Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, leo akiwa anawasilisha ripoti yake ya miezi 6 ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Makoa ameamua kujibu mapigo.
Kama mtakumbuka, wiki chache nyuma Lissu alimtuhumu Makonda kuhusika na jaribio la kumuua lililofanyika mwaka 2017.
Akiongea na wanahabari leo, Makonda amekana kuwa hakuhusika na shambulio la Lissu na kuongeza kuwa Lissu kwa sasa anapitia msoto mkali sana wa kisiasa na anamtumia yeye kama ngazi ya kurudi kwenye siasa.
"Kaka angu Tundu Lissu nimemsikia hata mimi lakini kwa hali aliyonayo siwezi kumshangaa. Na nafarijika kuona kwamba ameniona nafaa kumsaidia kujenga career yake ya kisiasa kwenye taifa letu, Na mimi sitaki kumjibu kwa sababu nikimjibu ntamuaibisha kaka yangu yangu"
"Watu wa Clouds wakirudi nyuma siku ya tukio watakumbuka hata siku tukio linatokea mimi nilikuwa Dar Es Salaam uwanja wa mnazi mmoja tulikuwa na kampeni ya matibabu. Kwa hiyo hata sehemu ya tukio sikuwepo"
"Ushauri pekee ambao ningewapa nyie wanahabari, mjitahidi sana kuangalia mtu mnayemuhoji yupo katika wakati gani. Na kwa kuwa alisemea Dodoma nilitegemea mumuombe apite Milembe aone kama yuko sawa au"