Makonda ajibu tuhuma za kumpiga risasi Tundu Lissu. Asema Lissu ana matatizo ya akili, aende Milembe

Makonda ajibu tuhuma za kumpiga risasi Tundu Lissu. Asema Lissu ana matatizo ya akili, aende Milembe

naunga mkono hoja ya kwamba muungwana yafaa apite hospitali husika Dodoma akacheki, yawezekana utaratibu wake wa fikra umeshake kidogo, na ndiyo maana haelewani kabisa na hata na viongozi waandamizi ndani ya chama chake🐒

You think is stupid like the guy? Hivi milembe ni sawa na Mirembe?
 
Makonda ni Bora akae kimya tu kwasababu unaweza kushiriki kupanga tukio na wewe ukawa eneo jingine lakini mpangaji mkuu wa tukio ukawa ni wewe, sio lazima kwamba ili uwe umeshiriki ni mpaka uwepo mwenyewe eneo la tukio, wa Tanzania sio wajinga kiivyo izo mambo tunazijua sana!
🎯👏👏👍
 
Mbona mnafikiri kama watoto wadogo vile ambao hata chekechea hawajafika...?

Ni huyu huyu muhusika kwa maagizo ya boss wake aliyekuwa Rais hayati John P. Magufuli...!

Ushahidi ni mlolongo wa matukio yasiyo ya kiungwana wala kubeba utu wa binadamu aliyotendewa victim (Tundu Lissu) na serikali ya Rais Magufuli (mtuhumiwa namba 1) wa unyama huo...

Aidha wote tunajua kuwa huyu jamaa (Paul Makonda) ndiye alikuwa "toto pendwa" wa Mwendazake na ndiye alikuwa anatumiwa kwenye kazi chafu chafu za viongozi wa serikali akiwemo Rais Magufuli...

Siku hiyo tukio hili linstokea, ndani ya mkoa wake (akiwa RC - DSM), kulikuwa na tukio Ikulu ya Rais kupokea taarifa/ripoti ya makinikia ya almasi. Ilikuwa ni ajabu "toto pendwa" huyu kutoonekana kwenye tukio hilo. Kumbe alikuwa Dodoma akiongoza kikosi cha mauaji ya Tundu Lissu bwana😕😕😕!!!!

Sasa angalia mlolongo wa matukio ya ushahidi wa kimazingira kuonesha uhusika wake na Rais wake (Mwendazake Magufuli...)👇🏻👇🏻👇🏻

1. Kauli za Hayati Rais John P. Magufuli mwenyewe kuwa "....Watu wote wanaoipinga serikali wakati ikiwa ktk vita ya kiuchumi, nyie askari mnajua huwa wanafanywa nini. Obviously, hawastahili kuishi...." Dakika chache baada ya kauli siku hiyo tarehe 7/9/2024, Dodoma eneo la AREA D, makazi ya viongozi, jamaa akamwagiwa risasi zaidi 37 akiwa ndani ya gari lake...

2. Eneo hilo la makazi ya viongozi ambalo huwa na ulinzi 7days & 24hrs mwaka mzima, siku hiyo na muda wa tukio hilo hakukuwa na mlinzi hata mmoja kwenye mageti yote..!

Swali rahisi tu ni hili: Hivi ni nani mwenye nguvu za kimsmlaka na uwezo wa kuondoa walinzi (askari polisi wote) kwenye lindo lao siku hiyo..???? Akili kichwani mwako...

3. Jengo - Apartment aliyokuwa akiishi Tundu Lissu alikuwa akiishi pia Waziri wa Nishati na Madini by then Meadard Kalemani na Waziri wa Afya (by then) Dr Haji Mponda. Aidha apartment hiyo ilikuwa na CCTV Cameras. Baada ya tukio, polisi walizichukua na mpaka leo polisi wanazo na hawataki kusema waliona nini...!!

4. Kunyimwa stahili na haki zake za matibabu huku akiwa mtumishi wa umma (mbunge....)

5. Kuvuliwa ubunge wake kwa sababu eti ni "mtoro kazini, hajulikani aliko..."

6. Job Ndugai (Spika wa Bunge by then) aliamuriwa na Rais Magufuli kuwa, akifa hata asiingizwe kwenye jengo la Bunge kuagwa na wenzake na badala yake maiti usiku kwa usiku ipelekwe kijijini kwao Singida na kuzikwa. ..

