Makonda: Ghalib usinilazimishe kusema uozo wako, achia mali yangu. Walioko nyuma yako nawajua

Makonda: Ghalib usinilazimishe kusema uozo wako, achia mali yangu. Walioko nyuma yako nawajua

ungekuwa unaelewa mambo ya mahakamani ungejua kuwa anayetakiwa kwenda mahakamani hapo ni bashite. GSM aende kufanya nini wakati yeye kila kitu kinatambulika na sheria? hati inasoma jina lake, vielelezo vya ujenzi n.k, bashite asipoenda ndio anapoteza haki yake, ila gsm asipoenda hapotezi kitu kwasababu haki yake tayari ipo mkononi mwake. hata kesho akimtibua bashite ni haki yake kwasababu eneo linasoma umiliki wake. kwahiyo bashite ndio anasubiriwa aende mahakamani.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Eti Ningejua Mambo Ya Mahakamani, Mzee Niko Kwenye field ya Sheria zaidi ya 20yrs

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi ilikua inaongozwa na cartels, sasa ndio tunaona madhara yake.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Eti Ningejua Mambo Ya Mahakamani, Mzee Niko Kwenye field ya Sheria zaidi ya 20yrs

Sent using Jamii Forums mobile app
kama upo kwenye field ya sheria, gsm anaenda mahakamani kudai nini hapo? kama kweli wewe ni mwanasheria. na bashite akiendelea kukaa hivyo umiliki atakuwa nao? kati ya bashite na gsm nani anatakiwa kwenda mahakamani, ongea kama mwanasheria. ukijibu hili swali nitakushukuru.
 
Mm Sio Mwanasheria

Muulize wakili wake Alex Mgongolwa ambae anadai mteja wake amemtuma aje public kueleza dhamira yao ya kwenda mahakamani.
 
Muulize wakili wake Alex Mgongolwa ambae anadai mteja wake amemtuma aje public kueleza dhamira yao ya kwenda mahakamani.
hujamsikiliza vizuri, amesema ataend amahakamani kufungua defamation kwa wale watakao chafua jina la mteja wake, hawatarajii kwenda mahakamani kutafuta umiliki wa ardhi hiyo kwasababu inasoma kw ajina lao na kuna nyaraka zote za umiliki. sasa wakienda mahakamani wanaenda kutafuta nini? si hata mahakama itawashangaa? yule ambaye jina lake halisomi, na hana hati ndio anatakiwa kwenda mahakamani kueleza kama kuna sababu yeyote inayoweza kuifanya mahakama imtambue kama mmiliki. hata asiye mwanasheria anajua hili.
 
Watoto wa marehemu wameanza kuteswa.. anyway yatima hadeki. Na bado tunasubiri mwenye jina lake aje kulidai ili abaki kiwa Bashite.
 
Namshauri Makonda amtafute Lissu ili asimamie kesi la sivyo kwenye hii kesi hatoboi
 
Naam Uozo Usemwe na walio nyuma yake wasemwe na wote waliokosea hata ikiwemo wewe (Makonda) sheria ifuate mkondo wake muwajibike..., Huenda kufichiana Uozo ndio kulipelekea wewe kupewa hicho kiwanja

Hii nchi haipaswi kuendeshwa kimafioso

The biggest looser hapa ni Tanzania kama nchi..., yaani hii nchi imekuwa kama Telenovella
Nae walioko nyuma yake ni akina nani?ni kwa nini hii serikali inawalinda majangili wanaotamba kama akina makonda?
 
View attachment 2148028
Wakati Wakili wa mfanyabiashara maarufu nchini, Ghalib Said Mohamed (GSM), Alex Mgongolwa ameweka wazi vielelezo vya umiliki wa eneo kiwanja namba 60 lililopo Regent Estate Kinondoni jijini hapa, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemtaka mfanyabiashara huyo kumwachia mali yake.

