Makonda: Ghalib usinilazimishe kusema uozo wako, achia mali yangu. Walioko nyuma yako nawajua

Makonda: Ghalib usinilazimishe kusema uozo wako, achia mali yangu. Walioko nyuma yako nawajua

Kwenye hili sakata la aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar na GSM yataibuka mengi Leo Makonda katishia kusema maovu ya GSM hii inaonesha wazi kuwa wote Wawili ni Matapeli wanajuana jinsi walivuokubaliana kufanya maovu yao.
Huenda GSM anafanya biashara za magendo ambazo Makonda anazijua ila alikuwa kamfichia madhambi yake. Acheni vyuma viumane[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa anajambia mbali halafu bado anaonekana kujisaha na huo uccm kwa ufupi wanaokupa kichwa ndio hao hao wanapanga kukuangusha bro ningekuwa mimi ndio wewe tangu Magu alivyodanja tu ningeuza kila kitu nikatimkia zangu canada kuomba hifadhi.
 
Kwenye hili sakata la aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar na GSM yataibuka mengi Leo Makonda katishia kusema maovu ya GSM hii inaonesha wazi kuwa wote Wawili ni Matapeli wanajuana jinsi walivuokubaliana kufanya maovu yao.
Huenda GSM anafanya biashara za magendo ambazo Makonda anazijua ila alikuwa kamfichia madhambi yake. Acheni vyuma viumane[emoji23][emoji23][emoji23]
Makonda alikuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ambao GSM anafanya biashara kama leo makonda atasema GSM anafanya maovu wakati alishawahi kuwa mkuu wa ulinzi katika mkoa huu na hakumchukulia hatua itakuwa anajifedhehesha mwenyewe
Hakuweza kimuajibisha pale alipokuwa na nguvu hivyo ni bora akae kimya
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
salehjembefacts_2792453760849943572_3442463079_0_1070x1109.jpg
 
Hizo mali kapataje hali ni mtumishi na mshahara wake unajulikana
.Achunguzwe
 
Makonda alikuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ambao GSM anafanya biashara kama leo makonda atasema GSM anafanya maovu wakati alishawahi kuwa mkuu wa ulinzi katika mkoa huu na hakumchukulia hatua itakuwa anajifedhehesha mwenyewe
Hakuweza kimuajibisha pale alipokuwa na nguvu hivyo ni bora akae kimya
Ni kweli ila aiunajua Makonda ni akili ndogo? Yeye anadhani atapata unafuu kwa kuanika uozo wa GSM.
 
Hakuna tajiri msafi..GSM anakulikana kwa madhambi yake toka home shopping centre..hoja dhaifu Sana kwa makonda. Hoja hiyo haiwezi kuondoa asionyeshe document ya umiliki. Makonda analia Lia Lia tu..huko mbele atakumbana na kesi ya utapeli au uvamizi au kutumia madaraka vibaya..Bora aachie tu kiwanja..msipe moyo kwa hili linaweza mpeleka ndani kiurahisi sana

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hii haileti maana yeyote kama Makonda hatoonesha vielelezo vya kumiliki eneo linalo gombaniwa!
 
Kwenye hili sakata la aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar na GSM yataibuka mengi Leo Makonda katishia kusema maovu ya GSM hii inaonesha wazi kuwa wote Wawili ni Matapeli wanajuana jinsi walivuokubaliana kufanya maovu yao.
Huenda GSM anafanya biashara za magendo ambazo Makonda anazijua ila alikuwa kamfichia madhambi yake. Acheni vyuma viumane[emoji23][emoji23][emoji23]
Kutishia kusema maovu ya mtu ni blackmail.

Kosa la kufaa kumshtaki anayesema anatishia kusema maovu.

Kama mtu ana maovu, yaseme tu.

Usiyatumie kama mtaji wa kumtisha.

Makonda anafanya blackmail.
 
Mimi sijali kama huyo GSM ni msafi au sio msafi .. ninachotaka ni makonda alipe kwa ushenzi aliofanya.. kuanzia kumpiga kofi mzee wetu Walioba hadi kuvamia studio za Clouds..

Hata kama atalipa kwa kosa ambalo hajafanya lakini alipe tu. Ili iwe fundisho kwa watu waliopo kwenye uongozi au watakaokuja kupata uongoz kwamba ukiwa kiongozi sio kwamba una akili kuliko wote unaowaongoza
 
Inaonesha kuwa hayo mabaya anayoyajua dhidi ya GSM ndio alitaka kuyatumia kum black mail ili amjengee nyumba ... kwa mamlaka aliyokuwa nayo kwanini hakumuwajibisha GSM?
 
Bashite bana..

Sasa "uozo" wa GSM unahusiana nini na kiwanja tajwa? 😀😀

Asichofahamu kutisha (coercison ama blackmail) pia ni kosa kisheria, tena kubwa zaidi...
Kweli kibao kimegeuka. Sasa Makonda kaishia kuwa mtu wa “kutishia kuanika uozo” wa mbaya wake!
 
Wakati Makonda akijiita Rais wa Dar es Salaam na Mkuu wa wakuu wa mikoa yote ya Tanzania alijionesha kama Sehemu ya Matajiri wa Bongo waliozaliwa na kukulia katika jiji la wenyewe jiji la Dar es salaam.Hata Juzi wakati Gharib alipofiwa na baba yake,Makonda alionekana hadharani wakati wa maziko ingawa alionekana kabisa yupo sehemu ambayo hakutakiwa.

Mimi binafsi Makonda ni mmoja kati ya watu amao niliwadharau sana.Kwangu mimi Makonda alikuwa jogoo wa Shamba aliyekuwa natajaribu kuwika mjini.Alikuwa mwenye tamaa nyingi,kiburi kikubwa majivuna pamoja na umbumbu na ulimbukeni wa madaraka.Alikuwa kiongozi mwenye upeo mdogo sana na mara chache alipojaribu kufanya jambo sahihi nyuma ya pazia alikuwa akifanya uozo mkubwa sana.

Katika historia ya dunia na siasa za Tanzania Makonda hakuwa na jambo la kipekee la kujivunia zaidi ya kuwa ni mtu wa kujikomba na kujipendekeza na opportunist ambaye hakuwa na aibu wala heshima binafsi.Makonda huyu ambaye analia kwamba anaonewa na kudhulumiwa alikuwa ni dhulmati asiyekuwa na aibu na ambaye alidiriki hata kuwadhulumu wale ambao walimheshimu na kumpenda.Makonda alimzunguka hayatiMagufuli na kumuingiza katika majaribu mengi sana kiasi kwamba mpaka JPM anaifariki dunia Makonda alikuwa ni mmoja kati ya watu waliochangia kumchafua sana JPM akifuatiwa na Yule jamaa aliyepata mvua 30 na yule anayemiliki timu ya mpira.

Swali langu la kujiuliza leo ni je Ushoga wa Makonda na GSM umefia wapi?Au ndo kama walivosema wahenga Kila zama na kitabu chake?

Makonda Pumzika kwa amani na usitafute huruma ya umma maana kwa Tanzania sisi wewe utabaki stori tu,Jiandae maana bado kuna watu wanataka kujua ile minazi uliyotoa Dar ukapeleka mwanza kama imeota.

Tulia tu dawa iingie vizuri kwa sasa.Mwisho wa yote umethibitisha ukweli wa kwamba madaraka ni koti la kuazima.Kubali yaishe UJIPANGE UPYA
 
Back
Top Bottom