Makonda: Ghalib usinilazimishe kusema uozo wako, achia mali yangu. Walioko nyuma yako nawajua

Mimi sijali kama huyo GSM ni msafi au sio msafi .. ninachotaka ni makonda alipe kwa ushenzi aliofanya.. kuanzia kumpiga kofi mzee wetu Walioba hadi kuvamia studio za Clouds..

Hata kama atalipa kwa kosa ambalo hajafanya lakini alipe tu. Ili iwe fundisho kwa watu waliopo kwenye uongozi au watakaokuja kupata uongoz kwamba ukiwa kiongozi sio kwamba una akili kuliko wote unaowaongoza
Hivi huyu Makondakta si ndio alikuwa chawa wa Riz1 na hao Danube au wapo wawili tofauti?
 
Jamaa anajambia mbali halafu bado anaonekana kujisaha na huo uccm kwa ufupi wanaokupa kichwa ndio hao hao wanapanga kukuangusha bro ningekuwa mimi ndio wewe tangu Magu alivyodanja tu ningeuza kila kitu nikatimkia zangu canada kuomba hifadhi.
canada tena wakati alipigwa pini na Pompeo
 
Kwa sasa makonda ni ‘joka la kibisa’ lisilo kuwa na meno, ajiandae GSM kalianzisha wafanya biashara wengi wanakuja kummaliza
 
View attachment 2148028
Wakati Wakili wa mfanyabiashara maarufu nchini, Ghalib Said Mohamed (GSM), Alex Mgongolwa ameweka wazi vielelezo vya umiliki wa eneo kiwanja namba 60 lililopo Regent Estate Kinondoni jijini hapa, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemtaka mfanyabiashara huyo kumwachia mali yake.

Mzozo wa kiwanja hicho umeibuka hivi karibuni, ambapo Makonda ameonekana katika video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii akisisitiza kuwa eneo hilo ni lake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Machi 12, 2022 jijini hapa Wakili Mgongolwa amemtaka mtu ambaye hakumtaja kwa jina, kuweka wazi vielelezo alivyonavyo vya umiliki wa eneo hilo na vielelezo kutoka Wizara ya Ardhi vinavyompa uhalali wa kulimiliki.

Hata hivyo, Makonda alipotafutwa kwa simu leo, amejibu kwa ujumbe wa WhatsApp, akisema; “GSM usinilazimishe kusema uozo wako achia mali yangu. Walioko nyuma yako nawajua.”

Kama hiyo haitoshi, katika ukurasa wake wa Instagram, Makonda aliweka video ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka ambayo pamoja na mengine alieleza haja ya kutaka Jeshi la Polisi kuchunguzwa, kisha akaweka ujumbe:

“Naunga mkono hoja ya Kamati Kuu, ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi, wanaolipaka tope Jeshi la Jolisi kwa kuwalinda wafanyabiashara MATAPELI wanaodhulumu mali za watu. Naomba tuanze na Dar es salaam na mimi Paul Makonda niko tayari kutoa ushirikianao.”

Madai ya GSM
Akifafanua zaidi kuhusu umiliki wa ardhi hiyo, Wakili Mgongolwa amesema, mteja wake Ghalib Said Mohamed alinunua ardhi wilaya ya Kinondoni, eneo la Regent Estate plot no. 60, title no. 186153/60, kwa lengo la ujenzi wa makazi Novemba 21, 2006."

Vilevile, Mgongolwa amesema Septemba 2017, mteja wake aliingia mkataba na kampuni ya ujenzi iitwayo Group Six International (Contract Class One) kwa ajili ya ujenzi wa eneo hilo wenye thamani ya Sh640 milioni.

"Ghalib aliomba kibali cha ujenzi na manispaa ya Kinondoni walitoa kibali hicho Oktoba 16, 2017 chenye kumbukumbu namba 00020032 kwa Ghalib Said Mohammed kwa ajili ya ujenzi eneo hilo," amesema.

