Pre GE2025 Makonda: Harusi yoyote itakayofungiwa Arusha Serikali ya mkoa italipia ukumbi

Pre GE2025 Makonda: Harusi yoyote itakayofungiwa Arusha Serikali ya mkoa italipia ukumbi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Unathibitishaje mtu sio mkazi? Maana wachagga wengi wapo Dar
Machalii wa chuga wanajulikana hata aende marekani miaka 10 akirudi bado ni yechu yechu ,huoni ata dogo janja kabadilika kila kitu kasoro Meno
 
Swali kidogo, hivi ofisi ya mkuu wa mkoa wana power ya kukusanya mapato ya aina yeyote mkoani na kupanga budget zao wenyewe za maendeleo? na vipi ofisi ina power yeyote ya miradi ya maendeleo kama barabara au umeme etc namaanisha power ya pesa na utekelezaji, sijawahi kuelewa hizi ofisi zaidi ya siasa za usalama fake na kupokea wageni kazi yake ni nini hasa?
 
Kwa hiyo matatizo aliyoyaona RC ni wanandoa kukosa hela za ukumbi? Hizi akili ni za mtu anaepumua au za Yunusi wa Bungeni? Kuna tofauti gani na DC aliyeona shida kubwa wilayani kwake ni kunyanduana na akaenda kupiga chabo Minyanduano?
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda amesema sherehe ya harusi yoyote itakayokuwa inafanyika Mkoani Arusha na kuhusisha wasiokuwa Wakazi wa Mkoa wa Arusha, Serikali ya Mkoa chini yake itagharamia ukumbi popote ndani ya Mkoa huo ili kufanikisha harusi hiyo.

Makonda amesema hayo wakati akiongea na Wadau mbalimbali wa maendeleo Mkoani Arusha leo July 08,2024 ambapo amesema lengo ni kuvutia zaidi Wageni na Watalii kufika Mkoani Arusha ili kuwa chachu ya kukuza uchumi wa Mkoa huo.

“Lengo letu sisi ni hatutaki kuwa na high season au low season, tunataka kutengeneza shughuli na matukio mbalimbali kuhakikisha kuwa muda wote uchumi unakuwa na kuendelea ili Mama wa mboga, bodaboda na kila Mtu anufaike na ugeni unaofika hapa Arusha”

====

Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Wazimu wa watu.
 
Kitu asichojua makonda ni kwamba Harusi nyingi watu wanafanyia kwenye maeneo ambayo Bwana harusi ana wadau wake au marafiki zake, maana ndio wanamchangia na ndio wahufhuriaji, Harusi sio kama mkutano wa injili. Ni ngumu sana Mtu atoke Kigoma akafanyoie harusi arusha kisa tu atalipiwa ukumbi wa laki nne au tano.
 
Ukisikia ndoa ya kaka iko viwanja vya halmashaur ndio hii sasa😂
 
Aim mall msizidi 70,,
M mall pakibabe,, iko Moshono, au gari zenu hazina mafuta ya kufika Moshono 😂😂😂
Kwakua mimi nimeshakua forena toka dar, ndoa yetu itafungiwa huko nchi za mbali Chugastan.
 
Aim mall msizidi 70,,
M mall pakibabe,, iko Moshono, au gari zenu hazina mafuta ya kufika Moshono 😂😂😂
Najua hela ya mchango itapungua sababu ukumbi bure🤣 so itakayobakia tutaongezea mafuta

Sema wachuga mmeupiga mwingiiiiii
 

Narudia tena, endapo Viongozi wa Tanzania wangekuwa na nidhamu kwenye matumizi ya kodi za wananchi, inawezekana kabisa Tanzania ingekuwa nchi ya uchumi wa juu pekee katika bara hili la Afrika.

Viongozi wa nchi hii wanachukulia kama pesa za Serikali ambazo ni kodi za wananchi ni pesa zao binafsi ambapo wanaweza kuzifanyia chochote wanachowaza wakati wowote ule.

Ndo mana leo tunaona kodi za wananchi zikitumia hovyo bila huruma ilihali nchi yetu ikiendelea kukopa kila siku na kuwa na huduma zisizoridhisha karibu kila sekta.

Jana Mkuu wa Mkoa wa Arusha ametangaza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itagharamia harusi zitakazofungwa Arusha. Ikumbukwe pesa zinazosemwa ni kodi za wananchi, fedha ambazo zinatakiwa kuhakikisha barabara zote za mitaani Mkoani Arusha kuwa za lami, shule zote kuwa na miondombinu sahihi pamoja na vitabu.

Fedha hizo ndizo zinatakiwa kuhakikisha kila hospitali na zahanati Arusha zina dawa za uhakika na wananchi wanapata huduma zote za msingi.

Narudia tena kuwakumbusha wana CCM wenzangu. Ulaya tunayoiona leo haikutokea kwa bahati mbaya ila kwa nidhamu katika matumizi ya kodi za wananchi. Mnaposafiri kwenda China, Ulaya na Marekani na kupiga picha kwenye barabara nzuri, miundombinu mizuri na hata kwenda kutibiwa kwenye hospitali nzuri vile vyote havijatokea kwa bahati mbaya ila ni kutokana na wenzetu wale kuwa na nidhamu kubwa kwenye matumizi ya kodi za wananchi.

Tusitamani ifike mahala Watanzania wagome kulipa kodi au waandamane kutaka Viongozi muondoke kwenye nafasi zenu ndo mjifunze kuwa kodi za wananchi sio za kutumiwa hovyo hovyo kama mnavyojiskia

Akili ni nywele, kila mtu ana zake!

Lord Denning
Qatar
 
Back
Top Bottom