Mzozo wa kiwanja hicho umeibuka hivi karibuni, ambapo Makonda ameonekana katika video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii akisisitiza kuwa eneo hilo ni lake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Machi 12, 2022 jijini hapa Wakili Mgongolwa amemtaka mtu ambaye hakumtaja kwa jina, kuweka wazi vielelezo alivyonavyo vya umiliki wa eneo hilo na vielelezo kutoka Wizara ya Ardhi vinavyompa uhalali wa kulimiliki.

Hata hivyo, Makonda alipotafutwa kwa simu leo, amejibu kwa ujumbe wa WhatsApp, akisema; “GSM usinilazimishe kusema uozo wako achia mali yangu. Walioko nyuma yako nawajua.”

Kama hiyo haitoshi, katika ukurasa wake wa Instagram, Makonda aliweka video ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka ambayo pamoja na mengine alieleza haja ya kutaka Jeshi la Polisi kuchunguzwa, kisha akaweka ujumbe:

“Naunga mkono hoja ya Kamati Kuu, ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi, wanaolipaka tope Jeshi la Jolisi kwa kuwalinda wafanyabiashara MATAPELI wanaodhulumu mali za watu. Naomba tuanze na Dar es salaam na mimi Paul Makonda niko tayari kutoa ushirikianao.”

Madai ya GSM
Akifafanua zaidi kuhusu umiliki wa ardhi hiyo, Wakili Mgongolwa amesema, mteja wake Ghalib Said Mohamed alinunua ardhi wilaya ya Kinondoni, eneo la Regent Estate plot no. 60, title no. 186153/60, kwa lengo la ujenzi wa makazi Novemba 21, 2006."

Vilevile, Mgongolwa amesema Septemba 2017, mteja wake aliingia mkataba na kampuni ya ujenzi iitwayo Group Six International (Contract Class One) kwa ajili ya ujenzi wa eneo hilo wenye thamani ya Sh640 milioni.

"Ghalib aliomba kibali cha ujenzi na manispaa ya Kinondoni walitoa kibali hicho Oktoba 16, 2017 chenye kumbukumbu namba 00020032 kwa Ghalib Said Mohammed kwa ajili ya ujenzi eneo hilo," amesema.

Ameongeza kuwa baada ya kibali hicho kutoka, Group Six walianza ujenzi na walipeleka malipo ya awali ya ujenzi Januari 31, 2018 huku mteja wake huyo akitekeleza sehemu ya mkataba kwa kulipa kiasi cha Sh51.92 milioni, malipo ambayo yana kithibitisho kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kuhusu mteja wake kuwa na uhusiano wa karibu na mlalamikaji, alisema, "mteja wangu na mtu ambaye kwenye mitandao amekuwa akizungumza kwamba anamiliki eneo hilo, mteja wangu katika kipindi anachozungumza huyo mtu cha mwaka 2012 alikuwa hamfahamu kabisa huyo mtu."

"Mimi leo nathibitisha uhalali wa miliki, unaweza ukawa na uhusiano na mtu lakini sio wa kibiashara wa kuuziana na kuhamishiana miliki licha ya kuingia katika makubaliano ya kuhamishiana miliki,"

Mgongolwa alisema kufahamiana na mtu ni jambo lingine na miliki ni jambo lingine, hivyo ushahidi wa vielelezo kisheria unakingwa na vielelezo hivyo, ambaye anasema ni eneo lake aweke wazi vielelezo vya kisheria.

"Tunatoa changamoto kwa mtu yoyote yule aje akinzane na vielelezo vyetu, huu ni ujenzi kwa mujibu wa mkataba na haujasimamiwa na mjomba au shangazi," amesema Mgongolwa.

Alisema yeye yuko radhi kumsikiliza ili wakapambane, alisema kama kuna mtu anadhani anayo haki katika umiliki huo, lakini kwa sasa hawatafanya chochote na endapo ataendelea na matukio hayo hivyo basi ngazi za kisheria zitafuatwa.