Ameongeza kuwa baada ya kibali hicho kutoka, Group Six walianza ujenzi na walipeleka malipo ya awali ya ujenzi Januari 31, 2018 huku mteja wake huyo akitekeleza sehemu ya mkataba kwa kulipa kiasi cha Sh51.92 milioni, malipo ambayo yana kithibitisho kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kuhusu mteja wake kuwa na uhusiano wa karibu na mlalamikaji, alisema, "mteja wangu na mtu ambaye kwenye mitandao amekuwa akizungumza kwamba anamiliki eneo hilo, mteja wangu katika kipindi anachozungumza huyo mtu cha mwaka 2012 alikuwa hamfahamu kabisa huyo mtu."

"Mimi leo nathibitisha uhalali wa miliki, unaweza ukawa na uhusiano na mtu lakini sio wa kibiashara wa kuuziana na kuhamishiana miliki licha ya kuingia katika makubaliano ya kuhamishiana miliki,"

Mgongolwa alisema kufahamiana na mtu ni jambo lingine na miliki ni jambo lingine, hivyo ushahidi wa vielelezo kisheria unakingwa na vielelezo hivyo, ambaye anasema ni eneo lake aweke wazi vielelezo vya kisheria.

"Tunatoa changamoto kwa mtu yoyote yule aje akinzane na vielelezo vyetu, huu ni ujenzi kwa mujibu wa mkataba na haujasimamiwa na mjomba au shangazi," amesema Mgongolwa.

Alisema yeye yuko radhi kumsikiliza ili wakapambane, alisema kama kuna mtu anadhani anayo haki katika umiliki huo, lakini kwa sasa hawatafanya chochote na endapo ataendelea na matukio hayo hivyo basi ngazi za kisheria zitafuatwa.

"Hata tunaondokana na hisia tunaenda na uhalisia, yoyote yule anayesema aridhi ni ya kwake iwe kimahusiano au lah, aje na vielelezo kwetu, mtu mwenye dhana tofauti milango ya kimahakama iko wazi, ila kwa sasa hawatakwenda mahakamani," amesema Mgongolwa na kuongeza kuwa wajibu wangu kama mwanasheria ni kuthibitisha umiliki halali kwa mteja wangu.

"Hatua tutakazozichukua kuanzia sasa itategemea na matukio ambayo yatafuata kwani ndiyo yatatupa mwongozo wa nini tukifanye, ikitokea hatua ya kwenda mahakamani tutakwenda, ikitokea kuangalia ngazi nyingine tutalipeleka kwa kuwa maelekezo yetu yako wazi tunatakiwa kulinda haki ya teja wetu sambamba na jina lake," amesema.

Source: Mwananchi
Sasa mbona mnatunziana uozo??
 
Wanaume wanajipigia pasi tu. Anatulizwa kifuani, anabinywa, anapewa mwanaume mwengine. Makonda alikua mtu flani wa Cheo, ila zaidi hakuweza kukaa na hawa mamafia. Hawa GSM ndio walimpa ujeuri, sasa anataka kushindana na wanaume. Wale GSM, GHARIB YULE SALAAH na Vichwa vingi sana vinavyowazunguka ni wajeuri. Hata mama Samia anajua hiki kikosi, hadi watoto wao mama samia anajua, hawa ni Miamba. Wamejitengeneza.
 
Kwenye hili sakata la aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar na GSM yataibuka mengi Leo Makonda katishia kusema maovu ya GSM hii inaonesha wazi kuwa wote Wawili ni Matapeli wanajuana jinsi walivuokubaliana kufanya maovu yao.
Huenda GSM anafanya biashara za magendo ambazo Makonda anazijua ila alikuwa kamfichia madhambi yake. Acheni vyuma viumane[emoji23][emoji23][emoji23]
Sasa hapo nani ni bwege?yaani ulikuwa mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa mkoa, leo hii unaanza kutoa tuhuma kama mlina ulanzi?!!kama anafanya biashara hizo yeye kama kiongozi wa mkoa, alichukua hatua gani!!yaani kama mkubwa akimuacha makonda , ili sheria ichukue mkondo wake, ya jambazi sabaya yatakuwa na nafuu!!sasa hata akiyasema kwa sasa hayatakuwa na nguvu sana kwani itonekana hakuwa na nia njema na taifa, kwani hadi maslahi yake yameguswa ndio amesikia uchungu huo?!!!serikali ile ilikuwa imejaa genge la wahuni tu,
 
