Makonda ajibu tuhuma za kumpiga risasi Tundu Lissu. Asema Lissu ana matatizo ya akili, aende Milembe

Serikali itupie jicho ufipa kabla hawajatoana macho
 
Attachments

  • IMG-20241117-WA0032.jpg
    IMG-20241117-WA0032.jpg
    118.5 KB · Views: 2
Huna akili maana haujui report ya makinikia ilipokelewa tarehe ngapi na Tundu Lissu alishambuliwa tarehe ngapi
 
Video ya tukio la Makonda siku aliyoshambuliwa Lissu iko mahali popote? Je, haiwezekani Makonda alikuwepo Dsm, halafu akapanda ndege kwenda Dodoma kuwahi shambulizi la Lissu?
 
hata mimi siku hizi simsikilizi Lissu na niliwahi kusema hivyo huko nyuma; ni mropokaji sana kama vile siyo mwana sheria. Wakati wa kesi kati ya Zito Kabwe na CHADEMA, Lissu aliongoza jopo la wanasheria wa CHADEMA wakati Zitto akiwakilishwa na wakili Albert Msonda peke yake, na CHADEMA ikapigwa chini
 
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, leo akiwa anawasilisha ripoti yake ya miezi 6 ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Makoa ameamua kujibu mapigo.

Kama mtakumbuka, wiki chache nyuma Lissu alimtuhumu Makonda kuhusika na jaribio la kumuua lililofanyika mwaka 2017.

Akiongea na wanahabari leo, Makonda amekana kuwa hakuhusika na shambulio la Lissu na kuongeza kuwa Lissu kwa sasa anapitia msoto mkali sana wa kisiasa na anamtumia yeye kama ngazi ya kurudi kwenye siasa.

"Kaka angu Tundu Lissu nimemsikia hata mimi lakini kwa hali aliyonayo siwezi kumshangaa. Na nafarijika kuona kwamba ameniona nafaa kumsaidia kujenga career yake ya kisiasa kwenye taifa letu, Na mimi sitaki kumjibu kwa sababu nikimjibu ntamuaibisha kaka yangu yangu"

"Watu wa Clouds wakirudi nyuma siku ya tukio watakumbuka hata siku tukio linatokea mimi nilikuwa Dar Es Salaam uwanja wa mnazi mmoja tulikuwa na kampeni ya matibabu. Kwa hiyo hata sehemu ya tukio sikuwepo"

"Ushauri pekee ambao ningewapa nyie wanahabari, mjitahidi sana kuangalia mtu mnayemuhoji yupo katika wakati gani. Na kwa kuwa alisemea Dodoma nilitegemea mumuombe apite Milembe aone kama yuko sawa au"
Kipindi hicho alikuwa na bifu na marehemu ruge mutahaba.
Yeye ndio ana matatizo ndio maana anapita kila kanisa anataka aombewe.
●Akiona mtu kabeba biblia anamkimbilia amuombee
●Akiona mtu kavaa kanzu +barakashia anampigia magoti kuomba aombewe.
●Amewanafikia Nape na Makamba
●Huyu mtu ni mfitini sana.
 
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, leo akiwa anawasilisha ripoti yake ya miezi 6 ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Makoa ameamua kujibu mapigo.

Kama mtakumbuka, wiki chache nyuma Lissu alimtuhumu Makonda kuhusika na jaribio la kumuua lililofanyika mwaka 2017.

Akiongea na wanahabari leo, Makonda amekana kuwa hakuhusika na shambulio la Lissu na kuongeza kuwa Lissu kwa sasa anapitia msoto mkali sana wa kisiasa na anamtumia yeye kama ngazi ya kurudi kwenye siasa.

"Kaka angu Tundu Lissu nimemsikia hata mimi lakini kwa hali aliyonayo siwezi kumshangaa. Na nafarijika kuona kwamba ameniona nafaa kumsaidia kujenga career yake ya kisiasa kwenye taifa letu, Na mimi sitaki kumjibu kwa sababu nikimjibu ntamuaibisha kaka yangu yangu"

"Watu wa Clouds wakirudi nyuma siku ya tukio watakumbuka hata siku tukio linatokea mimi nilikuwa Dar Es Salaam uwanja wa mnazi mmoja tulikuwa na kampeni ya matibabu. Kwa hiyo hata sehemu ya tukio sikuwepo"

"Ushauri pekee ambao ningewapa nyie wanahabari, mjitahidi sana kuangalia mtu mnayemuhoji yupo katika wakati gani. Na kwa kuwa alisemea Dodoma nilitegemea mumuombe apite Milembe aone kama yuko sawa au"
Hapa amepiga “fix” yaan magu awepo ikulu na kupoea maripot yeye awe anamipango mingine.
 
Ungenyamaza ndugu yangu, ungenyamaza mtani wangu. Wakati mwingine kunyamaza ni busara sana. Ni kuonesha una akili. Si wakati wote wa kuongea. Si wakati wote wa kujibu

Nyamaza.ni bora ukanyamaza ukasemekana hujui. Kuliko ukazungumza na kuthibitisha pasipo shaka kumbe ni kweli hujui. Ungenyamaza. Akili ya kuongea huna,akili na busara ya kujibu huna.

Kwa nini usingenyamaza? Unayakoroga maji yaliyotulia. Unayatindinganya. Maji yalianza kutulia. Unayatikisa tena. Why?kwa nini?
 
Back
Top Bottom