Pre GE2025 Makonda: Harusi yoyote itakayofungiwa Arusha Serikali ya mkoa italipia ukumbi

Pre GE2025 Makonda: Harusi yoyote itakayofungiwa Arusha Serikali ya mkoa italipia ukumbi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda amesema sherehe ya harusi yoyote itakayokuwa inafanyika Mkoani Arusha na kuhusisha wasiokuwa Wakazi wa Mkoa wa Arusha, Serikali ya Mkoa chini yake itagharamia ukumbi popote ndani ya Mkoa huo ili kufanikisha harusi hiyo.

Makonda amesema hayo wakati akiongea na Wadau mbalimbali wa maendeleo Mkoani Arusha leo July 08,2024 ambapo amesema lengo ni kuvutia zaidi Wageni na Watalii kufika Mkoani Arusha ili kuwa chachu ya kukuza uchumi wa Mkoa huo.

“Lengo letu sisi ni hatutaki kuwa na high season au low season, tunataka kutengeneza shughuli na matukio mbalimbali kuhakikisha kuwa muda wote uchumi unakuwa na kuendelea ili Mama wa mboga, bodaboda na kila Mtu anufaike na ugeni unaofika hapa Arusha”

====

Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kodi zetu sasa kulipia harusi! Ngoja niendelee kuvuta shuka labda GenZ wakisikia watanionea huruma.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema Serikali itagharamia kumbi kwa ajili ya harusi zitakazofungwa mkoani humo na maharusi wanaotoka nje ya jiji la Arusha ili kuvutia wageni na kukuza uchumi.

Amesema lengo ni kuongeza watu wengi ambao watasaidia kuongeza mzunguko wa pesa hivyo kukuza uchumi zaidi.
View attachment 3036819
Wakushi wa Mtwara wanakuja kufungia ndoa Arusha
 
Huu ni upuuzi ambao umejaa fikra za kijinga sana. Yaani uchumi wa Jiji la Arusha kuchochewa na mzunguko wa pesa utokanao na idadi kubwa ya harusi zinazofungwa!?

Vipi kuhusu sekta za utalii na ile ya madini!? Arusha miaka nenda rudi imepata umaarufu wake kupitia sekta hizi. Naamini hapa ndipo alipaswa kuja na ubunifu mpya ili kuchochea maendeleo zaidi
Nje ya hapo ni kutaka kujichoresha tu. Unaacha kutafuta nyama za mnofu, unaanza kupoteza muda ili kuhangaika na
utumbo!? Very low thinking 😩
Sikiliza hiyo video mpaka mwisho sio unasoma tu kichwa cha habari unaanza kupinga. Punguza akili mbovu hasi zenye kupinga hata kile usichokifahamu kwa kina.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema Serikali itagharamia kumbi kwa ajili ya harusi zitakazofungwa mkoani humo na maharusi wanaotoka nje ya jiji la Arusha ili kuvutia wageni na kukuza uchumi.

Amesema lengo ni kuongeza watu wengi ambao watasaidia kuongeza mzunguko wa pesa hivyo kukuza uchumi zaidi.
View attachment 3036819
Hii ndio shida ya nchi kuongozwa na Darasa la Saba, Jiji la Arusha shule za hapo tu kati kati ya jiji zimechoka mbaya ila mjinga anakuja na mawazo ya kijinga jinga.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema Serikali itagharamia kumbi kwa ajili ya harusi zitakazofungwa mkoani humo na maharusi wanaotoka nje ya jiji la Arusha ili kuvutia wageni na kukuza uchumi.

Amesema lengo ni kuongeza watu wengi ambao watasaidia kuongeza mzunguko wa pesa hivyo kukuza uchumi zaidi.
View attachment 3036819
Ameshaandaa michongo ya kulipia mabest wake kwa fedha za Serikali.
 
Back
Top Bottom