Makonda alikuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ambao GSM anafanya biashara kama leo makonda atasema GSM anafanya maovu wakati alishawahi kuwa mkuu wa ulinzi katika mkoa huu na hakumchukulia hatua itakuwa anajifedhehesha mwenyewe
Hakuweza kimuajibisha pale alipokuwa na nguvu hivyo ni bora akae kimya
Makonda kichwa panzi hajui hata miiko ya kazi aliyokuwa nayo
 
Kwenye hili sakata la aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar na GSM yataibuka mengi Leo Makonda katishia kusema maovu ya GSM hii inaonesha wazi kuwa wote Wawili ni Matapeli wanajuana jinsi walivuokubaliana kufanya maovu yao.
Huenda GSM anafanya biashara za magendo ambazo Makonda anazijua ila alikuwa kamfichia madhambi yake. Acheni vyuma viumane[emoji23][emoji23][emoji23]

Je, Makonda akiwa kama kiongozi wa mkoa na mwenyekiti wa usalama mkoa wa Dar kwa wakati huo, kuna hatua au jitihada zozote za kuzuia hayo maovu alifanya?
 
Hivi ule msikiti walipkuwa wanaujenga kwa pamoja ulikamilika?
 
Inaonesha kuwa hayo mabaya anayoyajua dhidi ya GSM ndio alitaka kuyatumia kum black mail ili amjengee nyumba ... kwa mamlaka aliyokuwa nayo kwanini hakumuwajibisha GSM?
very possible. unamkuta mtu ana kilema afu unakishikilia icho icho anakuwa mtumwa wako afanye chochote unachotaka akifanye. yule mtumwa huwa anafanya kujisafisha na kuondoa ushahidi wa kilema kile kwa siri bila wewe kujua akimaliza kujiimarisha anakuzingua na hauna ushahidi wa kilema kile.
 
Makontena ya furniture za walimu yalikua na nani nyuma yake? Usijitoe kuwa nyuma ya ghalib,tambua sasa huwezi mpigia mambosasa wala ikulu wacha dawa ikuingie

Sent from my TECNO S1 using JamiiForums mobile app
 
View attachment 2148028
Wakati Wakili wa mfanyabiashara maarufu nchini, Ghalib Said Mohamed (GSM), Alex Mgongolwa ameweka wazi vielelezo vya umiliki wa eneo kiwanja namba 60 lililopo Regent Estate Kinondoni jijini hapa, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemtaka mfanyabiashara huyo kumwachia mali yake.

Mzozo wa kiwanja hicho umeibuka hivi karibuni, ambapo Makonda ameonekana katika video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii akisisitiza kuwa eneo hilo ni lake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Machi 12, 2022 jijini hapa Wakili Mgongolwa amemtaka mtu ambaye hakumtaja kwa jina, kuweka wazi vielelezo alivyonavyo vya umiliki wa eneo hilo na vielelezo kutoka Wizara ya Ardhi vinavyompa uhalali wa kulimiliki.

Hata hivyo, Makonda alipotafutwa kwa simu leo, amejibu kwa ujumbe wa WhatsApp, akisema; “GSM usinilazimishe kusema uozo wako achia mali yangu. Walioko nyuma yako nawajua.”

Kama hiyo haitoshi, katika ukurasa wake wa Instagram, Makonda aliweka video ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka ambayo pamoja na mengine alieleza haja ya kutaka Jeshi la Polisi kuchunguzwa, kisha akaweka ujumbe:

“Naunga mkono hoja ya Kamati Kuu, ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi, wanaolipaka tope Jeshi la Jolisi kwa kuwalinda wafanyabiashara MATAPELI wanaodhulumu mali za watu. Naomba tuanze na Dar es salaam na mimi Paul Makonda niko tayari kutoa ushirikianao.”

