Makonda anaeneza ukabila? Ni nini kinamfanya aongee kisukuma huko usukumani?

saigilomagema

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2015
Posts
4,683
Reaction score
7,222
Hii tabia ya kuongea kisukuma akiwa mikoa ya wasukuma ni hatari, ni kueneza ukabila. Kwani watanzania wengine hawana lugha yao? Kwanini wasikitumie? Samia unatengeneza bomu. Hilo jamaa halifai anapsua nchi.

Kisukuma kilivyo kibaya mi ningeona aibu kukitumia tena karne hii.
 
Kwa misingi hiyo hata kuzungumza Kizungu itakuwa hatari kwa Usalama wa Taifa. na Ushahidi upo kwamba Lugha hiyo imegawa Taifa

Ukizingatia watanzania wana lugha yao ya Kiswahili.
 
Hapa tusiweke ukabila kwenye uongozi. Kikubwa tuangalie uwezo wa mtu. Wasukuma walishaongoza nchi na wameonyesha uwezo wao. Wazanaki walishafanya hivyo pia
 
Wewe ongea nawe kisandawe Kwan umezuiliwa

Anyway masuala ya ukabila ni kama unatembea juu ya mayai lazima yapasuke

Achana na kupondea kabila za watu
 
Na wewe kaongee kipare kule Machame
 
..siku mwanasiasa Mchagga akiongea lugha yao jukwaani utasikia makelele na matusi atakayorushiwa. Lakini wale wa "kabila kubwa" kuongea kilugha ruksa.
 
Mimi Naweza kusema sikubalini na Makonda ila kwa hili kaka Sikubaliani na wewe 100%..

Ulitaka aende Usukumani akaongee Kigogo?
Au aende akaongee kidigo au Kibondei au akaongee Kichaga?

Chuki zisizo na sababu Mpaka kwenye mambo ambayo hayapaswi chuki haya ni matumizi mabaya ya chuki..
Au unataka kuwa kama Lucas mwashambwa ambavyo anamchukia Mbowe?
 
Kufa maana wasukuma ndiyo waamuzi nani awe rais
 
Huu uhuru wa Kuongea sasa unavuka mipaka.

Ma moderators wamejishibia matoke wanashindwa kudadavua nini kinafaa kuwekwa Jamvini.

Uzi huu ni dhahiri wamelala, na hawafanyi kazi zao na kwa sababu za chuki zao za kikabila wameuacha uzi huu ubandikwe.

Moderators ndio defense ya kwanza, katika kukomesha Ukabila kushamiri Tanzania. Wameshindwa.!

Hii gia ya Uhuru wa kuongea ndio utakuja kitumaliza Watanzania. Shame on you.
 

Wewe kama hata kilugha chako hukijui,acha wivu wa kike na wewe kaongee lugha yako kwani umekatazwa
 
Mimi simchukii Mbowe na wala sijawahi kusema namchukia
 
Ulitaka aongee kisukuma akiwa Unyakyusani Mbeya?
 

Ubaya wa kisukuma ni kitu gani ?? kama huelewi si ingia google tu , mwangaluka 😛😛
 
This is clearly a form of hate speech and not free speech. Inashangaza sana.

It is a biased and hateful opinion(well huyu saigilo amejivua akili tu) that could potentially incite hatred and violance against Wasukuma people let alone the offices of Jamiiforums!

Yes, we can argue its a form of free speech, but when it is based on bias and hatred and incites violance amongst Tanzanians against Tanzanians, it becomes a hate speech.

Maxence Melo I am dismayed at seeing such a statement on your forum Ndugu. I know it is important to respect free speech, but also to prevent and condemn any form of discrimination, intolerance, or extremism. I appreciate all you do but this is crossing the line. Kama ni free speech basi muachie nyuzi zitakazo sema mpigwe na mayai viza popote mlipo.

Moderators mjitathmini.
 
Ukiusoma huu uzi kwa umakini utagundua kua mleta mada ndio ana chuki ya ukabila na ubaguzi wa ukabila tribalism,

Amemkosoa makonda kisha hapo hapo yeye mwenyewe amewadhihaki wasukuma na kuwaita washamba kisha akasema kisukuma ni kibaya.

..mtoa mada ana matatizo yake, lakini ukweli utabaki kwamba sio sahihi kwa kiongozi wa chama cha siasa kwenda kanda alikotokea na kuanza kuzungumza kilugha.

..tunaweza kujenga utamaduni mbaya wa wanasiasa kuzungumza kikwao wakati tulishaachana na mambo hayo.

..mtakumbuka jinsi wanasiasa walivyotuletea salamu za kidini ktk shughuli za serikali. Hiki anachokifanya Makonda msije mkashangaa kinazaa utamaduni mpya ikiwa tutakiendekeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…