Pre GE2025 Makonda: Harusi yoyote itakayofungiwa Arusha Serikali ya mkoa italipia ukumbi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Screenshot_20231102_120808_Remix.png
 
Aahh. Siwezi ongea mie nina hasira, kuanzia leo mie nawe ni paka na panya, uadui wetu ni zaidi ya mbea aliyeenda kumwambia mke wangu nipo lodge fulani na mchepuko 🤣😂
Kumbe shekhe unachepukaga🥸
Mke ulimpata kwa shida halafu unamletea drama! Unazingua
 
Land Rover
Masai
Harusi

Huyo ndiyo BASHITE anapenda MAKIKI kama msanii.
 
Hivi kuna tamko la makonda lilishawahi kufanikiwa consistently maana waalimu tu waliendelea kulipia nauli za daladala!!..

Hata hivyo wacha niwaache wafu wazikane
 
Narudia tena, endapo Viongozi wa Tanzania wangekuwa na nidhamu kwenye matumizi ya kodi za wananchi, inawezekana kabisa Tanzania ingekuwa nchi ya uchumi wa juu pekee katika bara hili la Afrika.

Viongozi wa nchi hii wanachukulia kama pesa za Serikali ambazo ni kodi za wananchi ni pesa zao binafsi ambapo wanaweza kuzifanyia chochote wanachowaza wakati wowote ule.

Ndo mana leo tunaona kodi za wananchi zikitumia hovyo bila huruma ilihali nchi yetu ikiendelea kukopa kila siku na kuwa na huduma zisizoridhisha karibu kila sekta.

Jana Mkuu wa Mkoa wa Arusha ametangaza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itagharamia harusi zitakazofungwa Arusha. Ikumbukwe pesa zinazosemwa ni kodi za wananchi, fedha ambazo zinatakiwa kuhakikisha barabara zote za mitaani Mkoani Arusha kuwa za lami, shule zote kuwa na miondombinu sahihi pamoja na vitabu.

Fedha hizo ndizo zinatakiwa kuhakikisha kila hospitali na zahanati Arusha zina dawa za uhakika na wananchi wanapata huduma zote za msingi.

Narudia tena kuwakumbusha wana CCM wenzangu. Ulaya tunayoiona leo haikutokea kwa bahati mbaya ila kwa nidhamu katika matumizi ya kodi za wananchi. Mnaposafiri kwenda China, Ulaya na Marekani na kupiga picha kwenye barabara nzuri, miundombinu mizuri na hata kwenda kutibiwa kwenye hospitali nzuri vile vyote havijatokea kwa bahati mbaya ila ni kutokana na wenzetu wale kuwa na nidhamu kubwa kwenye matumizi ya kodi za wananchi.

Tusitamani ifike mahala Watanzania wagome kulipa kodi au waandamane kutaka Viongozi muondoke kwenye nafasi zenu ndo mjifunze kuwa kodi za wananchi sio za kutumiwa hovyo hovyo kama mnavyojiskia

Akili ni nywele, kila mtu ana zake!

Lord Denning
Qatar
Wapi alisema atatumia pesa za serikali?
 
Mkoa gani walimu wanalipa nauli za daladala?
Halafu kumbe hii kauli aliitoa Makonda?
Naonaga walimu hawalipi, muhimu kitambulisho cha kazi
 
Wapi alisema atatumia pesa za serikali?
Acha kujidhalilisha dada yangu! We una heshima yako humu na kuna uzi wako nimetoka kumsema mtu kwa kukutukana.

Unaelewaje mtu anaposema kwa gharama za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa?

Kuna pesa za mtu binafsi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa? Au wewe unaelewa pesa za Serikali ni za kwenye Mawizara tu?
 
Kinachosikitisha nikuona kua hiki ndio kichwa wanachoona kinaubunifu katika chama chao!!!!kuna kitu hakipo sawa kwetu
 
Acha kujidhalilisha dada yangu! We una heshima yako humu na kuna uzi wako nimetoka kumsema mtu kwa kukutukana.

Unaelewaje mtu anaposema kwa gharama za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa?

Kuna pesa za mtu binafsi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa? Au wewe unaelewa pesa za Serikali ni za kwenye Mawizara tu?
Ukiogopa kutukanwa JF hautaingia, hilo lisikupe shida.

Mkuu wa Mkoa ana njia nyingi za kupata pesa nje ya pesa za bajeti ya serikali, ni ubunifu tu.

Tusihukumu bila ya ushahidi, kwa kudhani tu.