Duuh, hiyo ☝🏻☝🏻☝🏻 ni chuki na unyama uliopitiliza viwango vya shetani mwenyewe...!!

7. Wananchi kuzuiliwa na kupigwa marufuku na serikali ya CCM chini ya Hayati John P. Magufuli ku - sympathize na victim, familia yake, ndugu zake, wanachama na chama chake, mashabiki na wapenzi wake (kina sisi) hadharani kuvaa t-shirt za "GET WELL TUNDU LISSU", kufanya maombi kwenye viwanja vya wazi, kuchangia fedha za matibabu nk. Waliofanya haya, basi ilikuwa ni kwa kificho sana....

8. Wabunge wa CCM kupigwa marufuku na serikali na chama chao kwenda kumuona na kumsalimu hospitalini Nairobi na Ubelgiji. Waliofanikiwa kwenda ni kwa kuwa walikuwa na roho ngumu tu na badae baadhi walitoka CCM e.g Lazaro Nyalandu...

9 Funga kazi ni DRAMA za serikali kupitia Jeshi la Polisi, kukataa kutenda wajibu wao wa kuchunguza tukio hili la kihalifu (political attempted assassination) kwa vusingizio vya mara dereva kakimbia, mara Tundu Lissu mwenye kakimbia na hataki kutoa ushirikiano na ujinga mwingine mwingi kuanzia polisi wenyewe, Rais, mawaziri, bunge na,mamlaka zingine...

##Mpaka hapo na kwa circumstantial evidences hizi tunakosaje kuwajua wahusika? Na serikali ni kwanini ilikuwa inataka kumuua Tundu Lissu kijinga na kishamba kiasi hiki..??

Makonda anadai tarehe 7 SEPT 2017 hakuwepo Dodoma, alikuwa Dar Es Salaam. Sasa inabidi tupate majibu yasiyo na shaka kama ni kweli, au uongo.

Makonda anaweza kuwa amehusika, lakini sio lazima kwamba alikuwepo Dodoma. Pia Makonda anaweza kuwa alikuwepo na hakuhusika. Na anaweza kuwa alikuwepo Dodoma, na alihusika.

Vilevile Makonda anaweza kuwa alikuwa Dar Es Salaam, ktk shughuli zake kama RC, na baadae akapanda ndege kwenda Dodoma kuwahi "shughuli" ya Tundu Lissu. KInachotakiwa ni ushahidi usiokuwa na mashaka.
 
Anasema hataki kumjibu, wakati tayari ameishamjibu na kumtaja jina . Uungwana angekaa kimya. Kama kuna ya ndani zaidi wataanzia hapo alipojitetea nao kuonyesha wanayoyajua. Waungwana walisema kunyamaza ni jibu.
Mimi nafikiri Watanzania wanaomuamini huyu Zerobrain BASHITE ndiyo wapumbavu. Waache waendelee kutumika. Mtu aliyeshindwa hata kupata D mbili kwenye NECTA hawezi kuwa na fikra chanya. Ukiangalia tu sura ya Bashite na alivyojaza msambwanda hakuna namna anaweza kuwa na akili kichwani
 
Makonda anadai tarehe 7 SEPT 2017 hakuwepo Dodoma, alikuwa Dar Es Salaam. Sasa inabidi tupate majibu yasiyo na shaka kama ni kweli, au uongo.

Makonda anaweza kuwa amehusika, lakini sio lazima kwamba alikuwepo Dodoma. Pia Makonda anaweza kuwa alikuwepo na hakuhusika. Na anaweza kuwa alikuwepo Dodoma, na alihusika.

Vilevile Makonda anaweza kuwa alikuwa Dar Es Salaam, ktk shughuli zake kama RC, na baadae akapanda ndege kwenda Dodoma kuwahi "shughuli" ya Tundu Lissu. KInachotakiwa ni ushahidi usiokuwa na mashaka.

Hope atakuwa na majibu kwenye court of law kwa sasa ataspin tu kama kawaida!
 
