Pre GE2025 Makonda: Harusi yoyote itakayofungiwa Arusha Serikali ya mkoa italipia ukumbi

Pre GE2025 Makonda: Harusi yoyote itakayofungiwa Arusha Serikali ya mkoa italipia ukumbi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda amesema sherehe ya harusi yoyote itakayokuwa inafanyika Mkoani Arusha na kuhusisha wasiokuwa Wakazi wa Mkoa wa Arusha, Serikali ya Mkoa chini yake itagharamia ukumbi popote ndani ya Mkoa huo ili kufanikisha harusi hiyo.

Makonda amesema hayo wakati akiongea na Wadau mbalimbali wa maendeleo Mkoani Arusha leo July 08,2024 ambapo amesema lengo ni kuvutia zaidi Wageni na Watalii kufika Mkoani Arusha ili kuwa chachu ya kukuza uchumi wa Mkoa huo.

“Lengo letu sisi ni hatutaki kuwa na high season au low season, tunataka kutengeneza shughuli na matukio mbalimbali kuhakikisha kuwa muda wote uchumi unakuwa na kuendelea ili Mama wa mboga, bodaboda na kila Mtu anufaike na ugeni unaofika hapa Arusha”

====

Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Hiyo pesa akasaidie watoto yatima wapo wengi waliokwama kuendelea na masomo kwa kukosa ada
 
dronedrake please achana na babycare tafuta hata lishangazi ukumbi ni bure mimi naahidi chakula, vinywaji, na usafiri,

mpiga tarumbeta Poor Brain @msherheshaji To yeye

role model@evelyn salt na Mbaga Jr

atakayekuja kusikiza kusikilizia wakati wa honey moon ni.......naogopa kumtaja
Mm ntakuwa upande wa vyakula 😎
 
Angefanya la maana kama angegharamia harusi nzima, wapo watu wengi kama Lucas hawajafunga ndoa sababu hawana hela, ukumbi ni kitu kidogo sana, hivi kweli unaweza kushawishika kufunga ndoa kwa vile umepata ukumbi wa bure?
 
Ndio maana mara nyingi nachangiaga huku kwamba hizi ofisi za wakuu wa mikoa zifutwe kwani hazina kazi mahsusi zinazofanya.
Wakuu wa mikoa wengi ni wakurupukaji sasa kama huyu ukimuuliza hizo fedha za kugharamia hiyo shughuli zimetengwa kwenye fungu lipi kwenye vote yake sidhani kama atakuwa na jibu.
Ifike mahali hizi ofisi zifutwe kwani hakuna la maana wanalofanya zaidi ya kutumia kodi zetu bila tija
 
Kuna mtu alileta uzi huku kwanini makonda ni mkuu wa mkoa mwenye hela na anaweka waziwazi kuliko wakuu wa mkoa wengine
 
Back
Top Bottom