Makonda: Hakuna nilichojifunza, nitawanyoosha. Wasiopaka rangi nyumba zao katikati ya Mji TUTABOMOA

Huyu bwana umtake usimtake utamripot tu habar zake hahaha nikiripoti kutoka jf mimi ni erythrocyte kutoka chadema kwasasa nikiwa mkoa wa arusha kulipoti taarifa za makonda kutoka ccm, ujumbe maendeleo hayana chama
Yaani nimeshangaa sana asee, jamaa kakomaa kabisa na story ya Makonda wakati CDM wana uchaguzi za kanda huko.

Badala atuandikie malengo ya viongozi wa kanda anadinkidinki na PCM 😂!
 
Hii ilikua moshi siku ya mwenge moshi wanja ulipendeza sana hongereni wana moshi kwa ujumla
 
Japo mi si timu yake ila kwenye kuboresha usafi wa jiji, kupaka rangi majengo mjini kati na kuleta sijui mabasi ya ghorofa hapo kapatia, alichosahau ni kukamia kuondoa mirungi na bangi zilizojaa mjini maana inaharibu akili za vijana hadi kujifanya hamnazo "wadudu"!!

Mbona hakuzungumzia uwanja mpya wa michezo unaojengwa au sio kipaumbele?

Arusha lazima waombe poo!! Wengine itabidi wahamie Burundi maana saa hizi ni mwendo wa kwata tu huko!

Ukweli usemwe Bimkubwa kapatia sana uteuzi kumpeleka jombaa Arusha akawachangamshe watu wote hasa wadudu!!
 

Nakubaliana naye kwenye kupafanya Arusha pavutie kwa watalii.Vitu vinne vikubwa kwa utaliii ni 1) USALAMA 2) USALAMA 3)USALAMA 4)Miundombinu rafiki.

Nashauri makonda afanye study tour hapo kwa Kagame.atapata cha kujifunza cha kumsaidia kufanya mageuzi ya jiji la Arusha.
 
Asubuhi nilikuwa napitapita hapa nawaona mademu( teenage )smarter than usual katika mavazi yao. Nikafikiria labda hii inahusiana na Makonda.
Lakini huyu ni Makonda mpya---- nyumba zipakwe rangi.
 
Hata ufisadi wa Richmond wajinga kama ninyi mulituaminisha kuna backup ya system
 
Huyu ndio PAULO MAKONDA haniangushi , ni chizi na hii nchi inahitaji machizi.
 
Swadakta
 
Arusha wamewadharau sana wamewaletea mwehu awe mkuu wa mkoa!!!
 
Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda amezungumza mambo kadhaa wakati wa hafla ya kukadhiwa ofisi, iliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, Jumatatu Aprili 08.2024

"Naomba sana ushirikiano wenu, mnionyeshe upendo zaidi, bahati niliyonayo mimi ni kwamba naweza kuwa mtu yeyote mnayemtaka, hiyo ndio kitu pekee ambayo huwa namshukuru Mungu, yaani mimi naweza kujifunza nikawa kiongozi wa aina yoyote.

Ukitaka kiongozi anayekaa na Baba Kadinali Pengo tutasoma sala nitakuwa, ukitaka kiongozi anayekaa na 'General' tukaenda kwa kwata nitakuwa, kokote ambako ninyi mtataka na mimi nitakuwa hivyo, kwa hiyo nitabadilika kutokana na mahitaji yenu na speed tutakayokuwanayo.

Kwa hiyo mahitaji yenu yakiwa ni makubwa na mimi nitaenda kwa speed hiyo, mahitaji yenu yakiwa ni kidogo kidogo nitashindwa kwenda kwa speed kubwa kwa sababu nisiende peke yangu.

Kwa hiyo ni speed yenu tu, mkitaka mji upendeze, mkitaka Arusha ibadilike iwe ni mji wenye amani na utulivu ambapo hata mwananchi anaweza akasahau simu yake mahala akaitiwa itakuwa hivyo, mkitaka Arusha uwe mji wa kibiashara ili wafanyabiashara wetu wapate wafanye biashara zao hadi usiku wa manane itakuwa" alisema Paul Makonda.
 
Huyo kijana alitumika kuzima mjadala wa kuuzwa bandari zetu alipoteuliwa,

Hivi sasa pia anazima Ripoti ya CAG haijadiliwi tena.

Huo uchawi una mwisho.

Tusubiri.
 
Hayo ya Makonda, ngoja Erythrocyte wa CHADEMA aendelee kufanya u MC.

Ila mimi nitoe shukurani. Asante kwa picha, nitahakikisha inatumika kwa haki na wakati muafaka.

Wadada zetu wanapendeza kweli kweli.

Kidumu
 
Ndege wanaofanana mbawa huruka pamoja.
Hongera kwa mteuzi na mteule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…