Nyie kweli ni Viongozi wa uma gentleman 🐒
Ndrugu zango,
sio kwa ubaya Lakini...

kibaraka ana mental issues ni muhimu akapata usaidizi mapema. Atashambuliwa na kuumizwa na waandamizi wenzake wakidhani yuko fit kumbe mungwana na anapitia mental instability 🐒
 
Mtu akupe tuhuma nzito kama hzo ukae kimya kwamba ndo uungwana.Lissu kama ana ushahidi auweke hadharani na wengine tumuamini tofauti na hapo namuona kama mtu mwenye msongo.

Makonda anaweza kuwa alikuwa Dsm, halafu akapanda ndege kwenda Dodoma kuwahi "shughuli" ya Tundu Lissu. Majibu yake sio ya uhakika kwa asilimia 100%.
 
Hahaah ndio makonda asuggest medical care? Anyway tulisharusu nchi kuongozwa na mediocre hamna namna tunasoma na kuchitchat hapa siku ziende tu
nadhani hata mabwenyenye wanaomfadhili huko magharibi, wanaweza kushughulika nae coz baadae inaweza kua mbaya na mzigo mkubwa zaidi gentleman, kwa maoni yangu Lakini 🐒
 
naunga mkono hoja ya kwamba muungwana yafaa apite hospitali husika Dodoma akacheki, yawezekana utaratibu wake wa fikra umeshake kidogo, na ndiyo maana haelewani kabisa na hata na viongozi waandamizi ndani ya chama chake🐒
Mkuu hapo umeharibu kabisa umahiri wako wa thread. Nakushauri usijihusishe na kumfagilia Bashite. Bashite ananuka damu za watu wasio na hatia aliowaua kwa kutumwa na Magufuli. Huyu ni mhalifu mwenye bahati tu.

Lakini iko siku atakuja kujibu tuhuma za mauaji, utekaji na uvamizi wa kutumia silaha. Hii ni pamoja na unyang"anyi wa mali binafsi za wafanyabiashara
 
Nasubiri awajibu na Wamarekani waliomkataza kwenda nchini kwao...
Ameshawajibu.
Amesema walimzuia kwenda marekani kwasababu alipinga ushoga. Pia ameongeza kwamba marekani sio mbinguni sio lazima kwenda.
 
nadhani hata mabwenyenye wanaomfadhili huko magharibi, wanaweza kushughulika nae coz baadae inaweza kua mbaya na mzigo mkubwa zaidi gentleman, kwa maoni yangu Lakini 🐒

Mama yetu pia si kaenda kwa mabwanyenye haohao leo? Au hao wengine hawezi kushughulika na mama yetu kwa kuwa kuna chawa nyuma yake? Wakimfadhili mama ni partners wakifadhili usiowapenda ni bwanyenye?
 
Wewe Bashite ambaye jimbo tu moja la Uchaguzi uliangushwa unajilinganisha na mtu ambaye alipata kura 1.6M( kwa mujibu wa NEC yenu)..you are not serious
 
Mkuu hapo umeharibu kabisa umahiri wako wa thread. Nakushauri usijihusishe na kumfagilia Bashite. Bashite ananuka damu za watu wasio na hatia aliowaua kwa kutumwa na Magufuli. Huyu ni mhalifu mwenye bahati tu.

Lakini iko siku atakuja kujibu tuhuma za mauaji, utekaji na uvamizi wa kutumia silaha. Hii ni pamoja na unyang"anyi wa mali binafsi za wafanyabiashara
hayo mengine yote umesema sina hakika na kwahivyo sina haki hata ya kueleza au kushauri chochote...

Ila kwa mawaidha yake dhidi ya huyo mungwana kiongozi msaidizi wa Chadema Taifa, ambae tunaheshimiana sana, kwakweli na naunga mkono mawaidha ya RC, bila haya, wala aibu kwamba yafaa na yatakikana kiongozi huyo muandamizi wa Chadema akachunguzwe hiyo habari muhimu sana.

Fikra kua na afya ndiyo kila kitu kwa binadamu, ndrugu zango,
Ikianza kuharibika hiyo inakua ndiyo basi tena. Dalili zisizo za kitabibu ziko wazi kabisa ndrugo zango wadau 🐒
 
Watu wako bize wanafatilia upkoaji kko

Ova
 
Back
Top Bottom