote kwa niaba ya mkuu unayemtetea ? Kwa nini uling'oa CCTV camera zote ? Kwa nini mliondoa askari wote siku ya tukio. Kwa nini mlipiga marufuku watu kuvaa ti-shirts za sura yake Wala kumuombea,? Kwa nini mlimfuta ubunge eti ni mtoro wakati mnajua aliondoka Dodoma to Nairobi to Belgium akiwa hajitambui kwa risasi zenu,. Kwa nini zipo zaidi ya 10 na wengine wanaendelea ?
 
Hivi Makonda anafikiria kila mtu ni mjinga. Akae akijua wazi kwamba huenda ikawa TAL kajitokeza hadharani sababu anao ushahidi tosha wa tukio hilo. Labda Ushahidi huo utakuwa unamlenga mtuhumiwa bwana Makonda moja kwa moja. Huenda tutaona nani kati yao atakuwa mgonjwa wa akili.
Alipiga picha za serfie za ktosha on his way back to a monster city
 
naunga mkono hoja ya kwamba muungwana yafaa apite hospitali husika Dodoma akacheki, yawezekana utaratibu wake wa fikra umeshake kidogo, na ndiyo maana haelewani kabisa na hata na viongozi waandamizi ndani ya chama chake🐒
Mhhh,misimamo ya Lissu huwa haieleweki.kumbukeni enzi za kipindi cha je tutafika channel ten alivyokuwa anafunguka
 
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, leo akiwa anawasilisha ripoti yake ya miezi 6 ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Makoa ameamua kujibu mapigo.

Kama mtakumbuka, wiki chache nyuma Lissu alimtuhumu Makonda kuhusika na jaribio la kumuua lililofanyika mwaka 2017.

Akiongea na wanahabari leo, Makonda amekana kuwa hakuhusika na shambulio la Lissu na kuongeza kuwa Lissu kwa sasa anapitia msoto mkali sana wa kisiasa na anamtumia yeye kama ngazi ya kurudi kwenye siasa.

"Kaka angu Tundu Lissu nimemsikia hata mimi lakini kwa hali aliyonayo siwezi kumshangaa. Na nafarijika kuona kwamba ameniona nafaa kumsaidia kujenga career yake ya kisiasa kwenye taifa letu, Na mimi sitaki kumjibu kwa sababu nikimjibu ntamuaibisha kaka yangu yangu"

"Watu wa Clouds wakirudi nyuma siku ya tukio watakumbuka hata siku tukio linatokea mimi nilikuwa Dar Es Salaam uwanja wa mnazi mmoja tulikuwa na kampeni ya matibabu. Kwa hiyo hata sehemu ya tukio sikuwepo"

"Ushauri pekee ambao ningewapa nyie wanahabari, mjitahidi sana kuangalia mtu mnayemuhoji yupo katika wakati gani. Na kwa kuwa alisemea Dodoma nilitegemea mumuombe apite Milembe aone kama yuko sawa au"
Allah akbar
 
Mhhh,misimamo ya Lissu huwa haieleweki.kumbukeni enzi za kipindi cha je tutafika channel ten alivyokuwa anafunguka
watu wanafanya mzaha juu ya jambo hili, muungwana ana changamoto ndugu zangu..

kitakachoshangaza zaidi ni pale walio sawa kifikra pale chadema, kudhani wanapambana au kudeal na mtu ambae yuko fit kumbe changamoto.

Itakua hatari sana 🐒
 
Lissu atakuwa amepewa habari nyingi, na watu wengi. Katika habari hizo zipo habari za kweli, na nyingine sio za kweli. Utetezi wa Makonda una mashiko kwasababu ameeleza jambo mahsusi alilokuwa akifanya siku ambayo Lissu alishambuliwa. Kinachotakiwa kufanyika ni Lissu kueleza ana ushahidi gani wa Makonda kuwepo Dodoma siku ya tukio. Baada ya hapo umma utaweza kujua nani anasema ukweli. Swali linabaki palepale: nani ndani ya serikali alihusika na shambulizi dhidi ya Tundu Lissu?

Mkuu kwani kupanga shambulio ni lazima mastermind awepo eneo la tukio?
 
Back
Top Bottom