Madai ya GSM
Akifafanua zaidi kuhusu umiliki wa ardhi hiyo, Wakili Mgongolwa amesema, mteja wake Ghalib Said Mohamed alinunua ardhi wilaya ya Kinondoni, eneo la Regent Estate plot no. 60, title no. 186153/60, kwa lengo la ujenzi wa makazi Novemba 21, 2006."

Vilevile, Mgongolwa amesema Septemba 2017, mteja wake aliingia mkataba na kampuni ya ujenzi iitwayo Group Six International (Contract Class One) kwa ajili ya ujenzi wa eneo hilo wenye thamani ya Sh640 milioni.

"Ghalib aliomba kibali cha ujenzi na manispaa ya Kinondoni walitoa kibali hicho Oktoba 16, 2017 chenye kumbukumbu namba 00020032 kwa Ghalib Said Mohammed kwa ajili ya ujenzi eneo hilo," amesema.

Ameongeza kuwa baada ya kibali hicho kutoka, Group Six walianza ujenzi na walipeleka malipo ya awali ya ujenzi Januari 31, 2018 huku mteja wake huyo akitekeleza sehemu ya mkataba kwa kulipa kiasi cha Sh51.92 milioni, malipo ambayo yana kithibitisho kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kuhusu mteja wake kuwa na uhusiano wa karibu na mlalamikaji, alisema, "mteja wangu na mtu ambaye kwenye mitandao amekuwa akizungumza kwamba anamiliki eneo hilo, mteja wangu katika kipindi anachozungumza huyo mtu cha mwaka 2012 alikuwa hamfahamu kabisa huyo mtu."

"Mimi leo nathibitisha uhalali wa miliki, unaweza ukawa na uhusiano na mtu lakini sio wa kibiashara wa kuuziana na kuhamishiana miliki licha ya kuingia katika makubaliano ya kuhamishiana miliki,"

Mgongolwa alisema kufahamiana na mtu ni jambo lingine na miliki ni jambo lingine, hivyo ushahidi wa vielelezo kisheria unakingwa na vielelezo hivyo, ambaye anasema ni eneo lake aweke wazi vielelezo vya kisheria.

"Tunatoa changamoto kwa mtu yoyote yule aje akinzane na vielelezo vyetu, huu ni ujenzi kwa mujibu wa mkataba na haujasimamiwa na mjomba au shangazi," amesema Mgongolwa.

Alisema yeye yuko radhi kumsikiliza ili wakapambane, alisema kama kuna mtu anadhani anayo haki katika umiliki huo, lakini kwa sasa hawatafanya chochote na endapo ataendelea na matukio hayo hivyo basi ngazi za kisheria zitafuatwa.

"Hata tunaondokana na hisia tunaenda na uhalisia, yoyote yule anayesema aridhi ni ya kwake iwe kimahusiano au lah, aje na vielelezo kwetu, mtu mwenye dhana tofauti milango ya kimahakama iko wazi, ila kwa sasa hawatakwenda mahakamani," amesema Mgongolwa na kuongeza kuwa wajibu wangu kama mwanasheria ni kuthibitisha umiliki halali kwa mteja wangu.

"Hatua tutakazozichukua kuanzia sasa itategemea na matukio ambayo yatafuata kwani ndiyo yatatupa mwongozo wa nini tukifanye, ikitokea hatua ya kwenda mahakamani tutakwenda, ikitokea kuangalia ngazi nyingine tutalipeleka kwa kuwa maelekezo yetu yako wazi tunatakiwa kulinda haki ya teja wetu sambamba na jina lake," amesema.

Source: Mwananchi
Hii issue ukimwangalia Baashite unaona wazi ana akili kama za wale madada wanaopewa funguo za gari bila kadi!!
 
Bashite kapoteza Pambano Dakika za Awali kabisa
 
Back
Top Bottom