"Hata tunaondokana na hisia tunaenda na uhalisia, yoyote yule anayesema aridhi ni ya kwake iwe kimahusiano au lah, aje na vielelezo kwetu, mtu mwenye dhana tofauti milango ya kimahakama iko wazi, ila kwa sasa hawatakwenda mahakamani," amesema Mgongolwa na kuongeza kuwa wajibu wangu kama mwanasheria ni kuthibitisha umiliki halali kwa mteja wangu.

"Hatua tutakazozichukua kuanzia sasa itategemea na matukio ambayo yatafuata kwani ndiyo yatatupa mwongozo wa nini tukifanye, ikitokea hatua ya kwenda mahakamani tutakwenda, ikitokea kuangalia ngazi nyingine tutalipeleka kwa kuwa maelekezo yetu yako wazi tunatakiwa kulinda haki ya teja wetu sambamba na jina lake," amesema.

Source: Mwananchi

Ujinga huwezi kushinda kesi kwa kupitia CCM wakati huna vibali vya umiliki . Raisi hataweza kuongilia maswala kama haya wakati inaelekea GSM wana vibali vyote, wamefuata sheria na kulipa kodi zote. Lakini wametumia mkandarasi! Raisi Samia hata weza kumbyanganya mtu haki zake ili tu amfurahishe Makonda! GSM smart wame weka wakili 🙏 sasa Makonda anatakiwa kujibu na wakili sio WhatApp na sasa Mtoto wa Kikwete ambaye ni rafiki wa GSM ni waziri🤔.

Wito kwa vijana fanyeni kazi siasa sio kazi ni wito na ule utamaduni wa kizamani wa kufikiria utapata pesa kwenye siasa kwa rushwa umepitwa na wakati. Mitandao, kili na uchawa sio biashara
 
hujamsikiliza vizuri, amesema ataend amahakamani kufungua defamation kwa wale watakao chafua jina la mteja wake, hawatarajii kwenda mahakamani kutafuta umiliki wa ardhi hiyo kwasababu inasoma kw ajina lao na kuna nyaraka zote za umiliki. sasa wakienda mahakamani wanaenda kutafuta nini? si hata mahakama itawashangaa? yule ambaye jina lake halisomi, na hana hati ndio anatakiwa kwenda mahakamani kueleza kama kuna sababu yeyote inayoweza kuifanya mahakama imtambue kama mmiliki. hata asiye mwanasheria anajua hili.
Ni aina Gani ya Defamation Alex Mgongolwa anayozungumzia?
.
Je ni Defamation ya kudumu Kwa Maana ya libel-Defamation in permanent form
.
Au ni Defamation ya muda Kwa Maana ya slander-Defamation in temporary form?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu si ndo alifiwa juzi? Na makonda akaenda msibani? Kwahiyo walivyopeana pole akakumbuka kiwanja chake?
 
Naam Uozo Usemwe na walio nyuma yake wasemwe na wote waliokosea hata ikiwemo wewe (Makonda) sheria ifuate mkondo wake muwajibike..., Huenda kufichiana Uozo ndio kulipelekea wewe kupewa hicho kiwanja

Hii nchi haipaswi kuendeshwa kimafioso

The biggest looser hapa ni Tanzania kama nchi..., yaani hii nchi imekuwa kama Telenovella
Na Makonda akiwa sehemu ya uozo huo. Kuna wakati maisha yanatuonyesha maajabu makubwa sana.
Kama ningelikuwa sijaona baadhi ya uozo....
 
Ni aina Gani ya Defamation Alex Mgongolwa anayozungumzia?
.
Je ni Defamation ya kudumu Kwa Maana ya libel-Defamation in permanent form
.
Au ni Defamation ya muda Kwa Maana ya slander-Defamation in temporary form?.

Sent using Jamii Forums mobile app
ametoa warning, kabla hujajadili tafadhali nenda youtube sikiliza ile clip ndio uje hapa. naona wewe ni mgeni. ametoa warning tu kwamba wapo macho kuangalia mtu yeyote atakayeadhiri reputation ya mteja wao wanaweza kuelekezwa waende mahakamani, na hiyo ndio kazi yao. lakini hadi sasa hawajaelekezwa kufanya hivyo. its just a warning.
 
Back
Top Bottom