Pre GE2025 Makonda: Harusi yoyote itakayofungiwa Arusha Serikali ya mkoa italipia ukumbi

Pre GE2025 Makonda: Harusi yoyote itakayofungiwa Arusha Serikali ya mkoa italipia ukumbi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hakuna fedha zetu! Hizi ni kodi za wananchi wa nchi hii wote!

Basi kama vipi kodi zote mnazolipa wapewe viongozi na watoto wao kama ni sawa tu kula hela
Asa na wanaofunga ndoa c wananchi pia mbona hutk walipiwe izo ela unataka kutumia kwenye barabara tuh mkuu
 
Asa na wanaofunga ndoa c wananchi pia mbona hutk walipiwe izo ela unataka kutumia kwenye barabara tuh mkuu
Wapi wananchi wamesema hela zetu zikalipie ndoa za watu? Kwenye bajeti iliyopitishwa bungeni ulisikia kuna fungu la kwenda kulipia ndoa za watu likipitishwa kwenye bajeti ya Tamisemi?
 
Kwa hiyo shida ya wananchi kwa sasa ni vijana kuoa?

Wananchi wamekubali fedha zao kwenda kushughulikia vijana kuoa?
Hana uwezo wa kulipia ndoa yoyote, bali alikuwa anapiga domo kutaka kiki za siasa za kitoto.
 
Ameanzisha huo mfuko?

Kwa nini asingesema nitaanzisha mfuko?

Kwa nini akasema kwa gharama za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa?
Muulize mleta mada. Mimi nimeongelea tu njia za mkuu wamkoa anazoweza kufanya kuzalisha pesa, na napingana na hoja kuwa anatumia pesa za kodi kulipia watu gharama za harusi.

Akianzisha mfuko wakwepa kodi wengi watajipendekeza. Wana pesa hazina kazi.
 
Muulize mleta mada. Mimi nimeongelea tu njia za mkuu wamkoa anazoweza kufanya kuzalisha pesa, na napingana na hoja kuwa anatumia pesa za kodi kulipia watu gharama za harusi.

Akianzisha mfuko wakwepa kodi wengi watajipendekeza. Wana pesa hazina kazi.
Kwa nini unapingana na hoja wakati kwa maneno yake amesema zitagharamiwa na Ofisi yake?
 
Hana uwezo wa kulipia ndoa yoyote, bali alikuwa anapiga domo kutaka kiki za siasa za kitoto.
Accounting Officer wa Mkoa ni RAS. Mkuu wa Mkoa hana uwezo wa kuidhinisha malipo yeyote. RAS akiidhinisha itabidi aseme yalipwe kutoka fungu lipi! Na akifanya upuuzi huo Audit Querry zitamfuata. RAS anayejitambua atamtolea nje.

Amandla...
 

Narudia tena, endapo Viongozi wa Tanzania wangekuwa na nidhamu kwenye matumizi ya kodi za wananchi, inawezekana kabisa Tanzania ingekuwa nchi ya uchumi wa juu pekee katika bara hili la Afrika.

Viongozi wa nchi hii wanachukulia kama pesa za Serikali ambazo ni kodi za wananchi ni pesa zao binafsi ambapo wanaweza kuzifanyia chochote wanachowaza wakati wowote ule.

Ndo mana leo tunaona kodi za wananchi zikitumia hovyo bila huruma ilihali nchi yetu ikiendelea kukopa kila siku na kuwa na huduma zisizoridhisha karibu kila sekta.

Jana Mkuu wa Mkoa wa Arusha ametangaza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itagharamia harusi zitakazofungwa Arusha. Ikumbukwe pesa zinazosemwa ni kodi za wananchi, fedha ambazo zinatakiwa kuhakikisha barabara zote za mitaani Mkoani Arusha kuwa za lami, shule zote kuwa na miondombinu sahihi pamoja na vitabu.

Fedha hizo ndizo zinatakiwa kuhakikisha kila hospitali na zahanati Arusha zina dawa za uhakika na wananchi wanapata huduma zote za msingi.

Narudia tena kuwakumbusha wana CCM wenzangu. Ulaya tunayoiona leo haikutokea kwa bahati mbaya ila kwa nidhamu katika matumizi ya kodi za wananchi. Mnaposafiri kwenda China, Ulaya na Marekani na kupiga picha kwenye barabara nzuri, miundombinu mizuri na hata kwenda kutibiwa kwenye hospitali nzuri vile vyote havijatokea kwa bahati mbaya ila ni kutokana na wenzetu wale kuwa na nidhamu kubwa kwenye matumizi ya kodi za wananchi.

Tusitamani ifike mahala Watanzania wagome kulipa kodi au waandamane kutaka Viongozi muondoke kwenye nafasi zenu ndo mjifunze kuwa kodi za wananchi sio za kutumiwa hovyo hovyo kama mnavyojiskia

Akili ni nywele, kila mtu ana zake!

Lord Denning
Qatar
Vitu vingine ni vya kusoma na kuachana navyo kama vilivyo.
Ndio maana kila iitwapo leo wanasiasa wanaendelea kutawala fikra za watu,na watu nao pasipo kujua wanaingia King.
 
Nafikiri bora wangejenga Ukumbi wa serikali na anaetaka analipia gharama zake ila ukumbi bure
Kuelekea uchaguzi mtasikia mengi
Hata polisi wanaoshewa magari sasa
Nchi ina vituko
 
Huu ni upuuzi ambao umejaa fikra za kijinga sana. Yaani uchumi wa Jiji la Arusha kuchochewa na mzunguko wa pesa utokanao na idadi kubwa ya harusi zinazofungwa!?

Vipi kuhusu sekta za utalii na ile ya madini!? Arusha miaka nenda rudi imepata umaarufu wake kupitia sekta hizi. Naamini hapa ndipo alipaswa kuja na ubunifu mpya ili kuchochea maendeleo zaidi
Nje ya hapo ni kutaka kujichoresha tu. Unaacha kutafuta nyama za mnofu, unaanza kupoteza muda ili kuhangaika na
utumbo!? Very low thinking 😩
Punguza wivu.....,na makasiriko. Hiyo ni hatua mojawapo unaweza kumshauri nyingine unayoona inafaa
 
Back
Top Bottom