Makonda ajibu tuhuma za kumpiga risasi Tundu Lissu. Asema Lissu ana matatizo ya akili, aende Milembe

Yawezekana msongo kwa maoni yako yanayoheshimiwa. Lakini uko tayari kujibu maswali muhimu yote kwa niaba ya mkuu unayemtetea ? Kwa nini uling'oa CCTV camera zote ? Kwa nini mliondoa askari wote siku ya tukio. Kwa nini mlipiga marufuku watu kuvaa ti-shirts za sura yake Wala kumuombea,? Kwa nini mlimfuta ubunge eti ni mtoro wakati mnajua aliondoka Dodoma to Nairobi to Belgium akiwa hajitambui kwa risasi zenu,. Kwa nini zipo zaidi ya 10 na wengine wanaendelea ?
Ila bro haupo sawa sasa hayo maswal kuulizwa makonda kama nani? Makonda alikua mwenyekiti wa ulinz na usalama DSM sio DODOMA. Makonda alikua hana uwezo wa kutoa amri yoyote DOM cz sio area yake ya jurisdiction. Unaweza ukawa una maswali mazuri ila Makonda hausiki na majibu ya hayo maswal hata kidogo
 
Lisu ana matatizo ya akili, aende Mioembe. Hili siyo tusi, ni sifa.
 
Ila bro haupo sawa sasa hayo maswal kuulizwa makonda kama nani? Makonda alikua mwenyekiti wa ulinz na usalama DSM sio DODOMA. Makonda alikua hana uwezo wa kutoa amri yoyote DOM cz sio area yake ya jurisdiction. Unaweza ukawa una maswali mazuri ila Makonda hausiki na majibu ya hayo maswal hata kidogo
Nakubali challenge. Kwa uono wako hafifu utadhani siko sawa. Maswali ya tukio hili yamekosa majibu kwa miaka 7 mpaka sasa. Pili, mtu anayekana hakuvamia clouds wakati CCTV camera ilionyesha tukio, muda na picha unamwamini vipi kwa kauli zake. Tatu nchi ya Marekani imewahi kuweka zuio la kuingia nchini humo kwa sababu huyu jamaa amewanyima watu haki ya kuishi,, mauaji,, (killing/asanitaion) amewahi kukanusha ? Natambua jambo hili uzito wake hata kulijadili ni humu. Lakini bado uhai hauna mbadala. Hatuna Tanzania nyingine. Be serious.
 
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, leo akiwa anawasilisha ripoti yake ya miezi 6 ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Makoa ameamua kujibu mapigo.

Kama mtakumbuka, wiki chache nyuma Lissu alimtuhumu Makonda kuhusika na jaribio la kumuua lililofanyika mwaka 2017.

Akiongea na wanahabari leo, Makonda amekana kuwa hakuhusika na shambulio la Lissu na kuongeza kuwa Lissu kwa sasa anapitia msoto mkali sana wa kisiasa na anamtumia yeye kama ngazi ya kurudi kwenye siasa.

"Kaka angu Tundu Lissu nimemsikia hata mimi lakini kwa hali aliyonayo siwezi kumshangaa. Na nafarijika kuona kwamba ameniona nafaa kumsaidia kujenga career yake ya kisiasa kwenye taifa letu, Na mimi sitaki kumjibu kwa sababu nikimjibu ntamuaibisha kaka yangu yangu"

"Watu wa Clouds wakirudi nyuma siku ya tukio watakumbuka hata siku tukio linatokea mimi nilikuwa Dar Es Salaam uwanja wa mnazi mmoja tulikuwa na kampeni ya matibabu. Kwa hiyo hata sehemu ya tukio sikuwepo"

"Ushauri pekee ambao ningewapa nyie wanahabari, mjitahidi sana kuangalia mtu mnayemuhoji yupo katika wakati gani. Na kwa kuwa alisemea Dodoma nilitegemea mumuombe apite Milembe aone kama yuko sawa au"

Jamaa muuaji na Lissu yuko sawa kwenye hili
 
Hata kulijadili ni humu na zito
 
Kwa kauli hizi inadhibitishabbl kuwa Huyu Dogo dogo shule hamna kabisa
Ni tz pekee watu kama Hawa wanaweza kuwa na vyeo vikubwa
 
Utetezi wake ulikuwa dhaifu na hapakuwa na waandishi makini. Yaani siku hiyo Lisu anapigwa risasi ni siku ambayo Hayati Magufuli alikuwa akipokea ripoti ya Vito, viongozi wote walipaswa kuwa pale. Ni kweli inaingia akilini Rais ana kikao muhimu tena kinarushwa live, eti mkuu wa mkoa ambao ni mwenyeji yuko mnazi mmoja na shughuli yake? Hapo ndipo alipochemkia sasa. Na kwa nini ahangaike kuwajibia polisi kwa hoja dhaifu namna Ile!!! Ningekuwa yeye ningenyamaza kimya. Mtu mbunge anashanbuliwa kwenye makazi ya viongozi halafu yeye ndiye akaripoti polisi,ili wafanye uchunguzi!!! Mbona mtu anashtakiwa akijaribu kujiua?
 
Angetueleza na lile la Marekani kumpiga marufuku kukanyaga huko kwa sababu alidhulumu haki za watu kuishi! Kama ni kweli au si kweli?
 
Ungenyamaza ndugu yangu, ungenyamaza mtani wangu. Wakati mwingine kunyamaza ni busara sana. Ni kuonesha una akili. Si wakati wote wa kuongea. Si wakati wote wa kujibu

Nyamaza.ni bora ukanyamaza ukasemekana hujui. Kuliko ukazungumza na kuthibitisha pasipo shaka kumbe ni kweli hujui. Ungenyamaza. Akili ya kuongea huna,akili na busara ya kujibu huna.

Kwa nini usingenyamaza? Unayakoroga maji yaliyotulia. Unayatindinganya. Maji yalianza kutulia. Unayatikisa tena. Why?kwa nini?
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
 
Attachments

  • IMG-20241117-WA0032.jpg
    IMG-20241117-WA0032.jpg
    118.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom