Makonda anadai tarehe 7 SEPT 2017 hakuwepo Dodoma, alikuwa Dar Es Salaam. Sasa inabidi tupate majibu yasiyo na shaka kama ni kweli, au uongo.
Akosokekane Ikulu iliyo ndani ya mkoa wake ambako boss wake (Rais wake) alikuwa na shughuli maalumu ile ya kupokea ripoti ya makinikia...?
Hivi wewe unadhani ni shughuli gani ambayo ni muhimu zaidi ambayo RC wa DSM siku hiyo alikuwa anaifanya ndani ya mkoa wake huku aliyempa huo u - RC akiwa na kazi maalumu na muhimu ndani ya mkoa wake siku hiyohiyo huku viongozi wote muhimu wa kitaifa Jaji Mkuu, Spika wa Bunge, IGP, CDF, mawaziri, ma - DCs na ma - RCs wa mikoa mingine wakiwa pale...?
Hivi mnawezaje kudanganywa na kudanganyika kirahisi hivi na mtu huyu asiye na utu wala akili kabisa ya kuongea uongo huu huku dunia nzima ikimtazama..??
Makonda anaweza kuwa amehusika, lakini sio lazima kwamba alikuwepo Dodoma. Pia Makonda anaweza kuwa alikuwepo na hakuhusika. Na anaweza kuwa alikuwepo Dodoma, na alihusika...
Haya ni mawazo yako na ni mtazamo wako...
Lakini, jaribu kutumia circumstancial evidences na mlolongo wa matukio mabaya kumhusu kisha umpe hukumu yake..
Rafiki
bangusule, ushahidi wa kimazingira kwa tukio hili, unamfunga na kumlalia huyu jamaa kila kona. Ni bora angekaa kimya kama alivyokuwa ameamua kukaa kimya kuliko kupanua mdomo wake kujitetea kwa uzushi na uongo...!
Vilevile Makonda anaweza kuwa alikuwa Dar Es Salaam, ktk shughuli zake kama RC,
Ndugu, are you really thinking straight kweli...?
Aalikwe wapi na nani siku hiyo wakati boss wake Rais alikuwa na shughuli maalumu Ikulu ndani ya mkoa wake na viongozi karibu wote na baadhi ya RCs wenzake wakiwa wako pale..?
Mwaliko wowote kiprotokali kwa siku hiyo ulikuwa uwe surpassed na tukio la ikulu alikokuwa boss wake akifanya kazi hiyo muhimu ya kitaifa.....
Nakushauri tu kuwa, fikiri vizuri na kamwe usikubali kudanganyika na uongo huu toka kwa mtu huyu ambaye ameshakomaa kutenda uovu kwa kutumia madaraka yake vibaya (abuse of power) kwa kiasi cha kuwa sugu na kukosa hata tone la aibu..!
na baadae akapanda ndege kwenda Dodoma kuwahi "shughuli" ya Tundu Lissu.
Haa haa😁😁😁..
Sasa hapa umesema ukweli wako. Hata hivyo aliwahi tukio la Tundu Lissu wapi? Akiwa hospitalini au asubuhi kabla hajapigwa risasi? Funguka tukuelewe...
KInachotakiwa ni ushahidi usiokuwa na mashaka.
Kwanini msingemwambia awaoneshe hiyo tiketi ya ndege aliyopanda siku hiyo wakati mnamuuliza mawali huko Arusha leo? Na alipanda ndege ya shirika gani, ATCL au Precision ili tukafukue kwenye data base..?