Ikithibitika katumia pesa za Serikali kuwaozesha watu, mimi ni wa kwanza kumzozomokea, kwani mimi hata michango ya harusi huwa sitowi, napinga kabisa starehe za watu nikachangie wakati kuna mambo yangu chungu nzima ya kimaendeleo yananisubiri.

Lakini siwezi kumhukumu kwa kukisia tu.
 
Mkoa gani walimu wanalipa nauli za daladala?
Halafu kumbe hii kauli aliitoa Makonda?
Naonaga walimu hawalipi, muhimu kitambulisho cha kazi
Nakumbuka kipindi kile bhana makonda katoa kauli, sasa kuna teacher mmoja aligeuka na gari ila muda wa kutoa nauli akatoa kitambulisho 😁😁

Konda haelewi, anamuambia yule teacher akadai nauli kwa mkuu wa mkoa maana hawezi kupokea 200 kwa wanafunzi, free pass kwa maaskari na wajeshi. Na waalimu pia, sio biashara

Daladala zima likamuunga mkono ikiweml waalimu wengine waliotoa nauli. Teacher kusave issue akaanza kulia

"Waalimu tunanyanyasika, sisi ndo tunawafundisha kusoma A hadi Z na kuhesabu,ila mkikua mnatudharau, kazi zenu hizi ni sababu yetu". Konda haelewi ikabidi watu wamlipie yule teacher lakini bado alinung'unika safari nzima 😁😁
 
Ukiwa na akili kupinga kila kitu huwezi ukamuelewa makonda nini lengo lake ingawa ameliweka wazi lakini ndio dunia akili hazifanani
 
Ukiogopa kutukanwa JF hautaingia, hilo lisikupe shida.

Mkuu wa Mkoa ana njia nyingi za kupata pesa nje ya pesa za bajeti ya serikali, ni ubunifu tu.

Tusihukumu bila ya ushahidi, kwa kudhani tu.

Ikithibitika katumia pesa za Serikali kuwaozesha watu, mimi ni wa kwanza kumzozomokea, kwani mimi hata michango ya harusi huwa sitowi, napinga kabisa starehe za watu nikachangie wakati kuna mambo yangu chungu nzima ya kimaendeleo yananisubiri.

Lakini siwezi kumhukumu kwa kukisia tu.
Ana njia gani nyingi za kupata pesa?

Kwenye kuendesha Serikali hakunaga assumptions kuna facts.

Unaposema harusi zitagharamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inamaanisha fedha zitatoka kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na hizo ni kodi za wananchi. Maana hakuna pesa ya mtu binafsi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Kama kuna external funding unatakiwa ku declare pia. Maana kuna uwezekano criminal gangs zikatakatisha pesa zao kupitia Ofisi za Serikali!
 
Mkoa gani walimu wanalipa nauli za daladala?
Halafu kumbe hii kauli aliitoa Makonda?
Naonaga walimu hawalipi, muhimu kitambulisho cha kazi
Walimu wanalipa dala dala acheni kudanganyana watu.kama wanaojifungua,wajawazito wanalipia matibabu iwe walimu?miongozo ya serikali ni hewa hata mashuleni michango iko lukuki tu.mara mitihani mara hiki ni vurugu tupu.mm mwanangu yuko darasa la Saba anadaiwa 125k.hii serikali ni ya wazushi na waongo tu.
 
Ana njia gani nyingi za kupata pesa?

Kwenye kuendesha Serikali hakunaga assumptions kuna facts.

Unaposema harusi zitagharamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inamaanisha fedha zitatoka kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na hizo ni kodi za wananchi. Maana hakuna pesa ya mtu binafsi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Kama kuna external funding unatakiwa ku declare pia. Maana kuna uwezekano criminal gangs zikatakatisha pesa zao kupitia Ofisi za Serikali!
Akianzisha mfuko tu wa kusaidia wanaooana na kampeni za hapa na pale za kutunisha mfiuko, tosha kabisa.

Zipo harambee za kila namna.

Mkuu wa mkoa akisema, siku fulani tutafanya chakula cha jioni, tutapiga mnada nafasi za kukaa, faida yake itakwenda mfuko wa kusaidia vijana wanaooana, watu watajaa na nafasi isiwepo.
 
Ameanzisha huo mfuko?

Kwa nini asingesema nitaanzisha mfuko?

Kwa nini akasema kwa gharama za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa?
 
Kwa hiyo shida ya wananchi kwa sasa ni vijana kuoa?

Wananchi wamekubali fedha zao kwenda kushughulikia vijana kuoa?
Usitupangie na feza zetu bhn we hutak wananchi nao wale hela za serikali walau kidogo
 
Back
Top Bottom